KUOTA UMECHOMWA KISU/KUOTA UMEPIGWA RISASI.

KUOTA UMECHOMWA KISU/KUOTA UMEPIGWA RISASI.

Kuota umechomwa kisu au Kuota umepigwa risasi kuna maanisha nini?


Awali, ni vyema kujua kuwa si kila ndoto aotayo mtu, ina maana katika maisha yake, Hilo ni vizuri ukalifahamu, Ndoto nyingi tunazoziota kila siku zinatokana na shughuli zetu za kila siku (Mhubiri 5:3), au mazingira yanayotuzunguka, au mambo ambayo tunayawaza mara kwa mara, au  tulishawahi kuyaona, au kuyapitia sehemu Fulani katika maisha yetu (Isaya 29:8)..

Naweza kusema asilimia 90 ya ndoto tunazoziota kila siku zinaangukia katika kundi hili,.Hapo ndipo watu wengi wanaposhindwa kuelewa, wanataka kila ndoto wapate tafsiri ya rohoni, au maishani, hilo jambo halipo, utaishia kudanganywa, au kujidanganya mwenyewe, Kumbuka kinachoweza kueleza hatma ya maisha yetu kwa ufasaha wote, sio ndoto tunazoziota usingizini, bali Neno la Mungu tunaloliishi kila siku.

Mungu anaziita ndoto kama makapi ukifananisha na Neno lake(Yeremia 23:28-29). Akiwa na maana kuwa mtu Yule anayeishi kwa kulishika Neno lake, Ni bora kama ngano, kuliko yule anayetafuta maana za ndoto zilizofananishwa na makapi.

Ni mara chache, ndoto zinabeba ujumbe, ili kutambua ndoto yako inatoka kwa Mungu au kwa shetani, au kwako mwenyewe, basi fungua hapa usome kwanza>>> Nitajuaje kama ndoto ni ya Mungu au ya Shetani?

KUOTA UMECHOMWA KISU/KUOTA UMEPIGWA RISASI.

Hivyo ukiwa umeshasoma, na unao uhakika kabisa kuwa ndoto uliyoota, si ya kawaida, imekujia kwa uzito mwingine wa kitofauti, imekushtua sana, imeonekana kama ni jambo la halisi kabisa, basi upo ujumbe wa rohoni.

Sasa kwa namna ya kawaida, ukishaona mpaka mtu amefikia hatua ya kukuchoma kisu, au amekupiga risasi ni wazi kuwa kuna jambo ulilifanya, au unalifanya sasa hivi, ambalo  limemchukiza sana, kiasi cha kufikia  uamuzi wa kuona kufa kwako ni bora kuliko kuishi.

Vivyo hivyo katika ndoto ukiona umepigwa risasi, au umechomwa kisu, au upanga, au mkuki,au kitu chenye ncha kali, hiyo  ni ishara kuwa maishani mwako, lipo jambo ambalo unalifanya, halifurahiwi na wengine, aidha ni zuri au baya,

Katika biblia tunasoma habari ya mtu mmoja, aliyeitwa Egloni mfalme wa Boabu, huyu, aliwatumikisha Israeli kwa muda wa miaka 18, na hiyo yote ilikuwa ni kutokana na makosa yao wenyewe(Israeli)..Lakini walipomlilia Mungu, awaokoe kutoka katika utumwa na mateso ya mfalme huyu, Mungu akawasikia ndipo akawapelekea mwokozi aliyeitwa Elihu.

Huyu Elihu alijifanya kama mjumbe, aliyeituwa na Israeli, kumbe hila zake zilikuwa ni kwenda naye katika chumba cha siri, ili wakiwa wao wawili peke yao achomoe upanga wake na kumchoma tumboni, Tusome kidogo..

Waamuzi 3:20 “Basi Ehudi akamwendea; naye alikuwa anaketi peke yake katika chumba chake cha baridi. Ehudi akasema, Mimi nina ujumbe utokao kwa Mungu kwako wewe. Basi akainuka katika kiti chake.

21 Ehudi akaunyosha mkono wake wa kushoto, akaushika huo upanga kuutoa hapo katika paja lake la kuume, akamtia tumboni mwake;

22 hicho kipini nacho kikaingia ndani pamoja na huo upanga wenyewe; nayo mafuta yakashikamana tena juu ya upanga, kwani hakuutoa tena upanga tumboni; nao ukatokea kwa nyuma.

23 Ndipo Ehudi akatoka nje barazani, akamfungia milango ya hicho chumba na kuifunga kwa ufunguo.

24 Basi alipokuwa amekwisha toka nje, hao watumishi wake wakaenda; wakaona, na tazama, hiyo milango ya chumba ilikuwa imefungwa kwa ufunguo; nao wakasema, Hapana budi amejifunika miguu yake ndani ya chumba cha baridi.

25 Wakangoja hata wakatahayari; na tazama, hakuifungua milango ya chumba; basi wakatwaa ufunguo, na kuifungua; na tazama, bwana wao alikuwa ameanguka nchi, naye amekufa”.

Umeona? Sasa huyu Elgoni alichomwa kutokana na makosa yake, lakini, pia wapo wengine waliochomwa kutokana na haki zao, mfano mmojawapo ni Bwana wetu YESU KRISTO..Yeye alichomwa mkuki pale msalabani, sio kwasababu alikuwa mwovu hapana.

Hivyo na wewe jiangalie ni wapi katika maisha yako, pana vita kwa wengine, wewe umesimama, Ikiwa upo ndani ya Kristo basi, ujue maadui wa imani wapo, lakini huna haja ya kuogopa, Kwasababu Mungu atakupigania, kikubwa unachopaswa ufanye ni kuzidi kuwa mwombaji.

Lakini kama upo nje ya Kristo, ukweli ni kwamba, licha tu kuzungukwa na hatari za maadui, lakini, maisha yako ya rohoni yapo hatarini.. Mungu anaweza kweli kukuepusha na hatari za mwilini, lakini zile za rohoni za ibilisi hawezi kukuzuia kutokana na kwamba wewe ni milki ya ibilisi.

Jiulize ukifa leo ghafla katika dhambi utakuwa mgeni wa namna huko uendako?

Hivyo ndugu ikiwa unahitaji kumpa leo YESU maisha yako..Basi uamuzi huo utakuwa ni busara sana kwako, Kama upo tayari kufanya hivyo, moja kwa moja fungua hapa, kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba.>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Na hayo mengine yaliyosalia Mungu atakujalia rehema zake.

Bwana akubariki.

Kwa mafundisho zaidi ya Neno la Mungu.

Whatsapp: +255 789001312

Group la whatsapp 

  Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

 

Mada Nyinginezo:

Kuota unafanya Mtihani.

KWANINI TUNAPASWA TUJIZUIE?

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

MWAKA WA BWANA ULIOKUBALIWA.

HUYU MELKIZEDEKI NI NANI?

NILIMWONA SHETANI, AKIANGUKA KUTOKA MBINGUNI.

ZIFAHAMU HUDUMA KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments