“Vya Kaisari mpeni kaisari”  ni vipi hivyo tunavyopaswa tumpe?.

“Vya Kaisari mpeni kaisari”  ni vipi hivyo tunavyopaswa tumpe?.

Na pombe na sigara si ni vya Kaisari (yaani serikali imevihalalisha), hivyo si ni sawa kuvitumia..?

Jibu: Kumekuwa na tafsiri nyingi juu ya huo mstari “Vya Kaisari mpeni Kaisari na vya Mungu mpeni Mungu”… Wengine wanatafsiri vya Kaisari kama vitu vyote viovu vya ulimwengu.. Hivyo tumepewa ruhusa ya kuvifanya hivyo, lakini pia tusiache kuvifanya vya Mungu.. “Kwamba tunapoenda disko hapo tumempa Kaisari vya kwake, vile vile tunapoenda kanisa, hapo tumempa Mungu vya kwake”..

Lakini je! Hiyo ndio tafsiri yake au ndio maana ya huo mstari?

Tusome..

Luka 20:21 “Wakamwuliza, wakisema, Mwalimu, twajua ya kwamba wasema na kufundisha yaliyo ya haki, wala hujali cheo cha mtu, bali unafundisha njia ya Mungu kwa kweli

22 JE! NI HALALI TUMPE KAISARI KODI, AU SIVYO?

23 Lakini yeye alitambua hila yao, akawaambia,

24 Nionyesheni dinari. Ina sura na anwani ya nani? Wakamjibu, Ya Kaisari.

25 Akawaambia, Basi, vya Kaisari mpeni Kaisari, na vya Mungu mpeni Mungu”.

Hapo utaona Vya Kaisari Bwana alivyovimaanisha ni “KODI” na mambo yote yanayofanana na hayo..(Kwa ufupi mambo yote mema)..kama Ushuru, uwajibikaji, utulivu, amani n.k

Ndio maana Bwana akawauliza swali, sarafu hiyo ina sura ya nani?..wakajibu ya Kaisari..na ndipo akajibu vya Kaisari mpeni Kaisari..Maana yake vile vyote Kaisari anavyovihimiza na kuvihitaji vya lazima  “basi apewe” kwasababu havihitaji kwa lengo baya!!.. bali zuri kwa watu wake!.

Kama maandiko yanavyosema katika…

1Wakorintho 13:3 “KWA MAANA WATAWALAO HAWATISHI WATU KWA SABABU YA MATENDO MEMA, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? FANYA MEMA, NAWE UTAPATA SIFA KWAKE;

4 kwa kuwa yeye ni MTUMISHI WA MUNGU KWAKO KWA AJILI YA MEMA…”

Umeona hapo?.. maandiko yanasema watawalao ni watumishi wa Mungu kwako KWA AJILI YA MEMA!!…Kwahiyo yote ya lazima ambayo Kaisari aliyahitaji kutoka kwa watu, ni mambo MEMA na si Mabaya!!

Sasa mambo hayo ni yapi?..ambayo Kaisari aliyahitaji na ambayo ni lazima “apewe”?

 1. KODI

Kaisari alihitaji “kodi” na lengo la kodi, sote tunajua kuwa sio Baya!….kwasababu kodi hazitumiki kwenda kumnufaisha yeye, bali kuwanufaisha wananchi wote, kwa kutengeneza miundo mbinu ya msingi, na matumizi mengine muhimu.. Hivyo Taifa lisilokusanya kodi haliwezi kuendelea.. Kwahiyo Kodi ni jambo ambalo halikinzani na Neno la Mungu..Ndio maana Bwana Yesu akaamuru tuwape kodi wenye mamlaka.

1Wakorintho 13:6 “KWA SABABU HIYO TENA MWALIPA KODI; KWA KUWA WAO NI WAHUDUMU WA MUNGU, WAKIDUMU KATIKA KAZI IYO HIYO.

7 Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima”.

 2. AMANI na UTULIVU.

Kaisari, alihubiri “Amani na utulivu”…kwasababu watu wakiwa watulivu, Ufalme wake utajengeka… hivyo hakuhitaji wauaji, hakuhitaji waasi, hakuhitaji watu wenye vurugu, hakuhitaji wezi, hakuhitaji wahuni n.k.

Hivyo mtu akiwa muuaji, (alikuwa hajampa Kaisari yaliyo yake)…kwasababu yeye alikuwa anahitaji watu walio wazuri (na ilikuwa ni amri sio ombi)…Ilikuwa si ruhusa kuua mtu, wala kujichukulia sheria mkononi n.k”.

Na mambo mengine yote ya lazima, (kumbuka yapo mambo ya lazima ambayo wenye mamlaka waliyaagiza na yapo yasiyo ya lazima).. Hakuna Mfalme anayewalazimisha watu wake wanywe pombe!..lakini atawalazimisha wawe na Amani na Utulivu na vile vile walipe kodi. Sasa mambo hayo ambayo ni ya Lazima, MENGI NI MAZURI!!.. Ndio maana Bwana aliamuru tuyafanye hayo.

Vile vile hata sasa… tunapaswa tunayo amri ya kumpa Kaisari yaliyo yake!.. (Tunapaswa tulipe kodi, au ushuru pale inapotubidi)..hali kadhalika sheria za nchi zinatulazimisha kuwa watulivu, watu wa amani na watiifu, na watu wa Staha..hatuna budi kuwa hivyo..(Na kwa kufanya hivyo tutakuwa tumempa Kaisari yaliyo yake)..Kwasababu mambo hayo hayakinzani na Neno la Mungu.

Lakini swali ni je!.. Kama vya Kaisari ni Kodi, ushuru, na mambo mengine yanayofanana na hayo, je ya Mungu nayo ni yapi?..Ambayo Bwana Yesu alisema tumpe!. (..Akawaambia, Basi, vya Kaisari mpeni Kaisari, NA VYA MUNGU MPENI MUNGU..”.

Tusome,

Mathayo 9:13 “Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi”.

Bwana anahitaji tumwombe yeye Rehema, (anahitaji tutubu)!.. Hicho ndio kitu cha kwanza anachokihitaji kutoka kwetu..na wala si sadaka zetu!!.. Sasa sio kwamba sadaka zetu hazina maana kwake la!.. zina maana kubwa sana, lakini kinachotangulia ni Rehema..

Tusome,

Mathayo 23:23 “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, NA REHEMA, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, WALA YALE MENGINE MSIYAACHE”.

Umeona hapo?..sadaka tunapaswa kumpa Bwana, lakini REHEMA ni muhimu Zaidi.. Toba ni muhimu sana…

Na toba halisi ni ile inayoendana na matendo.. Maana yake tunatubu, kwa kumaanisha kuziacha dhambi!.. Hicho ndicho Mungu anachokihitaji kwetu.. Hali kadhalika hata baada ya kutubu, na kukaa katika Imani, hatuna budi kuendelea kujitakasa kila siku, kwa Neno la Mungu..(Hayo ndio mambo ambayo Mungu anayataka kutoka kwetu).

Je umeokoka?.. Umetubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha, na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana Yesu Kristo?, na kupokea Roho Mtakatifu?…Na hata kama umeshaokoka.. je unajitakasa kila siku kwa Neno la Mungu??

Kama bado basi bado hujaanza kuyafanya mapenzi ya Mungu, haijalishi unatoa sadaka kiasi gani?.. Sicho kitu cha kwanza Mungu anachokihitaji kutoka kwako, bali anahitaji wewe upate Rehema kutoka kwake kwa kutubu.

Hivyo kama leo hii ungependa kutubu na kumkaribia Mungu Zaidi.. basi unaweza kuwasiliana nasi kwa namba (katika mwisho wa somo), ili tuweze kukuongoza sala fupi ya Toba..ambayo itamkaribisha Bwana Yesu katika Maisha yako.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Vyombo vya uzuri ni vipi vinavyotajwa katika biblia?

YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.

Bahari mbalimbali zilizoorodheshwa kwenye biblia.

Mizimu ni nini?

UFUNUO: Mlango wa 3 part 3

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments