TAFUTA KWA BIDII KUWA MTAKATIFU.

TAFUTA KWA BIDII KUWA MTAKATIFU.

Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tujifunze biblia, Neno la Mungu wetu.

Neno la Mungu linasema…

Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”

Andiko hilo ni muunganiko wa maneno mawili, Neno la kwanza ni “TUTAFUTE KWA BIDII KUWA NA AMANI NA WATU WOTE”, na neno la pili, ni “TUTAFUTE KWA BIDII KUWA WATAKATIFU”.

Ni sawa na mtu aseme “katafute shati na kiatu chumbani”…tukiichambua sentensi hiyo tunapata maneno mawili, 1) Tukatafute shati na pia 2) Tukatafute kiatu.

Vivyo hivyo hapo biblia iliposema “Tutafute kwa bidii kuwa na amani na watu wote” na “huo utakatifu”..imemaanisha “tutafute amani” na pia “tuutafute kwa bidii utakatifu”.

Ikimaanisha kuwa utakatifu, ni wa kutafutwa, Tena kwa bidii sanaa!!..

Na ni kwanini tumeambiwa tuutafute kwa bidii???…Ni kwasababu hapana mtu atakayemwona Mungu asipokuwa nao.

Unaweza usiwe na Imani kama ile ya Eliya lakini bado ukamwona Mungu, unaweza usiwe mhubiri wa madhabahu  lakini bado ukamwona Mungu.(Kwa kumtumikia Mungu kwa njia nyingine).

Lakini ukikosekana utakatifu, kumwona Mungu haiwezekani.

Na utakatifu maana yake ni kukaa mbali na kila aina ya dhambi.

Mtume Paulo kwa ufunuo wa Roho alizidi kilisisitiza hilo katika kitabu cha Wagalatia 5:19-20.

Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,

20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,

21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, KATIKA HAYO NAWAAMBIA MAPEMA, KAMA NILIVYOKWISHA KUWAAMBIA, YA KWAMBA WATU WATENDAO MAMBO YA JINSI HIYO HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU”.

Hapa mwisho anamalizia kwa kusema “watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”. Hii inaogopesha sana..

Sasa Utakatifu, tunautafutaje?..

  1. KWA KUZISHINDA TAMAA ZETU.

Dhambi yoyote kabla haijaleta madhara huwa inaanza kama mbegu ndogo..biblia inasema chanzo cha dhambi ni tamaa.

Yakobo 1:14 “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.

15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti”.

Unapokuwa na uwezo wa kuzitawala tamaa zako, basi dhambi kwako itakuwa mbali, na hivyo siku zote utajiweka katika hali ya utakatifu..lakini kila kitu kinachokuja mbele yako wewe unakitamani, kila mtindo wa uvaaji, ulaji au mtindo wa kimaisha unaokuja mbele zako unautamani, basi fahamu kuwa upo hatarini kuupoteza ukamilifu wako.

2. KWA KUKAA MBALI NA VICHOCHEO VYOTE VYA DHAMBI.

Dhambi inayo vichocheo, kama vile hasira ilivyo na vichocheo, kwa mfano vichocheo vya dhambi ya uasherati ni utazamaji wa pornography, mazungumzo mabaya na ya mizaha, makundi mabaya ya watu, uvaaji mbaya, filamu za kidunia ambazo asilimia kubwa maudhui zake ni kuchochea tamaa ya zinaa, vile vile magroup na kurasa mbalimbali katika mitandao ya kijamii kama vile facebook, whatsapp, instagram na mengineyo.

Mtu anayekesha muda wote kwenye facebook au kwenye mitandao mingine ya kijamii, mtu huyo kamwe asitegemee atakuwa salama..

Biblia inasema “Tutafute kwa bidii!!”…Sio kwa ulegevu..Maana yake “ukamilifu” hatuwezi kuupata tukiwa walegevu.

3. KWA KUOMBA NA KUJIFUNZA NENO.

Tunapokuwa waombaji, katika ulimwengu wa roho shetani na mapepo yake yananakaa mbali nasi..Hivyo na viwango vyetu vya utakatifu vinapanda..Vile vile tunapokuwa watu wa kujifunza Neno la Mungu, tunakuwa tunatakasika kwasababu Neno la Mungu lina maonyo ndani yake, na linatufunza na kutukumbusha kudumu katika Imani na utakatifu. Dalili ya kwanza ya mtu anayerudi nyuma kiimani, ni kupungukiwa na nguvu ya kujifunza Neno. Hivyo ili na sisi viwango vyetu vya utakatifu vipande hatuna budi tuwe wasomaji wa Neno la Mungu (yaani biblia) .

Bwana atusaidie, tuupate utakatifu!

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

TAFUTA MSAMAHA HALISI, NA SI MSAMAHA TU!

UTAKASO NI SEHEMU YA MAISHA YA MKRISTO YA KILA SIKU.

MAPENZI YA MUNGU NI YAPI?

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

Kwanini Eliya alijulikana kama “Eliya Mtishbi”?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments