NAYE AKASIMAMA JUU YA MCHANGA WA BAHARI.

NAYE AKASIMAMA JUU YA MCHANGA WA BAHARI.

Shalom, jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe milele.

Karibu tujifunze Neno lake.

Ukisoma kitabu cha Ufunuo sura ya 12, utaona habari kuu inayouzungumziwa pale ni kuhusu mapambano ambayo aliyafanya tangu akiwa mbingu mbinguni, na anayoendelea kufanya hadi sasa.

Utaona mapambano hayo yamegawanyika katika vipengele vikuu vitatu. Cha kwanza vita ile aliyoifanya mbinguni akiwa na malaika zake, ambayo alishindwa, na matokeo yake akatupwa chini,

Kipengele cha pili utaona ni ile vita aliyoifanya na yule mwanamke aliyemzaa mtoto mwanaume, ambaye nchi ilimsaidia. Na mwanamke yule analiwakilisha Kanisa la Israeli  kwa ujumla. Wakati Bwana Yesu anazaliwa, utaona shetani kwa kupitia Herode alikuwa ameshaanza kuleta maafa Israeli, kwa kuwaaua wale watoto wote waliozaliwa wakati mmoja na Yesu, lengo likiwa ni kumwinda Yesu, afe, Lakini Mungu akamuhamisha Kristo akilimbilie Misri kwa muda, na hiyo ilikuwa ni kulinusuru taifa zima.

Na kipengele za cha tatu na cha mwisho ambayo ndio kiini cha somo letu la leo  Ni vita ambayo shetani aliita kwa uzao wake wote wa huyo mwanamke uliosalia. Yaani wote watakaofanana na Kristo, waisraeli wa rohoni, hao ndio anamalizia kufanya nao vita , na vita hiyo ni endelevu, ilianza  tangu kipindi kile Kristo anaondoka duniani, mpaka leo hii, ni itaisha na unyakuo.

Lakini kuna jambo moja la kuona pale, shetani alipoanza kufanya vita na kanisa la Kristo, hakusimama mbinguni tena au nyuma yetu kuleta mafuriko, kama alivyofanya kwa yule mwanamke, hapana, bali biblia inatuambia alikwenda kusimama JUU YA MCHANGA WA BAHARI.

Ufunuo 12:13 “Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.

14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.

15 Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.

16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.

17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake AFANYE VITA JUU YA WAZAO WAKE WALIOSALIA, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; NAYE AKASIMAMA JUU YA MCHANGA WA BAHARI”.

Sasa mchanga wa bahari unawakilisha nini?

Hapo inaposema kwenye mchanga wa habari inamaanisha kwenye  ufukwe, yaani alikwenda kusimama ufukweni, mpakani, kati ya habari na nchi kavu. Hii ikiwa na maana vita vyake hasaa vipo pale mpakani, kuhakikisha kinachotoka habarini hakiji nchi kavu. Na hata kama kikitokea kimevuka nchi kavu, basi hakitapita hivi hivi tu.

Sasa kibiblia habari au palipo na maji mengi inawakilisha ulimwengu,(Ufunuo 17:15) ..Na nchi kavu ni wokovuni..Bwana Yesu alimwambia Petro njo nami nitakufanya kuwa mvuvi wa watu. Yaani kuwatoa watu kutoka kwenye ulimwengu na kuwaleta katika Nuru ya wokovu,

Hii ikiwa na maana mtu yeyote ambaye hajaokoka, kwamba yupo baharini, hivyo akishaokoka, ni anakuwa anahamishwa kutoka kwenye maji na kuletwa nchi kavu.

Hivyo sasa tunamwona hapa shetani kasimama ufukweni, lengo lake likiwa ni kukipinga kile kinachotoka kule kuja nchi kavu. Kumpinga mtu Yule ambaye anataka kutoka kwenye dunia na kuja katika wokovu. Mtu yule nayetaka kuacha kuishi maisha yake machafu na kuja katika maisha mapya ya utakatifu. Hapo ndipo vita vya ibilisi vilipo haswaa.

Hapo ndipo utakapokutana na shetani, hakuna mahali pengine utamwona ibilisi kwa uwazi wote kama hapo. Ndio vita vyake vilipo. Hatahangaika na wewe ambayo sikuzote upo dhambini, wala hutamwona akikugasi, lakini siku ambapo unafanya uamuzi ndipo utakapomwona akitaka kukusumbua, kama vile alivyotaka kumwangamiza Kristo tu alipozaliwa duniani.

Lakini ni wajibu wetu kumshinda, na tunamshinda kwa damu ya mwanakondoo na kwa Neno la ushuhuda wetu sawasawa na

Ufunuo 12:11 “Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa”.

Hivyo kaa ukijua kuwa pale unapotaka kufanya badiliko la kweli la maisha hapo ndipo pa muhimu sana, na shetani analijua hilo na ndio maana anasimamia hapo, kwahiyo ni wajibu wako kumshinda, haijalishi ataleta vita vya aina gani, Kumbuka hizi ni siku za mwisho, na Bwana Yesu alisema, ufalme wa mbinguni unapatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu ndio watakaouteka. Mathayo 11:12

Kwahiyo huna sababu ya kuanza kuogopa kudharauliwa, au kuchekwa, au kutengwa au kudhihakiwa kisa tu umeamua kuokoka au kuishi maisha ya wokovu. Jitwike msalaba wako umfuate Yesu, ili upokee taji la ushindi ufikapo kule.

Bwana akubariki

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

JINSI  DHAMBI ILIVYO NA SHINIKIZO KUBWA SANA.

JINSI SHETANI ANAVYOZUIA MAJIBU YA MAOMBI YETU.

KAMA MKRISTO FAHAMU ZIPO HATUA UTAPIGISHWA NA MUNGU.

JIFUNZE KUTOA KATIKA HAZINA YAKO VITU VIPYA NA VYA KALE.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Emmanuel Kitengule
Emmanuel Kitengule
2 years ago

Barikiwa sana mwalimu, naamini huu ni wakati wa kuijua KWELI kisawaswa na kuifuata.Tumekaa kwenye UONGO kwa muda mrefu na kuaminishwa huo lakini Mungu ni mwema anatuletea kweli ili tupone.