NAYAJUA MATENDO YAKO.

NAYAJUA MATENDO YAKO.

Mara kadhaa, Bwana Yesu kabla hajasema Neno lolote alianza kwanza na kauli hii “Nayajua matendo yako” Kwamfano Soma vifungu hivi uone alivyosema, (Ufunuo 2:2, 2:19, 3:1, 3:8).

Nikwanini aanze kwa kusema hivyo? Ni kwasababu anataka hilo tuliweke akilini, tufahamu kuwa yupo karibu sana na hatua zetu kuliko tunavyoweza kudhani, hususani zile ambazo tunafikiri kuwa yeye hazijui, au hazioni.  Tutawaficha wanadamu lakini yeye kamwe hatuwezi kumficha chochote.

Wewe ni mchungaji, unazini na washirika, unazungumza lugha za mizaha na wake za watu, unadhani Kristo hajui nia yako, halafu unasimama madhabahuni unahubiri habari za wokovu..Bwana anakupa onyo, tena kali sana, anayajua matendo yako, na hasira yake ipo juu yako.

Wewe ni mkristo, unasema umeokoka, umebatizwa, unashiriki meza ya Bwana, lakini kwa siri unatazama picha za ngono, unafanya uasherati..Ukija kanisani unasema Bwana Asifiwe! Tena bila aibu unasimama na madhabahuni kuimba..utamficha mchungaji, utawaficha washirika wote, utamficha hata na shetani..Lakini Yesu anayajua matendo yako nje-ndani..Anajua mnapokutania, mnapotekelezea mipango yenu miovu, anajua ni nini unachofanya unapokuwa chumbani mwenyewe.

Wewe ni mwanandoa, unaigiza kwamba unampenda mwenzi wako, muwapo pamoja, lakini akisafiri kidogo tu, mkiwa mbali, unachepuka, mke umetoa mimba nyingi, na huko nje wewe mume umezaa watoto, hata mkeo haujui, unadhani unamficha  nani rafiki? .

Leo hii lipo kundi kubwa la washirikina  miongoni mwa watakatifu, tukiachilia mbali wachawi, lakini cha ajabu hujawahi kumsikia hata mmoja akijivunia kazi yake hiyo au akijitangaza? Wameficha hirizi chini ya biashara zao, wana mazindiko kwenye nyumba zao, wanajifanya wana maadili na hodari wa kusema AMEEN!!..Lakini hawajui kuwa Bwana anayajua matendo yao.

Ufunuo 3:1  “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. NAYAJUA MATENDO YAKO, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.

2  Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.

3  Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako”

Ndugu ni heri ukatubu, uwe na amani na Kristo katika nyakazi hizi za hatari, kwasababu ukiendelea na hali hiyo hiyo utakufa na kwenda kuzimu, na adhabu yako itakuwa ni kubwa sana.

Bwana anasema…

“Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema”. (Mithali 28:13)

Leo hii ziungame dhambi zako, usiyafiche moyoni hayo unayoyafanya, wala usione aibu, wakati ndio sasa, hata kama umeshindwa kuacha, au hujui cha kufanya kwa uliyoyatenda, embu mfuate kiongozi wako wa kiroho mshirikishe akupe ushauri,.aombe pamoja na wewe,  Ili Bwana akusamehe makosa hayo uliyoyofanya.

Unachopaswa kufanya ni kutubu tu kwa kumaanisha..Ukiwa na nia kweli ya kuacha, ili Bwana atakusamehe na kukusaidia kuyashinda, lakini ukiwa upo vuguvugu, hueleweki, bado unayo hatia ya dhambi..kwasababu anayajua matendo yako.

Ufunuo 3:15  “NAYAJUA MATENDO YAKO, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

16  Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa change”.

Jimimine kwelikweli kwa YESU akusaidie..Wakati wa Yesu kuyahukumu mambo yote ya sirini, umekaribia sana, Hukumu ipo karibu. Jiepushe nayo. (Warumi 2:16, 1Wakor 4:5). Ni wakati wa lala-salama.

Ikiwa utapenda kupata msaada huo wa kumkaribisha tena Kristo upya maishani mwako. Basi waweza wasiliana nasi kwa namba hizi kwa ajili ya mwongozo huo bure. +255693036618 / +255789001312.

Bwana akubariki.

Shalom. (Bwana Yesu anarudi).

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

KUONGOZWA SALA YA TOBA

NINI MAANA YA KUTUBU

TOFAUTI YA UBATIZO WA YOHANA NA UBATIZO WA BWANA YESU

SEMA KWA LUGHA NYINGINE.

Kupiga ramli ni nini katika biblia?

Kumwambia mtu mwenye dhambi kuwa atakwenda kuzimu asipotubu Je! ni kuhukumu?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
NEEMA ALICE
NEEMA ALICE
1 year ago

Amen nimebarikiwa sana kweli Mungu alinijua kabla hata kuzaliwa na sasa nimfiche nini .. Mungu awabariki nyote Kwa kazi nzuri ya kuhubiri neno la Mungu 🙏🙏🙌

Awey
Awey
1 year ago

Aminaa aminaa ah nikweli kabisa ndugu Bwana Yesu akubariki sanaa