Kuota unasubiriwa mahali fulani uhutubie, halafu unachelewa.

Kuota unasubiriwa mahali fulani uhutubie, halafu unachelewa.

SWALI: Kuota nasubiriwa mahali Fulani, nihutubie halafu mimi nachelewa, au natingwa na mambo mengine ina maana gani?


JIBU: Ndoto ya namna hii, mara nyingi huwa inaotwa na makundi ya watu ambao wanawajibika katika kuwahudumia wengine, aidha ni viongozi, au wahubiri.

Na huwa zinakuja katika sura tofauti tofauti, wengine wanaota wanasubiriwa kwenye mikutano wahutubie, lakini wanajikuta, wakicheleweshwa na mambo madogo madogo, pengine foleni, au watu, au vishughuli visivyokuwa na msingi. Wengine wanaota wanapaswa wapande madhabahuni wawahubirie wengine, lakini mara wanajiona wapo uchi, wanatafuta suti zao wavae, hawazioni, muda unazidi kwenda, mpaka mwishoni watu wanaondoka, wote na yeye bado hajatokea madhabahuni. N.k.

Hivyo ukiota ndoto ya namna hii tafsiri yake ni kuwa, wewe kama kiongozi kiwango chako cha utayari katika  nafasi hiyo Mungu aliyokuweka bado kipo chini. Na ndio maana unashindwa kufika pale, yapo mambo ambayo yanatia vikwazo kwako. Bwana anasema..

2Timotheo 4:2  “lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho”

Hivyo unachopaswa kufanya ni kuondoa visababu, au hivyo vizuizi vidogo vidogo, mbele yako, ambavyo pengine vinakusababishia uone huo sio wakati ufaao, kwa kumtumikia Mungu, kisha kuwa tayari, kusimama na Bwana kwa ukamilifu wote, kama askari ambaye amevitwa utayari miguuni kwa ajili ya  vita.

Waefeso 6:13  “Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.

14  Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,

15  na kufungiwa miguu UTAYARI tupatao kwa Injili ya amani”

Kwa kuzingatia hayo, utakuwa umelitatua hilo tatizo, katika wito wako.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Kuota unapigana na mtu.

KUOTA UPO KANISANI.

KUOTA UNALIA/UKIOTA UNALIA KWA UCHUNGU.

KUOTA UMECHOMWA KISU/KUOTA UMEPIGWA RISASI.

MTAWATUPIA MBWA NYAMA HIYO.

NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.

Kama Malkia Esta alijipamba je! Kuna ubaya gani wanawake wa wakikristo wa leo kujipamba?.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Christina Gervas
Christina Gervas
1 month ago

Ubarikiwe mtumishi leo nimesoma maana ya ndoto ya kuchelewa nmepata uelewa wa nini kinaendelea kwenye maisha yangu! Ee Mungu nisaidie niweze kuvuka vikwazo vinavyofanya nisifike sehemu unayotaka nifike kwa wakati. Amen!

Emmanuel Kitengule
Emmanuel Kitengule
1 year ago

Bwana akubariki sana mwalimu kwa mafafanuzi mazuri kabisa.