JE MGOGORO WA URUSI NA UKRAINE,UMETABIRIWA KIBIBLIA?

JE MGOGORO WA URUSI NA UKRAINE,UMETABIRIWA KIBIBLIA?

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia.

Leo tutajifunza juu ya mgogoro wa Urusi na Ukraine, Je Mgogoro huu umetabiriwa katika biblia?

Awali ya yote, kabla hatujaendelea mbele, tusome kwanza mstari ufuatao..

Mathayo 24:6 “NANYI MTASIKIA HABARI ZA VITA NA MATETESI YA VITA; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado.

7 Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali.

8 Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu”.

Hapo anasema, kutatokea na tetesi za vita lakini “ule mwisho bado”.

 Kwahiyo “Tetesi hizi za vita”…ndio Mwanzo wa Utungu tu!..(Maana yake ndio tumeukaribia ule mwisho)..Lakini mwisho wenyewe bado haujafika..(Unyakuo bado haujapita, lakini ndio upo karibuni kutokea).

Sasa tukirudi kwenye swali, je Mgogoro wa Urusi na Ukraine, ni wapi umetabiriwa katika biblia?

Mgogoro wa Urusi na Ukraine, haujatabiriwa popote katika biblia, kama vile vita vya Maji-Maji na Mau-Mau, jinsi ambavyo havikutabiriwa katika biblia, ndivyo hivyo hivyo Urusi na Ukraine, biblia isingeweza kuandika kila kitu!.

Lakini mgogoro huu, UNAFUNGUA NJIA kwaajili ya vita kuu iliyo karibuni kutokea kipindi si kirefu kati ya URUSI na TAIFA LA ISRAELI.. Vita kati ya Urusi na Israeli ndiyo iliyotabiriwa katika biblia (Ambayo vita hiyo tunaisoma katika kitabu cha Ezekieli 38 na 39).

Vita hii ipo karibu sana kupiganwa.. Ambapo Taifa la Urusi, (Gogu na Magogu) Kwa kiburi chake litaingia katika mgogoro na Taifa la Israeli, na mataifa ya kiarabu, yaliyo na uadui na Taifa la Israeli yataungana na Urusi kupanga kuiondoa katika ramani ya dunia.. Lakini siku hiyo maandiko yanasema..Mungu atatokea na kuwapigania Israeli, kama alivyowapigania zamani..

Mataifa yanayotajwa kushirikiana na Urusi katika vita hiyo ni Irani, Libya, Uturuki, Palestina, Jordani na mataifa ya kando kando ya Israeli. Biblia haijatoa sababu ya Urusi kutaka kuivamia Israeli ni ipi, lakini litazuka jambo tu ambalo litayapeleka mataifa hayo mawili katika vita hivyo.

Na lengo la Mungu kuruhusu vita hivyo ni kulifuta Taifa la Urusi, lililonyanyuka moyo wake, hali kadhalika kuyaondoa baadhi ya Mataifa ya kiarabu yanayoiilaani Israeli. Na Ijapokuwa Urusi ni Taifa kubwa, na lenye nguvu kiuchumi na kijeshi, lakini siku hiyo Bwana ataligeuza kuwa vumbi, kutakuwa hakuna tena Taifa la Urusi duniani!.

Ezekieli 38:14 “Basi, mwanadamu, tabiri, umwambie Gogu, Bwana MUNGU asema hivi; Katika siku ile watu wangu, Israeli, watakapokaa salama, hutapata habari?

15 NAWE UTAKUJA KUTOKA MAHALI PAKO, KUTOKA PANDE ZA MWISHO ZA KASKAZINI, WEWE, NA WATU WA KABILA NYINGI PAMOJA NAWE, WOTE WAMEPANDA FARASI, KUSANYIKO KUBWA, NA JESHI KUU;

16 nawe utapanda juu uwajilie watu wangu, Israeli, kama wingu kuifunika nchi; itakuwa katika siku za mwisho, nitakuleta upigane na nchi yangu, ili mataifa wanijue, nitakapotakaswa kwako, Ewe Gogu, mbele ya macho yao.

17 Bwana MUNGU asema hivi; Je! Wewe ndiwe niliyemnena zamani za kale, kwa vinywa vya watumishi wangu, manabii wa Israeli, waliotabiri siku zile kwa muda wa miaka mingi, ya kwamba nitakuleta upigane nao?

18 ITAKUWA KATIKA SIKU HIYO, GOGU ATAKAPOKUJA KUPIGANA NA NCHI YA ISRAELI, ASEMA BWANA MUNGU, GHADHABU YANGU ITAPANDA KATIKA MIANZI YA PUA YANGU.

19 Kwa maana katika wivu wangu, na katika moto wa ghadhabu yangu, nimenena, Hakika katika siku ile kutakuwako tetemeko kubwa katika nchi ya Israeli;

20 hata samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama wa kondeni, na vitu vyote vitambaavyo juu ya nchi, na wanadamu wote walio juu ya uso wa nchi, watatetemeka mbele ya uso wangu; nayo milima itatupwa chini, na magenge yataanguka, na kila ukuta utaanguka chini.

21 Nami nitaita upanga, uje juu yake katika milima yangu yote, asema Bwana MUNGU; nao upanga wa kila mtu utakuwa juu ya ndugu yake.

22 Nami nitamhukumu kwa tauni, na kwa damu; nami nitanyesha mvua ifurikayo, na mvua ya mawe makubwa sana, na moto na kiberiti juu yake, na vikosi vyake, na watu wa kabila nyingi walio pamoja naye.

23 Nami nitajitukuza, na kujitakasa, na kujidhihirisha, mbele ya macho ya mataifa mengi; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana”.

Katika vita hiyo maandiko yanasema Mizoga ya watu watakaouawa, itakusanywa kwa kipindi cha miezi 7, (Mizoga itazagaa kila mahali). Warusi wengi watakufa ndani ya ardhi ya Israeli, na dunia nzima itamwogopa Mungu wa Israeli..

Ezekieli 39:11 “Tena, itakuwa katika siku hiyo, nitampa Gogu pa kuzikia katika Israeli, bonde la wapitao, upande wa mashariki wa bahari; nalo litawazuia wapitao; na huko watamzika Gogu na watu wake jamii yote; nao wataliita, Bonde la Hamon-Gogu.

12 NA KWA MUDA WA MIEZI SABA nyumba ya Israeli watakuwa wakiwazika, wapate kuisafisha nchi.

13 Naam, watu wote wa nchi hiyo watawazika; itakuwa ni sifa kwao katika siku ile nitakapotukuzwa, asema Bwana MUNGU.

14 Nao watawachagua watu wa kufanya kazi ya daima, watakaopita kati ya nchi, ili kuwazika waliosalia juu ya uso wa nchi, ili kuisafisha; miezi saba itakapokwisha kupita watatafuta.

15 Na hao wapitao kati ya nchi watatafuta; na mtu ye yote aonapo mfupa wa mtu, ndipo atakapoweka alama karibu nao, hata wazishi watakapouzika katika bonde la Hamon- Gogu.

16 Tena, Hamona litakuwa jina la mji. Hivyo ndivyo watakavyosafisha nchi”.

JE VITA HII YA URUSI NA UKRAINE NI NINI INAONGEZA KWA URUSI?

Vita hii, inaiongezea Urusi Ujasiri, na kuiaminisha kuwa inaweza kufanya jambo Fulani la kuisumbua dunia. Ujasiri huo unaongeza kiburi chake dhidi ya Mungu, na unaandaa mazingira ya kuishukia Israeli, kama vile Mfalme wa Ashuru, (Senakeribu) alivyojiongezea Ujasiri hata kupanga kuishukia Yuda, huku akimtukana Mungu wa Israeli..kwasababu tu aliyashinda mataifa mengine yote yaliyomzunguka, hivyo akalidharau Taifa dogo la Yuda, na hata kufikia hatua ya kumtukana Mungu wa Israeli

Lakini Mungu alikishusha kiburi chake kwa kuliangamiza jeshi lake lote pasipo kupigana vita, vile vile na kwa kumuua yeye mwenyewe. (2Wafalme 19:1-37). Ndicho kitakachotokea kwa Taifa la Urusi, litalidharau Taifa la Israeli na kumbe ndio litakuwa limejipeleka kwenye mwisho wake.

Vita hiyo ya Urusi na Israeli, ipo karibuni sana kutokea, ghafla tu, litanyanyuka kama lilivyoanza kwa Ukraine, na kupanga kuivamia Israeli, na wakati huo huo mataifa ya kiarabu yataungana..Baada ya hapo dunia itakuwa imebakisha vita moja ya Harmagedon, (ya Mungu mwenyezi na mataifa yote ya dunia yaliyosalia).

Na unyakuo wa kanisa unaweza kutokea kipindi kifupi kabla ya vita hii, au kipindi kifupi baada ya vita hiyo (ya Urusi na Israeli), kutokea..

Lakini yote katika yote ni kwamba tunaishi katika siku za Mwisho, na Yesu yupo mlangoni kurudi, kuwachukua watakatifu wake. Je umejiandaaje?

Umempokea Bwana Yesu?, umebatizwa?, umepokea Roho Mtakatifu?.. kama bado unangoja nini leo hii usiokoke.. Au unasubiri siku ile ya hukumu ya Mungu ikujie kwa ghafla?

1Wathesalonike 5:3 “Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa”.

Kama leo hii umeamua kuanza Maisha ya wokovu, kwa kumpokea Bwana Yesu Maishani mwako, basi unaweza kuwasiliana nasi kwa namba hizi hapa chini, ili tukuongoze sala ya Toba, itakayomkaribisha Yesu ndani yako.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

JE NI KWELI SAMAKI NGUVA YUPO?

NAYE AKASIMAMA JUU YA MCHANGA WA BAHARI.

Chuo cha vita vya Bwana ni kipi?(Hesabu 21:14)

MAUAJI YA HALAIKI NDANI YA KANISA.

MAISHA ULIYOPITIA NYUMA NI USHUHUDA TOSHA WA WEWE KUMTUMIKIA MUNGU

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
10 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Edson Mugisha
Edson Mugisha
1 year ago

Naiombea huduma hii ikue, ipae juu kama tai kuliko jana kwa jina la BWANA YESU!

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Hakika imenibariki

Dionis
Dionis
2 years ago
Reply to  Anonymous

Ninabarikiwa na huduma hii…Mungu awabariki.

cleophace shukuru
cleophace shukuru
2 years ago

Mungu ni mkuu mno. hakuna kilichosemwa katika biblia kisichodhihirishwa. MUNGU awabariki mno na kuzidi.

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Amen..ni wakati wa kuwa macho sana, Bwana Yesu yu karibu.

lucas mhula
lucas mhula
2 years ago

Amen 🙏🙏

enock amilio
enock amilio
2 years ago

Hakika mimi nitasimama katika mnara nimsikilize Mungu