MADHARA YA KUTOIJUA KWELI YOTE!

MADHARA YA KUTOIJUA KWELI YOTE!

Kuna madhara makubwa sana ya KUTOIJUA KWELI YOTE!.. Unaweza kuijua kweli tu!, lakini usiijue kweli yote…Watu wengi leo hii wanaijua kweli… “lakini hawaijui kweli yote”.. Jambo ambalo linafungua mlango mkubwa sana wa shetani kuleta Uharibifu.

Hebu tuangalie mfano wa watu wawili ambao waliijua kweli, lakini si YOTE!.

 1. MFALME ABIMELEKI

 Ibrahimu, alimwambia Mfalme Abimeleki kuwa Sara ni “Dada yake” ..lakini hakumwambia kuwa Sara pia ni “mke wake”.. alimwambia vile kwa hofu ya kuuawa..kwasababu Sara alikuwa ni mzuri wa uso.

Sasa sio kwamba Ibrahimu alimdanganya Mfalme Abimeleki!.. hapana! Hakumdanganya kwasababu ni kweli Sara alikuwa ni dada Ibrahimu.. Wameshea baba mmoja, ila mama mbali mbali. Kwahiyo alikuwa ni kweli dada yake. Hivyo hakumwambia uongo Mfalme Abimeleki.. Lakini tatizo ni kwamba hakumwambia KWELI yote!.. alimwambia kweli iliyo NUSU tu!.. na matokeo yake ni kumletea Abimeleki hatari ya kuawa na Mungu..

Tusome,

Mwanzo 20:1 “Ibrahimu akaondoka huko kwenda nchi ya kusini, akakaa kati ya Kadeshi na Shuri, naye akatembea katika Gerari.

 2 Ibrahimu akamnena Sara mkewe, Huyu ni ndugu yangu. Basi Abimeleki mfalme wa Gerari akapeleka watu akamtwaa Sara.

3 Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu.

4 Basi Abimeleki alikuwa hakumkaribia, akasema, Ee Bwana, Je! Utaua hata taifa lenye haki?

 5 Je! Hakuniambia mwenyewe, Huyu ni ndugu yangu? Na mwanamke mwenyewe naye alisema, Huyu ni ndugu yangu. Kwa ukamilifu wa moyo wangu, na kwa kuwa safi mikono yangu, nimefanya hivi.

6 Mungu akamwambia katika ndoto, Nami nimejua ya kwamba kwa ukamilifu wa moyo wako umefanya hivi, ndipo nami nikakuzuia usinitendee dhambi, kwa hiyo sikukuacha umguse.

7 Basi sasa umrudishe mwanamke kwa mtu huyo, maana yeye ni nabii, naye atakuombea, upate kuishi. Bali usipomrudisha, fahamu ya kwamba kwa hakika utakufa wewe na watu wote ulio nao.

 8 Abimeleki akaamka asubuhi na mapema, akawaita watumwa wake wote, akawaambia maneno hayo yote masikioni mwao, nao watu hao wakaogopa sana.

9 Kisha Abimeleki akamwita Ibrahimu, akamwambia, Umetutenda nini? Nimekukosa nini, hata ukaleta juu yangu na juu ya ufalme wangu dhambi kuu? Umenitenda matendo yasiyotendeka.

10 Abimeleki akamwambia Ibrahimu, Umeona nini hata ukatenda jambo hili?

11 Ibrahimu akasema, Kwa sababu naliona, Yakini hapana hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa ajili ya mke wangu.

12 NAYE KWELI NI NDUGU YANGU, BINTI WA BABA YANGU ILA SIYE MWANA WA MAMA YANGU, NDIPO AKAWA MKE WANGU”.

Umeona hapo mstari wa 12?.. “Ibrahimu hakusema uongo, alisema Kweli lakini si yote”

 2. HAWA

Hawa aliambiwa ukweli na shetani, lakini hakuambiwa ukweli wote!.. Aliambiwa kwa kula tunda, “Atakuwa kama Mungu, akijua mema na mabaya”..huo ni ukweli kabisa! Kwani alipokula tu lile tunda, alikuwa kama Mungu kwa kujua mema na mabaya…

Mwanzo 3:22 “Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele”

Lakini shetani hakumwambia ukweli wote kwamba, licha ya kuwa utakuwa kama Mungu akijua mema na mabaya lakini Zaidi ya hayo, atakuwa pia amejitenga mbali na uwepo wa MUNGU, na umemuasi Mungu moja kwa moja. (Hayo hakumwambia)..kwasababu laiti angemwambia Hiyo kweli yote!, Hawa asingelisogelea lile tunda!.

Umeona Madhara ya kutoijua kweli yote?..

Yalimletea Mfalme Abimeleki hatari ya kifo, kwa kumtwaa Sara.. vile vile, yalimletea Hawa anguko kubwa ambalo mpaka leo tunaona madhara yake.

Vile vile shetani leo hii, anawaambia watu ukweli, lakini hawaambii kweli yote!..na watu wanajitumainisha katika ile kweli, lakini hawataki kuitafuta kweli yote..

Kwamfano Neno linasema, kila amwaminiye Bwana Yesu amevuka kutoka mautini kuingia uzimani..

Yohana 5:24 “Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani”.

Hiyo ni KWELI KABISA!..Lakini kweli yote inasema hatuna budi kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu na kuishi Maisha matakatifu baada ya hapo..

Mathayo 16:16 “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.

Maana yake hatuishii kumwamini Bwana Yesu tu!, halafu basi..bali tunapaswa pia tubatizwe!..Na pia haiishii kubatizwa tu..bali pia tunapaswa tujazwe Roho Mtakatifu na tuishi Maisha matakatifu baada ya hapo ndipo tutakapomwona Mungu..

Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, NA HUO UTAKATIFU, AMBAO HAPANA MTU ATAKAYEMWONA BWANA ASIPOKUWA NAO”.

Na sio tu katika eneo la wokovu tunahitaji kuijua kweli yote, bali katika mambo mengine yote!.. leo hii watu wanaamini kuwa Mungu anaangalia moyo!..Hiyo ni kweli, lakini SI KWELI YOTE!.. Kweli yote inasema..

Warumi 12:1 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana”.

Na tena inasema..

1Wakorintho 6:19 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe”

Kwahiyo hatupaswi miili yetu, kuivika vibaya, hatupaswi kuichora, kuitoboa toboa, kuilevya, au kuiharibu kwa namna yoyote ile.(www wingulamashahidi org)

Sasa swali la kujiuliza?..Utawezaje kuijua KWELI yote!.

Ashukuriwe Mungu, kwa zawadi ya Roho aliyotumwagia.. huyo ndio suluhisho la mambo yote..

Yohana 16:13 “Lakini yeye atakapokuja, HUYO ROHO WA KWELI, ATAWAONGOZA AWATIE KWENYE KWELI YOTE; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe…”

Je! Leo unataka kuyajua mapenzi ya Mungu, katika ukamilifu wote?..unataka kuijua kweli yote ya Maisha yako ya kiroho na kimwili?..Basi tafuta Roho Mtakatifu…sasa utauliza, utampataje Roho Mtakatifu ndani yako?..Biblia imetupa kanuni..kuwa ni kwa kutubu, na kubatizwa..

Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38 PETRO AKAWAAMBIA, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, NANYI MTAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU.

39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”.

Bwana akubariki

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Ni madhara gani yatampata mtu yule anayetafsiri Neno isivyopaswa!

NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?

NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?

Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?

MUUNGANO WA DINI NA MADHEHEBU YOTE, UMEKARIBIA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
2 years ago

Amen barikiwe mnoo🙏🙏