MAJINI WAZURI WAPO?

MAJINI WAZURI WAPO?

Majini ni nini? Je kuna majini wazuri?, je pete za majini ni zipi? na namba za majini ni zipi?..Je kuna njia yoyote ya kupata utajiri wa haraka?

JIBU: Kwanza ni vizuri kufahamu majini ni nini?…Majini ni jina lingine la roho zilizoasi mbinguni, ambazo zilitupwa chini duniani pamoja na lusifa ambaye ndiye alikuwa kiongozi wao.

Majini jina lingine yanaitwa mapepo..wakati wakiwa mbinguni lusifa ambaye ndiye shetani aliwadanganya wasimame kinyume cha Mungu na kutaka kuwa kama Mungu…Lakini walishindwa vita vile na Malaika walio upande wa Mungu na kuishiwa kutupwa chini duniani.

Ufunuo 12:7 “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.

9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye”

Kazi ya majini haya baada ya kutupwa duniani ni kwenda kinyume na kusudi la Mungu juu ya mwanadamu. Hivyo yanapambana usiku na mchana kuhakikisha kusudi la Mungu juu ya mwanadamu halifanikiwi. Majini haya au kwa lugha nyingine mapepo hayataki mwanadamu hata mmoja afike mbinguni. Hivyo yanatumia ujuzi wao na akili zao zote kuhakikisha yanatimiza malengo yao.

Kumbuka walioposhindwa vita mbinguni (kama tunavyosoma katika kitabu cha Ufunuo 12) hawakunyang’anywa na Mungu nguvu walizokuwa nazo wala ujuzi..walifukuzwa wakiwa na nguvu walizopewa na Mungu kadhalika na fahamu zao…Hivyo wanazo mpaka sasa nguvu… Ingawa sisi tuliookoka tumepewa nguvu zilizo kuu zaidi zao kupitia damu ya Yesu Kristo.

JE KUNA MAJINI WAZURI?

Majini wote ni wabaya hakuna jini hata mmoja aliye mzuri. Shetani aliye mkuu wa majini hayo anatumia nguvu kubwa kuwadanganya watu kwamba kuna majini wazuri..lengo lake ni ili watu wajishughulishe kuzitafuta roho hizo na kujishikamanisha nazo. Na kwa pamoja wafanye kazi ya kuziangusha roho nyingine.

JE PETE ZA MAJINI NI ZIPI?

Majini yanaweza kumwingia mtu yoyote kwa kupitia njia yoyote ile ambayo ipo kinyume na mapenzi ya Mungu sio pete tu!..Majini/mapepo yanaweza kumwingia mtu kwa kupitia mawigi ya kichwani, kwa kupita vipodozi, wanja, kwa kujichora tattoo,kwa kufanya ibada za sanamu na pia njia kuu ni kwa kupita kufanya uasherati na mtu ambaye si mke wako au mume wako na pia kwa kuangalia picha za ngono. Pete inaweza kuwa ni njia ya mwisho kabisa ya kuingiza majini ndani ya mtu.

Mtu anapokwenda kwa mganga au anapojiunga na kikundi fulani cha kichawi kama freemason na vingine anaweza kukabidhiwa pete, mkufu, picha au chochote kile…vitu hivyo ni mlango pia wa kuingiza roho za majini ndani ya mtu.

JE NAMBA ZA MAJINI NI ZIPI?

Maelfu ya watu wasio na ufahamu wanazunguka mitandaoni kutafuta namba za majini..Majini ni roho! hayawezi kuwa na namba za simu za mkononi. Mawakala wao ambao ni waganga wa kienyeji na wachawi ndio wenye namba za simu lakini si mapepo. Hayo ni maroho yanafanya kazi katika ulimwengu wa roho…

JE KUNA NJIA YOYOTE YA KUPATA UTAJIRI WA HARAKA KUPITIA MAJINI?

Uongo mkubwa shetani anaowadanganya wengi ni kwamba kwake kuna fedha za bure na za haraka!..Nataka nikuambie ndugu hicho kitu hakipo..lengo la shetani ni kukupeleka tu kuzimu hakuna lingine.

Njia ifuatayo ndiyo anayoitumia shetani kuwapatia watu mali kwa njia ya majini.

1.Anatumia mtu jini/pepo..Lile pepo linaweza kuwa la aina yoyote ile, aidha zinaa, ulevi, wizi, uuaji n.k Sasa lile jini, tuchukue mfano la zinaa linapomwingia mtu..au mtu anapokwenda kwa waganga kutafuta mali anapewa pete..Na ile pete ndani yake imebeba mojawapo ya hilo jini..labda tuseme la zinaa..Mtu anapoivaa lile pepo la zinaa linamwingia..yule mtu akitoka pale anakuwa mwasherati kupita kawaida…kama ni mwanamke anakuwa ni kahaba kupita kawaida…na hivyo linamsukuma kwenda kufanya kazi ya ukahaba. Na kwa kupitia hiyo kazi ya ukahaba ndipo anapopata fedha.. Lakini si kwamba anakaa tu na kisha fedha zinaingia.

Kadhalika na wizi, ni hivyo hivyo..pepo la wizi linamwingia na linakwenda kumfanya kuwa mwizi hodari..na kwa wizi ule anapata mali zisizohalali.

Na hivyo hivyo mauaji..Pepo linamwingia mtu na kumfanya aone kuua sio shida tena na kwa kupitia mauaji yale anapata kazi nyingi za ujambazi na hivyo kupata fedha kwa kazi hiyo.

Kwahiyo hakuna fedha za bure kwa shetani..Anakupa jini/pepo na jini hilo linakwenda kukutumikisha kupata hizo mali. Na hautakaa tu baada ya kuipokea hiyo pete..kwamba fedha zidondoke.

Hata wale wanaofanya uchawi ujulikanao kama chuma ulete..Nao pia wanavalishwa pepo hilo ambalo linawafanya wateseke kwa hali na mali kufanya uchawi huo..gharama wanazotumia kufanya uchawi huo ni mkubwa kuliko hata faida wanazozipata huko.

Hivyo kuyatafuta majini au kujishughulisha nao ni kujitesa na ni kwenda kinyume na mpango wa Mungu…Kufanya kazi na majini/mapepo ni kuwa Adui wa Mungu rasmi asilimia 100. Na kujitengenezea daraja zuri la kuwa miongoni mwa watakaoteswa sana katika ziwa la moto baada ya hukumu.

Na madhara ya kuwa na majini ni mauti..Majambazi wote kama Neema ya Kristo haitawapitia wanaishia kupigwa risasi, makahaba wote kama Neema ya Kristo haitawafikia wanaishia kufa kwa magonjwa…vivyo hivyo wezi wanaishia kuchomwa moto..Mafisadi wanaishia kufungwa..wachawi wanaishia kufa kifo cha ghafla n.k

Sasa kwanini kudanganyika na uwongo wa shetani kwamba kwake kuna fedha za bure?..Kwamba ni kuvaa pete tu, ni kuchinja mbuzi tu!..shetani anakuambia ni kuvaa pete tu lakini hakuambii ukahaba atakaokwenda kukutumikisha nao.

Hivyo kama Kama hujampa Kristo maisha yako. Mgeukie Leo..usitafute mali wala msaada kwa shetani na wala hakuna majini wazuri watakaokusaidia kupunguza ugumu wa maisha..shetani yeye kashaasi, anachokisubiria tu ni kutupwa katika ziwa la moto..na anataka kwenda na wengi..hivyo anatumia uongo wa kila namna kujaribu kuvuta watu kwake..tumwache aende yeye peke yake sisi tumgeukie Kristo tumaini la utukufu.

Bwana akubariki sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii 0789001312

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi


Mada Nyinginezo:

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Deodictor Panja
Deodictor Panja
2 years ago

Wazuri wapo kweli

Anonymous
Anonymous
3 years ago

Jini urudisha aje?

Anonymous
Anonymous
3 years ago

Jini ni nini

Saimon maina karumbe
Saimon maina karumbe
4 years ago

nataka