Yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.

Yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.

SWALI: Nini maana ya huu mstari? Hapo anaposema yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.

Mhubiri 10:8

[8]Mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani yake;  Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.


JIBU: Mistari hiyo inawazumgumzia watu ambao wanasababisha matatizo kwa wenzao. Au watu wanaowakosesha wengine waliokuwa tayari katika njia sahihi.

Na ndio maana hapo anaanza kwa kusema mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani yake..Akiwa na maana kuwa dhara lile unalolipanga kwa mwingine limpate ndilo hilo hilo litakupata wewe.

Mfano wa watu kama hawa katika biblia ni Hamani, ambaye alikua adui wa Mordekai na wayahudi wote, mpaka akafikia hatua ya kumtengenezea msalaba Mordekai, lakini kinyume chake msalaba ule ndio ukamtundika yeye mwenyewe.

Lakini kwenye hicho kipengele cha pili anasema Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.. Maana yake ni kuwa maboma sikuzote hujengwa kwa lengo la kudhibiti maadui, tukiachilia mbali wanadamu, lakini pia wanyama wakali kama fisi, mbweha na nyoka wasivamie mifugo.

Hivyo anaposema abomoaye boma..anamaanisha aondoaye ulinzi wa mwenzake ili maadui kama nyoka wapite, wawadhuru, kinyume chake atadhurika yeye.

Hii ikifunua nini? 

Wapo watu leo hii, wanaoondoa maboma ya watu wengine kwa hila zao. Na maboma yanayomaanishwa hapo si mengine zaidi ya YESU KRISTO. Yeye ndio boma letu, Biblia inasema hivyo..

Zaburi 18:2

[2]BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu,  Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia,  Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.

Hivyo watu watu wanawakosesha kwa kuwalaghai ili ibilisi awameze, wanawazuia wasimwabudu Mungu sawasawa na mapenzi yake, wanawazuia wasimwombe Mungu wao, ili wapoe..lakini kinyume chake wao ndio watamezwa. Na Bwana atawaponya watu wake.

Mfano wa watu kama hawa,ni  wale maliwali wa Umedi waliompangia visa Danieli, ili asimwombe Mungu wake, kutwa mara tatu. Wakidhani kuwa ndio atapotelea mbali kwenye tundu la simba. Lakini kinyume chake wao ndio walimezwa na ibilisi.

Hivyo kamwe usijaribu kumkosesha mtu wa Mungu, wala usijaribu kumwondolea boma lake (Yesu Kristo), ukadhani ndio tayari atarudi nyuma. Wewe ndio utarudishwa nyuma na shetani.

Tusiwe watu wa kusababisha mabaya/madhara kwa wengine. Ndio kiini cha mistari hiyo.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

UBATILI.

Wale Nyoka wa Moto jangwani, walikuwa ni wa namna gani?

JIHADHARI NA UONGO WA SHETANI UNAOKARIBIANA NA UKWELI.

NJIA YA KUPATA WOKOVU.

Biblia ina maana gani inaposema akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko?

Mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments