Karibu tujifunze biblia na huu ni mwendelezo wa kitabu cha Ufunuo leo tukiwa katika ule mlango wa 19,
Tunasoma..
1 Baada ya hayo nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, sauti kubwa mbinguni, ikisema, Haleluya; wokovu na utukufu na nguvu zina BWANA MUNGU wetu. 2 kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki; maana AMEMHUKUMU YULE KAHABA MKUU aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake. 3 Wakasema mara ya pili, Haleluya. Na moshi wake hupaa juu hata milele na milele. 4 Na wale wazee ishirini na wanne, na wale wenye uhai wanne, wakasujudu na kumwabudu Mungu, aketiye katika kile kiti cha enzi, wakisema, Amina, Haleluya. 5 Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu. “
2 kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki; maana AMEMHUKUMU YULE KAHABA MKUU aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake.
3 Wakasema mara ya pili, Haleluya. Na moshi wake hupaa juu hata milele na milele.
4 Na wale wazee ishirini na wanne, na wale wenye uhai wanne, wakasujudu na kumwabudu Mungu, aketiye katika kile kiti cha enzi, wakisema, Amina, Haleluya.
5 Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu. “
Katika mistari hii ya mwanzo tunaona mbingu ikishangalia kuanguka kwa yule mwanamke kahaba ambaye aliyewakosesha watu wote na kuiharibu nchi kwa uasherati wake, kama tulivyoona katika sura iliyotangulia ya 18. Na kahaba huyu si mwingine zaidi ya kanisa Katoliki
na ni kwa jinsi gani alihukumiwa? Tunasoma Mungu alitumia zile pembe 10 (Ufunuo 17:16) ambayo ni mataifa 10 yatakayounda umoja wa ulaya kwa wakati huo, ndio yatakayomkasirikia yule mwanamke kahaba na kumtekeza kabisa kwa moto,kwa maelezo marefu juu ya hukumu ya yule kahaba fautilia link hii >>> UFUNUO 18
Na ndio sababu tunaona mbingu zikishangalia, zikisema hukumu za Mungu ni za haki kwa kuwa kahaba huyu alimwaga damu za watakatifu wengi wa Mungu na ndio maana hukumu yake ikaja na moshi wake hupaa juu hata milele na milele kuashiria kuwa pigo lake haliponyeki ni la kifo cha milele wala hata kaa anyanyuke tena kuwakosesha watu wanaokaa juu ya nchi kwa uasherati wake. Mstari wa 5 unasema..
5 Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu.
KARAMU YA HARUSI YA MWANA-KONDOO.
Tukiendelea kusoma mstari wa 6-10.
6 Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki. 7 Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari. 8 Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu. 9 Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu. 10 Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.
6 Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki.
7 Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.
8 Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.
9 Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.
10 Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.
Katika vipengele hivi, Arusi ya mwanakondoo inazungumziwa na mkewe amekwisha jiweka tayari, kumbuka kuna tofauti kati ya Arusi na Karamu,. Siku zote ndoa ikishafungwa (Arusi), kinachofauta ni KARAMU, Kwahiyo Karamu ni sherehe ya kuifurahia “ndoa/arusi mpya”. Vivyo hivyo na kwa YESU KRISTO kama Bwana Arusi yeye naye ana bibi-arusi wake ambaye ndio KANISA lake TAKATIFU bikira safi asiye na mawaa.
Kwahiyo katika ukristo NDOA hii inaendelea sasa hivi kufungwa duniani na hii ilishaanza tangu kipindi BWANA YESU alichopaa kwenda mbinguni mpaka leo, katika vile vipindi vyote 7 vya makanisa , na amekuwa akikusanya bibi-arusi wake kwa kila kipindi na kila nyakati na hadi sasa anaendelea kufanya hivyo,takribani miaka 2000 sasa. Na kuoana huko ni kati ya MTU na NENO LA MUNGU, na kama tunavyofahamu NENO ni YESU KRISTO MWENYEWE, hivyo wale walishikao na kuliishi NENO ndio waliooana na KRISTO
Na sio mkristo vuguvugu anayesema mimi nimeokoka halafu haliishi na halipokei NENO LA MUNGU, kwa mfano ukimwambia mtu biblia inasema hivi yeye anasema dhehebu langu halinifundishi hivyo, ukimuuliza ni kwanini ubatizo wa watoto wachanga haulingani na NENO la Mungu atakwambia dini yetu haifundishi hivyo. Mtu anajiita mkristo lakini anaupenda ulimwengu kuliko kumpenda Mungu, ukimuuliza kwanini unakunywa pombe, atasema dini inaruhusu kunywa pombe, acha kuhukumu, hapo mtu huyo anakuwa ameoana na ulimwengu badala ya Kristo (NENO), Hivyo anafanya uasherati mkuu wa kiroho.
Kwahiyo fahamu ndoa inaendelea sasa hivi katika roho, usipoana na KRISTO (NENO LA MUNGU), utaona na shetani kwa mafundisho yake ya uongo yanayolipinga NENO LA MUNGU. Kwahiyo ni vizuri sasa hivi ukajitambua upo upande upi?.
Mtume Paulo alisema katika 2Wakorintho 11:2-4″ Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi”.
Hivyo ni jukumu kwa kila nayejiita mkristo sio tu kuwa bikira bali kuwa BIKIRA SAFI!!
Tukisoma katika mathayo 25 tunaona mfano ya wale wanawali li kumi (10), watano werevu na watano wakiwa wapumbavu. Kumbuka wote 10 walikuwa MABIKIRA wakimngoja Bwana wao, lakini kilichowatofautisha ni kwamba wale wapumbavu hawakuwa na mafuta ya ziada katika taa zao ambayo ni “ufunuo wa NENO LA MUNGU katika ROHO MTAKATIFU”,. jambo hilo tu liliwafanya wasiingie KARAMUNI japo wote walikuwa ni mabikira, kwahiyo kujiita mkristo tu haitoshi ni lazima pia uwe na ufunuo wa NENO LA MUNGU, na ndoa inafanyika hapa duniani lakini KARAMU itafanyika mbinguni pale bibi-arusi safi atakapokwenda kwenye unyakuo.
Kama tunavyosoma wale 5 werevu waliingia karamuni bali wale wapumbavu walifungiwa nje vivyo hivyo katika hichi kipindi cha mwisho kutakuwa na makundi mawili ya wakristo, werevu na wapumbavu, werevu ni wale wanaolishika na kuliishi NENO LA MUNGU bila kujali kitu kingine chochote, hao wataenda na Bwana na kuingia katika KARAMU YA MWANAKONDOO, Lakini wale wapumbavu wasiojiweka tayari, kwa kukataa uongozo wa Roho Mtakatifu katika NENO lake, hawa watatupwa giza la nje! kwenye dhiki kuu, wakati wenzao wanafurahi na Bwana katika utukufu mbinguni na kupewa thawabu zao za milele na ndio maana mstari wa 8 tunasoma bibi-arusi ” ..amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.”
Katika hii karamu kutakuwa na mambo ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia mambo ambayo Kristo kawaandalia hao wateule wake (yaani bibi-arusi wake safi), hawa watakuwa na miili ya utukufu sana na ndio baadaye watashuka na BWANA kuja kutawala aulimwengu kwa muda wa miaka 1000 wakiwa kama makuhani na wafalme wa dunia nzima,uzao mteule, watu wa milki ya Mungu, na BWANA YESU KRISTO, akiwa kama BWANA WA MABWANA, na MAFALME WA WAFALME. haleluya!!. Kosa kila kitu ndugu lakini usiikose hiyo karamu, uchungu siku hiyo hautakuwepo sana katika mateso ya dhiki kuu, hapana bali uchungu utakuja sana pale utakapogundua kuwa umekosa thawabu za milele, na usidanganyike eti huko tunapokwenda wote tutakuwa sawa tunafanana! hayo mawazo futa, kule kutakuwa na madaraja tofauti tofauti, wapo watakaokuwa wakuu sana, na wakawaida sana na ni itakuwa hivyo milele, kwanini leo hii unang’ang’ana na vitu vinavyoharibika usijiwekee hazina mbinguni?.
Mstari wa 9 unasema “.. Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.”
VITA YA HAR-MAGEDONI
11 Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. 12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. 13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu. 14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi. 15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo ala mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi. 16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA. 17 Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu; 18 mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa. 19 Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake. 20 Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti; 21 na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.
12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.
14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.
15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo ala mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.
16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.
17 Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu;
18 mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa.
19 Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake.
20 Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;
21 na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.
Katika aya hizi tunaona Yohana akionyeshwa mbingu zikifunguka na kuona farasi mweupe, na yeye aliyempanda, anaitwa Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. Huyu sio mwingine zaidi ya BWANA YESU KRISTO na hapo anaonekana akiwa na vilemba vingi juu ya kichwa chake ikiashiria kuwa anamiliki juu ya wafalme wengi,
Na anaonekana pia akishuka pamoja na jeshi la mbinguni, sasa kumbuka hili jeshi sio malaika bali ni wale watakatifu (bikira safi) waliokuwa wamekwishanyakuliwa mbinguni sasa baada karamu kuisha watarudi duniani wakiwa kama MIALE ya moto kama BWANA alivyo, jambo hili tunaona Henoko miaka mingi iliyopita alionyeshwa Yuda 1:14 Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu,
15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake. “
Kwahiyo Bwana atakapokuja wafalme wote wa dunia watakuwa wamekusanyika tayari kupigana naye, mahali panapoitwa Harmagedoni huko Israeli (Ufunuo 16:16) pale zile pembe 10 za yule mnyama pamoja na wafalme kutoka mawio ya jua ambazo ni nchi za mashariki ya mbali kama Japan, China, Korea, Singapore n.k.
Ufunuo 16:12-16″ Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua. 13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. 14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi. 15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.) 16 Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni. “
Ufunuo 16:12-16″ Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.
13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.
14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.
15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)
16 Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni. “
lakini vita hii itadumu ndani ya muda mfupi sana, kwamaana KRISTO hapigani kwa kutumia silaha za kibinadamu, bali siku zote yeye anatumia NENO, kwasababu yeye mwenyewe ni NENO, na ndio maana tukisoma hapo juu jina lake anaitwa NENO LA MUNGU, kwahiyo kwa kuzungumza tu pale megido kutakuwa ni bahari ya damu, mabilioni ya watu watakufa, na kama tunavyosoma katika mstari wa “17 Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu;
Ndege wengi wataalikwa kuja kula nyama za watu wanajiona majemedari na wafalme wa nchi, kwahiyo unaweza ukatengeneza picha yatakuwa ni mauaji ya namna gani yeye ndiye atakayekanyaga lile shinikizo la ghadhabu ya Mungu, na ukisoma ufunuo 14:20, utaona shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, DAMU ikatoka katika shinikizo mpaka kwenye hatamu za farasi, kwa mwendo wa maili 200, “hii ni picha kuonyesha kwamba damu nyingi sana itamwagika kiasi cha kwamba ndege wengi wa angani watakusanyika kula nyama za mizoga ya watu.Hivyo vita hii ndio itakayohitimisha utawala mbovu wa dunia hii na kuleta utawala mpya wa BWANA YESU KRISTO duniani.
Na katika ule mstari wa mwisho tunasoma
20 “Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;
21 na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.”
Kwahiyo zile roho mbili kati ya zile tatu chafu kama vyura, zilishikwa na kutupwa katika lile ziwa la moto, kumbuka hapo anaposema mnyama na nabii wa uongo anamaanisha zile roho zilizokuwa zinawaendesha huyu mnyama na nabii wa uongo, lakini ile roho ya tatu ambayo ni roho ya shetani itafungwa kwa muda wa miaka 1000, kisha itafunguliwa tena kwa muda mfupi habari hii tutaisoma zaidi katika sura inayofuata ya 20,
Hivyo ndugu fahamu kuwa kanisa tunaloishi leo ni kanisa la mwisho la 7 linaloitwa LAODIKIA, na mjumbe wake ameshapita, muda wowote BWANA anakuja kumchukua bibi-arusi wake safi tu, aliyekwisha kujiweka tayari kwa kupokea Roho Mtakatifu na kuishi kwa NENO tu, je! umejiweka tayari kwenda naye? au utakuwa mwanamwali mpumbavu (yaani mkristo mpumbavu) vuguvugu?. Maombi yangu Bwana akufanye kuwa BIKIRA SAFI. ili sote siku ile kwa neema za BWANA TUKUTANE KATIKA ILE KARAMU YA MWANA KONDOO.
MUNGU AKUBARIKI.
Kwa mwendelezo >> UFUNUO: Mlango wa 20
Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara, kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.
Mada Zinazoendana..
KARAMU YA MWANA-KONDOO.
NDOA NA HARUSI TAKATIFU.
MAANDALIZI YA UJENZI WA HEKALU LA TATU YAPO TAYARI.
KUWA MAKINI NA MITANDAO, NI SHIMO REFU.
Rudi Nyumbani.
Print this post