Watu wenye ulemavu wa akili, wataenda mbinguni?

Watu wenye ulemavu wa akili, wataenda mbinguni?

Jibu: Hapana!, watu wenye ulemavu wa akili kikweli kweli, Bwana akirudi hawataenda!, watabaki kukumbana na ghadhabu ya Mungu.!.

LAKINI SISI TUNAVYOMTAFSIRI MTU MWENYE ULEMAVU WA AKILI, NI TOFAUTI NA MUNGU ANAVYOMTAFSIRI.

Sisi tunamtafsiri mtu mwenye ulemavu wa akili ni yule tunayemwona haeleweki anapozungumza, anatokwa na mate mdomoni, na hawezi kujimudu mwenyewe!..na mtu aliye na akili timamu ni yule, tunayemwona anaoga vizuri na kuwa nadhifu na mwenye utashi wa kidunia! Anayekubalika kila mahali.. lakini kwa Mungu sivyo.

1Wakorintho 3:18 “Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima.

19 MAANA HEKIMA YA DUNIA HII NI UPUZI MBELE ZA MUNGU. KWA MAANA IMEANDIKWA, YEYE NDIYE AWANASAYE WENYE HEKIMA KATIKA HILA YAO”.

Sasa mtu mwenye MATATIZO YA AKILI, kibiblia ni yupi?

Tusome, mistari ifuatayo ili tuweze kujua “Mlemavu wa akili ni yupi mbele za Mungu”.

 1. MTU MZINIFU.

Mithali 6:32 “Mtu aziniye na mwanamke HANA AKILI KABISA; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake”.

Wakati unaona mtu anayedondosha mate, kama hana akili, kumbe Mungu anakuona wewe unayezini kuwa HUNA AKILI KABISA!.. Tena hasemi “huna akili” tu!..bali anamalizia na neno “kabisa”. Kwahiyo kumbe mtu anayezini ni Tahira!, mbele za Mungu… ni heri uwe unashindwa kuyamudu mate yako kuliko kuwa mzinifu.

 2. MTU ANAYEDHARAU WENGINE.

Mithali 11:12 “ASIYE NA AKILI HUMDHARAU MWENZIWE; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza”.

Kama unamdharau huyo  unayemwona hawezi kuongea kama wewe, au hawezi kupambanua kama wewe, au hana heshima kama yako, au uwezo kama wako.. basi tambua kuwa mbele za MUNGU, Wewe ndio HUNA AKILI (Una matatizo ya akili) kuliko huyo unayemdharau.

1Wakorintho 3:18 “Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima.”

 3. MTU ANAYEWAONEA WENGINE!

Mithali 28:16 “Mkuu ALIYEPUNGUKIWA NA AKILI HUWAONEA WATU SANA; Bali achukiaye kutamani ataongeza siku”

Ikiwa una cheo Fulani, au wewe ni mkubwa kicheo au kiumri, katikati ya watu, na hutendi haki bali unawaonea wengine, basi fahamu kuwa mbele za Mungu, unayo matatizo ya akili, haijalishi dunia nzima inakuona una akili, mbele za Mungu unao ulemavu wa akili.

Kwaufupi kuishi Maisha ya dhambi na ya kutomtafuta Mungu, na huku unajua kabisa kuwa unapaswa umtafute Mungu, HUKO NI KUKOSA AKILI.

Zaburi 14:2 “Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu”.

Kwahiyo, kwa hitimisho ni kwamba “wale tunaowaona sisi ni walemavu wa akili, waliopo mahospitalini”..Mungu hawaoni hivyo!.. Na Bwana anateta nao!, kwa namna yao, na watahukumiwa kwa namna yao!..Wewe huwezi kuongea nao, lakini Bwana anaweza kuongea nao, kwasababu yeye ndio aliyewaumba…

Wewe huwezi kuwaelewa lakini Bwana anawaelewa, kwasababu ni yeye ndiye kawaumba..hawezi kukiumba kitu ambacho kitamshinda yeye kukielewa.

Wewe huwezi kuona kama wanamwabudu Mungu, au wanamtukuza Mungu, au wana dhambi lakini Mungu ndiye anayewajua mienendo yao…

Hivyo kwasababu Bwana ndiye anayewajua na ndiye atakayewahukumu, wapo watakaoingia mbinguni, na wapo ambao hawataingia.. (Wanadamu wote siku za mwisho watasimama mbele ya kiti cha hukumu).

Lakini sisi tunaojiona tuna akili timamu, huku tunazini, au tunafanya dhambi, huku tunatembea nusu-tupu barabarani, huku tunapaka rangi nyuso zetu, huku tunajichora Ngozi zetu, huku tunaabudu sanamu!..tujue mbele zake Mungu ni “walemavu wa akili” , haijalishi dunia nzima itatuthaminisha kiasi gani, basi mbele zake ni “walemavu wa akili”. Hivyo ili tuwe na akili hatuna budi kumtafuta Mungu, kwa kumwamini Bwana Yesu na kuyashika maneno yake.

Mathayo 7:24 “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;

25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba”.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Nini maana ya “Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia?

CHAPA YA MNYAMA

Wibari ni nani?(Mithali 30:26)

INJILI YA MANENO LAINI ITAKUGHARIMU.

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Awey
Awey
1 year ago

Hii nikweli tupu

Brian Masiga
Brian Masiga
2 years ago

Ntaka kua mnjili

Cathy
Cathy
2 years ago

Wow!
Somo zuri sana. Ama kweli Mungu hufanya vitu tofauti kabisa na akili za ki-binadamu. Mawazo yake ni makuu sana na akili zake hazichunguziki. Nashukuru kujua jinsi gani biblia inatafsiri mtu asiye na akili.
Asante sana mwandishi.
Mungu awabariki Wingu la Mashahidi.
Amen.