JE NI KWELI SAMAKI NGUVA YUPO?

JE NI KWELI SAMAKI NGUVA YUPO?

Je ni kweli kuna samaki nguva?..Je kwenye  biblia nguva katajwa?

Jibu: Ukweli ni kwamba hakuna mahali popote katika biblia palipotajwa uwepo wa samaki aina ya nguva. Maana yake ni kwamba hakuna kiumbe cha namna hiyo kilichoumbwa na Mwenyezi Mungu.

Lakini utauliza je! hicho wanachokiona watu ni nini? ambacho kimaumbile kinaonekana nusu mtu nusu samaki?

Jibu ni kwamba vinavyoonekana na watu vyenye umbo kama hilo ni roho za mapepo. Kumbuka biblia inasema shetani anao uwezo wa kujigeuza na kuwa hata Malaika wa Nuru (Kasome 2Wakorintho 11:14), sasa si zaidi kujigeuza na kuwa kiumbe kiumbe kingine chochote chenye umbo la ajabu?. Anao huo uwezo, anaweza kujiguza na kuwa kama nusu mtu nusu mbuzi, anaweza kujigeuza na kuwa nusu mtu nusu nyoka, vivyo hivyo anao uwezo wa kujigeuza na kuwa nusu mtu nusu samaki (ambao ndio hao wanaojulikana kama nguva).

Sasa shetani na mapepo yake wote wanao huo uwezo wa kujigueza na kuwa hivyo viumbe vya ajabu..Na lengo lao ni lile lile moja..Kuwapoteza wanadamu na kuwaweka mbali na kweli ya Mungu, na hatimaye wafe katika dhambi zao na kuingia Jehanamu ya moto, wala hana lingine. Hivyo shetani kila siku anabuni njia mpya za kuwafanya watu wawe wabaya zaidi na kuzidi kuuamini uongo wake.

Sasa haya mapepo ambayo yanajigeuza maumbile..huwa hayawatokei wala hayawaingii watu waliookoka (Yaani waliomwamini Yesu Kristo na kuoshwa dhambi zao kwa damu yake). Huwa yanawatokea na kuwaingia watu ambao katika roho wapo dhaifu sana, na hao ni wale wote ambao wapo nje ya Neema ya Yesu Kristo. Huwa yanawajia katika ndoto, kuwahimiza kufanya jambo fulani lililo kinyume na neno la Mungu au kuwapa hisia ambayo ni kinyume na Neno la Mungu..

Na hisi kubwa na ya kwanza yanayopeleka kwa mtu ni hisia ya ZINAA na UASHERATI. Kwasababu hiyo ndio dhambi ya kwanza ambayo shetani anatumia kumwangusha nayo mwanadamu na ndio Dhambi ya asili.

Hisia ya pili ni.. kutenda mabaya, aidha kuabudu sanamu, au miungu, kuwa mshirikina, au wakati mwingine yanamletea mtu hisia za kuwa na chuki na jamii ya watu fulani, au mtu fulani na kumpeleka hata kutamani kuua, au kuiba au kudhuru. Hiyo ndio kazi ya mapepo hayo yanapomwingia mtu ndani yake…na haya yana majina mengi (wengine wanayaita majini, wengine vibwengo n.k)..lakini ndio hayo hayo mapepo…

Mapepo haya yakiwemo hayo yanayojigeza na kuwa huo mfano wa nguvu, huwa hayamtokea mtu kwa macho, yanakuwa ni roho ambazo zinamwingia mtu au zinatembea na mtu, na mtu anaweza kuziona tu katika ndoto..lakini si katika macho ya asili..Lakini pia kama mtu huyo hali yake ya roho ipo chini sana yanaweza kumtokea kabisa na akayaona dhahiri, wengi wa wanaoyaona hayo ni wale ambao ni wachawi au waganga, au washirikina…ambao wameshajiuza kwa shetani kikabisa.

Kwahiyo nguva si kiumbe kilichoumbwa ambacho kinaishi baharini, bali ni roho za mapepo, kama umewahi kuota upo na nguva au umewahi kumwona..Basi tambua kuwa hali yako katika roho ipo chini sana na ni hatari.

Hivyo suluhisho ni kumpa Yesu maisha yako, unapoamua kugeuka na kutubu kwa kumaanisha kuacha dhambi na maisha ya machafu uliyokuwa unaishi huko nyuma, na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi, roho hizo zitakuacha hata pasipo kwenda kuwekewa mikono na mtu yoyote na utakuwa huru mbali na utumwa wa roho za mapepo.

Bwana akubariki sana.

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
lucas mhula
lucas mhula
2 years ago

Asante sana wana wa Mungu mbarikiwe kwa kutufanya kuijua kweli ya Mungu siku hadi siku mimi mda mwingine naona kukutana nanyi kwenye mitandao hii ni muujiza kuliko muujiza tuliyo izoea, Mungu aendelee kuwapa ufunuo wake siku hadi siku.🙌🙌🤝🙏

Ben Japhet
Ben Japhet
3 years ago

Hakika nabarikiwa kwangu mafundisho haya ni makubwa na makuu sijui ningeyapata wapi bila nyinyi kuwepo Mungu azidi kuwa nanyi siku zote za uhai wenu,Nami ni Ben Japhet wa dar es salaam tabata