KUOTA UNALIA/UKIOTA UNALIA KWA UCHUNGU.

KUOTA UNALIA/UKIOTA UNALIA KWA UCHUNGU.

Kuota unalia kwa uchungu/Ukiota unalia maana yake ni nini kibiblia?.


Zipo ndoto zenye maana, na pia zipo ndoto zisizo na maana yoyote katika maisha ya mtu, hizi za pili ni ndoto ambazo zinatengenezwa na ubongo wako tu wenyewe, kwa kuchukua matukio ambayo aidha ulishawahi kuyafanya au kuyapitia huko nyuma, au mazingira unayoishi sasa, au mambo unayoyafanya mara kwa mara.

Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi…;”

Kwamfano kama wiki iliyopitia ulikuwa unahudhuria sana kwenye sherehe, tarajia moja ya ndoto unazoziota kila siku kuwa za namna hiyo.. Vivyo hivyo na ndoto hii ya kuota unalia/ukiota unalia kwa uchungu, inaweza kuja kutokana na mazingira yako ya nyuma, Wengine walifiwa na jamaa zao wa karibu kipindi sio kirefu, wengine walikuwa misibani.n.k..Hivyo ubongo unachukua matukio hayo na kuyarudia rudia kwenye ndoto zetu za kila siku.


Lakini pia ndoto ya namna hii inaweza  kuja kwa namna ya kitofauti sana, pengine hujafiwa siku za hivi karibu, au hujapitia matatizo yoyote mazito ya kukufanya uwe katika huzuni kubwa..Lakini unashangaa usiku umeota unalia kwa uchungu mwingi, bila kujua sababu ya kulia kwako ni nini. Unalia tu, unalia tu,

Ukiona hivyo basi lipo jambo unapaswa ulijue rohoni..

Ndugu unayesoma ujumbe huu, fahamu kuwa hizi ni siku za mwisho, na Yesu anakaribia kuja kulinyakua kanisa lake. Mwisho wa dunia upo karibu sana.

Kuota unalia kwa uchungu, Ni Mungu anakuonyesha kuwa jinsi hali itakavyokuja kuwa huko mbeleni ikiwa utaachwa katika unyakuo, na watu wote watakavyokuwa..Haijalishi wewe ni muislamu, ujumbe huu unakuhusu pia wewe, kiama kipo karibu, watu wataomboleza, kwa kilio na uchungu usioeleza,  kwa hayo mambo ya kutisha ambayo Mungu atayaleta katika hii dunia,

Biblia inasema hivi;

Sefania 1:14 “Hiyo siku ya Bwana iliyo kuu i karibu; I karibu, nayo inafanya haraka sana; Naam, sauti ya siku ya Bwana; SHUJAA HULIA KWA UCHUNGU MWINGI HUKO!

15 Siku ile ni siku ya ghadhabu, Siku ya fadhaa na dhiki, Siku ya uharibifu na ukiwa, Siku ya giza na utusitusi, Siku ya mawingu na giza kuu,

16 Siku ya tarumbeta na ya kamsa, Juu ya miji yenye maboma, Juu ya buruji zilizo ndefu sana.

17 Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda Bwana dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi.

18 Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya Bwana; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha”.

Unaona, hali itakavyokuwa kwa watu hata wale wanaojiona mashujaa leo, watalia kwa uchungu mwingi..

Isaya 33:7 “ANGALIA, MASHUJAA WAO WANALIA NJE, WAJUMBE WA AMANI WANALIA KWA UCHUNGU.

8 Njia kuu zimeachwa, msafiri amekoma; ameyavunja maagano, ameidharau miji, hamjali mtu.

9 Nchi inaomboleza, na kulegea; Lebanoni imetahayarika na kunyauka; Sharoni imekuwa kama jangwa; Bashani na Karmeli zimepukutika majani”.

Ni mambo ya kutisha sana, ikiwa leo Yesu amerudi, na umeachwa, kitakachokuwa kinaendelea kwako, ni zaidi ya ulichokiona katika ndoto..

Yeremia 4:8 “Kwa sababu hiyo jifungeni nguo za magunia; ombolezeni na kulia kwa uchungu; kwa maana hasira kali ya Bwana haikugeuka na kutuacha.

9 Na katika siku hiyo itakuwa, asema Bwana, moyo wa mfalme utapotea, na moyo wa wakuu wake; na makuhani watastaajabu, na manabii watashangaa”.

Mathayo 13:41 “Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi,

42 na kuwatupa katika tanuru ya moto, NDIKO KUTAKUWAKO KILIO NA KUSAGA MENO”.

Yapo maandiko mengi yanayoelezea maombolezo yatakayokuwa yanaendelea katika kipindi hicho lakini hatuwezi kuiorodhesha yote hapa, Kama utapenda kufahamu kwa marefu juu ya siku hiyo ya mwisho itakavyokuwa basi fungua hapa usome.>>> MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

Hivyo Kama wewe hujaokoka, na unajijua kabisa unaishi katika maisha ya dhambi, basi ni vema ukamgeukia Kristo leo, ayaokoe maisha yako, Kukutana na ujumbe huu sio bure, Umeoteshwa ndoto hiyo ni kwasababu Mungu ana mpango na wewe. Hivyo usifanye moyo wako mgumu, mkabidhi Yesu maisha yako leo aanze kutembea na wewe na hakika utamwona kwa namna ambayo hukuwahi kumtazamia, na atahakikisha kuwa mabaya hayo yote hayatakukuta ikiwa atarudi leo..

Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki sana.

Pia angalia vichwa vya masomo mengine chini, fungua upitie naamini vitakutoa sehemu moja kiroho hadi nyingine.

 Ikiwa utapenda kupata mafundisho ya Neno la Mungu ya kila siku kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwa namna hii: +255 789001312

Au jiunge kwa kubofya hapa chini;

Group la whatsapp  Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

 

Mada Nyinginezo:

NA YEYE ALIYEKETI JUU YA WINGU AKAUTUPA MUNDU WAKE JUU YA NCHI, NCHI IKAVUNWA.

SIKU ILE NA SAA ILE.

MAONO YA NABII AMOSI.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

FAHAMU MAJIRA ULIYOPO NA NINI UNAPASWA UWE NACHO.

NA NENO LA BWANA LILIKUWA ADIMU SIKU ZILE.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
JUMA YASIN
JUMA YASIN
2 years ago

SAWA