Jina la Bwana na Mwokozi wetu, Yesu Kristo libarikiwe.. Karibu katika kujifunza Neno la Mungu wetu, ambalo ni Taa iongozayo miguu yetu na Mwanga wa Njia yetu. (Zab. 119:105).
Kuna tofauti ya kusamehewa makosa, na kuondolewa Dhambi.. Watu wengi sana wanasamehewa makosa yao na Mungu..lakini bado wanakuwa hawajaondolewa dhambi, Kusamehewa ni kitu kingine na kuondolewa ni kitu kingine..
Mtu wa kidunia, ambaye hata hamwamini Kristo anaweza kufanya kosa fulani, labda la kuiba na akastahili kufungwa, mtu huyo anaweza kumlilia Mungu, na Mungu akamsamehe kosa hilo na kumwepushia mbali adhabu ya kufungwa, lakini hiyo haimaanishi kuwa ndio kashapata ondoleo la dhambi zake zote.
Utakumbuka wale watu waliomsulubisha Bwana msalabani.. Bwana Yesu aliwaombea Msamaha.. Lakini kwa kuowaombea kule msamaha, haikumaanisha kuwa tayari wameshaokoka na kwamba wakifa wanaenda mbinguni. La! bado walikuwa wana dhambi, ya asili, ambayo hiyo haiondoki kwa kuombewa au kutamkiwa bali kwa mtu mwenyewe kuamua kuchukua hatua ya kufanya maamuzi..
Ingekuwa inaondoka kwa kutamkiwa tu, basi kazi ya wokovu ingekuwa ni rahisi sana, BWANA YESU Asingetuambia tujikane nafsi, asingetuambia tukabatizwe, ANGETUTAMKIA TU DUNIA NZIMA KUWA, TUMESAMEHEWA DHAMBI, na sisi tungekuwa tumestarehe.
Lakini haikuwa hivyo, bali kulikuwa na kanuni maalumu, Na kanuni hiyo ndio ile tunayoisoma katika.. Matendo 2:38, ya KUTUBU NA KUBATIZWA!.
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.
Kwahiyo wale Makuhani, na Maaskari waliomsulubisha Bwana hawakupata Ondoleo la Dhambi, kwasababu formula la kupata ondoleo la dhambi, ili kupata uzima wa milele, na kuokoka na ghadhabu ya Mungu ya ziwa la Moto, ndio hiyo ya kutubu na kubatizwa.
Wao walichokipata ni msamaha tu, wa lile tendo walilolifanya la kumsulubisha Bwana, lakini kama kulikuwa na uzinzi walioufanya juzi, au uuaji walioufanya wiki iliyopita, au wizi walioufanya mwaka uliopita, ambao hawakuutubia, bado walikuwa na hatia ya dhambi hizo, Hivyo walisamehewa kosa hilo moja tu, la kumsulubisha Bwana aliyekuwa mwenye haki, lakini makosa mengine yalibaki pale pale.
Maana yake ni kwamba, kama Bwana Mungu alikuwa amepanga kuwaadhibu kwa kosa hilo la kumsulubisha Bwana Yesu, basi alighairi kwa kuwa waliombewa msamaha. Lakini Msamaha huo walioupata sio Ule wa kuepukana na ziwa la Moto, au wa kuwapatia uzima wa Milele..bali wal lile kosa tu!
Msamaha uletao uzima wa milele, na utuepushao na ziwa la Moto, ni ule tuupatao kwa sisi wenyewe kuamua kutubu dhambi zetu zote kwa kumaanisha kuziacha, na kubatizwa katika ubatizo sahihi, kama ishara ya kufa na kufufuka na Kristo katika upya wa roho, na kupokea Roho Mtakatifu. (Msamaha huu ndio utuleteao uzima wa Milele, na ndio wa muhimu).
Je na wewe umepokea msamaha upi?..Umepata msamaha tu!, au Msamaha kamili..
Inawezekana kila siku unaamka asubuhi na kuomba toba!, ni kweli Bwana ni Mwingi wa Rehema atakusamehe, lakini kama USIPOPATA MSAMAHA KAMILI WA ONDOLEO LA DHAMBI ambao huo unakuja kwa wewe kuamua kutubu, kwa kumaanisha kuacha Dhambi zako zote.
Kama bado hujapata Msamaha kamili, basi utafute leo kwa bidii.
Maran atha!
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Bwana aliposema “sikuja kutangua torati bali kuitimiliza” alikuwa anamaanisha nini?
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.
About the author