MAPENZI YA MUNGU NI YAPI?

MAPENZI YA MUNGU NI YAPI?

Bwana Yesu alisema maneno haya katika Mathayo 7:21-23.

Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; BALI NI YEYE AFANYAYE MAPENZI YA BABA YANGU ALIYE MBINGUNI”

22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.

Sasa unaweza kujiuliza hayo “Mapenzi ya Mungu ndio yapi” Kwasababu hapo tunaona kumbe hata unaweza kutoa pepo lakini ukawa bado huyafanyi mapenzi ya Mungu…vile vile unaweza ukawa unatabiri na kutoa unabii na unabii huo ukatimia lakini, bado ukawa mbali na mapenzi ya Mungu.

Sasa Mapenzi ya Mungu ni yapi?..ambayo tukiyafanya hayo hata kama tutakuwa hatutoi pepo wala kutoa unabii wala kutabiri bado tuta urithi ufalme wa mbunguni?.

Tusome,

1 Wathesalonike 4:2 “Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu.

3 Maana HAYA NDIYO MAPENZI YA MUNGU, KUTAKASWA KWENU MWEPUKANE NA UASHERATI;

4 KILA MMOJA WENU AJUE KUUWEZA MWILI WAKE KATIKA UTAKATIFU NA HESHIMA;

5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu”.

Umeyaona Mapenzi ya Mungu?
Kumbe Mapenzi ya Mungu si miujiza wala upako, bali UTAKATIFU..

Kumbe hata tukiwa na Imani kubwa ya kuweza kugeuza maji kuwa asali bado upo uwezekano mkubwa wa kupotea katika ziwa la moto, kama HATUNA UTAKATIFU.

Hii ni tahadhari kubwa sana kwetu..Lakini biblia inazidi kulithibitisha hilo kwetu katika..

Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, NA HUO UTAKATIFU, AMBAO HAPANA MTU ATAKAYEMWONA MUNGU ASIPOKUWA NAO” .

Ndugu yale maono unayoyaona katika ndoto, ni kweli ni ya kiMungu lakini hayo sio tiketi ya kukufikisha mbinguni, tiketi ya kukufikisha mbinguni ni utakatifu wa mwili na roho.

Ile imani iliyo nayo kiasi kwamba chochote utakachokisema kwa jina la Bwana kinatokea, sio tiketi ya kufika mbinguni kama hutaacha uasherati wako, au ulevi wako, au wizi wako au utukanaji wako.

Ile ahadi Mungu aliyokuonyesha kwa njia ya unabii au ndoto, sio tiketi ya wewe kuurithi uzima wa milele, kama hutadumu katika kuyafanya mapenzi ya Mungu (Yaani Utakatifu).

Uuimbaji unaoimba, unabii unaoutoa, lugha unazonena hazitakufikisha popote kama hutaamua kujitakasa kwa kuacha kuvaa vimini, kuacha kuvaa suruali (kama ni mwanamke), kuacha kujipaka uso rangi, kuacha kuvaa kope na kucha za bandia, kama hutaacha kuvaa hereni, wigi na kupaka lipstiki na kunyoa kiulimwengu..

Utauliza inamaana wanawake kuvaa suruali  na vimini sio mapenzi ya Mungu?..Jibu ni NDIO!. Rejea vizuri hiyo mistari…

“KILA MMOJA WENU AJUE KUUWEZA MWILI WAKE KATIKA UTAKATIFU NA HESHIMA”.

Sasa jiulize vimini ni nguo za heshima?, Suruali ni nguo za heshima?..Je unaweza kwenda kumtambulisha mchumba wako kwa wazazi wako akiwa amevaa Suruali?? Au vimini??..Kama huwezi basi jua hayo sio mavazi ya heshima na hayafai..na mapenzi ya Mungu ni “kila mtu kuuweza mwili wake kwa utakatifu na Heshima

Kama hutaacha hayo yote, na umesikia kama hivi, basi siku ile utatimiza huu unabii unaosema.. “wengi watasema siku ile wakisema, hatukufanya hichi au kile” na Bwana atawakataa dhahiri.

Mimi na wewe na ndugu zetu tusiwe watu hao watakaotimiza huo unabii.

Bali tujiepushe na dhambi na kujitakasa, ndivyo tutakavyofanya mapenzi ya Mungu.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

Je suruali ni vazi la kiume tu?

KUJIPAMBA NI DHAMBI?

Kama Malkia Esta alijipamba je! Kuna ubaya gani wanawake wa wakikristo wa leo kujipamba?.

KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)

Watu wenye ulemavu wa akili, wataenda mbinguni?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
2 years ago

Amina

Costantine Lucas
Costantine Lucas
2 years ago

Moja ya mapenzi ya Mungu ni kuishi Kwa kufuata amri zake zote bila ubaguzi

Lucas mhula
Lucas mhula
2 years ago

Amina Sana hilo somo zuri mmno naomba Kama kungekuwa Kuna sehemu ya kushare ingekuwa vizuri sana, nitalikuta facebook?