Ni wapi katika biblia panaonyesha kuwa suruali ni vazi la kiume tu? Na vipi juu ya kanzu!, mbona kama ni mfano wa gauni lakini linavaliwa na wanaume, kwanini Suruali isivaliwe pia na wanawake!
Jibu: Vazi la Suruali mara ya kwanza katika biblia lilivaliwa na Makuhani.
Mungu aliwapa amri makuhani watengeneze suruali ambazo zilitofautiana kimaumbile, waliambiwa watengeneze suruali fupi (yaani kaptula), Na vile vile walikuwa wanavaa zile ndefu ambazo zilifika kabisa mpaka chini kwenye viiko vya miguu.
Kutoka 28:41 “Nawe mvike huyo nduguyo Haruni na wanawe nao mavazi hayo; nawe watie mafuta, na kuwaweka kwa kazi takatifu, na kuwatakasa, ili wapate kunitumikia mimi katika kazi ya ukuhani. 42 Nawe wafanyie SURUALI ZA NGUO YA KITANI, ili kufunika tupu ya miili yao; suruali hizo zitafika tangu kiunoni hata mapajani; 43 na Haruni na wanawe watazivaa, hapo watakapoingia katika hema ya kukutania, au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike katika mahali patakatifu; wasije wakachukua uovu, wakafa; hii itakuwa ni amri ya milele kwake yeye, na kwa wazao wake”.
Kutoka 28:41 “Nawe mvike huyo nduguyo Haruni na wanawe nao mavazi hayo; nawe watie mafuta, na kuwaweka kwa kazi takatifu, na kuwatakasa, ili wapate kunitumikia mimi katika kazi ya ukuhani.
42 Nawe wafanyie SURUALI ZA NGUO YA KITANI, ili kufunika tupu ya miili yao; suruali hizo zitafika tangu kiunoni hata mapajani;
43 na Haruni na wanawe watazivaa, hapo watakapoingia katika hema ya kukutania, au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike katika mahali patakatifu; wasije wakachukua uovu, wakafa; hii itakuwa ni amri ya milele kwake yeye, na kwa wazao wake”.
Na katika Israeli hakukuwa na Kuhani Mwanamke!, Makuhani wote walikuwa ni wanaume. Hivyo lilikuwa ni vazi la kiume. (Soma pia Kutoka 39:27, na Walawi 6:10)
Vile vile tunaweza kulithibitisha hilo kipindi kile cha akina Shedraka, Meshaki na Abednego. Wakati Mfalme Nebukadneza alivyowatupa katika lile tanuru la moto, maandiko yanasema walitupwa kule hali wamevaa suruali zao na kanzu zao na joho zao.
Danieli 3:21 “Basi watu hao wakafungwa, hali wamevaa SURUALI ZAO, na kanzu zao, na joho zao, na mavazi yao mengine, wakatupwa katikati ya ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto. 22 Basi kwa sababu amri ya mfalme ilikuwa ni kali, na ile tanuru ilikuwa ina moto sana, mwako wa ule moto ukawaua wale watu waliowashika Shadraka, na Meshaki, na Abednego”.
Danieli 3:21 “Basi watu hao wakafungwa, hali wamevaa SURUALI ZAO, na kanzu zao, na joho zao, na mavazi yao mengine, wakatupwa katikati ya ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto.
22 Basi kwa sababu amri ya mfalme ilikuwa ni kali, na ile tanuru ilikuwa ina moto sana, mwako wa ule moto ukawaua wale watu waliowashika Shadraka, na Meshaki, na Abednego”.
Sasa Shedraka, Meshaki na Abednego hawakuwa wanawake, bali wanaume!, na hakuna popote katika biblia panataja au kuonyesha mwanamke kavaa suruali, kama hawa wakina Shedraki au kaagizwa kuvaa suruali kama hawa Makuhani.Hakuna!!. Ikifunua kuwa hilo ni vazi la kiume!
Maandiko yanasema.
Kumbukumbu 22:5 “Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako”.
Mwanamke yeyote kuvaa suruali ni machukizo mbele za Mungu, Suruali sio vazi la kumsitiri mwanamke, hakuna mwanamke yeyote anayevaa suruali na kuonekana kama kajisitiri, badala yake ataonekana kama kajidhalilisha au kajifunua..Na maandiko yanasema wanawake na wavae mavazi ya kujisitiri.
1Timotheo 2:9 “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani”
Hivyo mwanamke yeyote hapaswi kuvaa suruali, wala vimini wala nguo zozote zinazochora maungo yake.
Na pia Kanzu, halikuwa vazi la kike!, kanzu lilitumika kama vazi la Nje!, kama vile mtu anavyovaa koti!.. Ndio maana utaona hapo wakina shedraka, Meshaki na Abednego walikuwa wamevaa suruali na kanzu kwa nje. Kwahiyo Kanzu halikuwa gauni, Gauni ni vazi la kike lililotengenezwa mahususi kufuatia maumbile ya mwanamke!. Na ndilo wanawake wa kikristo wanapaswa walivae.
Sasa inawezekana ulikuwa hulijui hili kuwa hilo ni vazi la kiume, lakini leo umejua na ndani ya kabati lako kumejaa suruali, nataka nikuambie, usingoje kesho, leo leo zitoe kazichome moto!, wala usimpe mtu!.. zichome na tafuta magauno au sketi ndefu!, usiogope kuonekana mshamba mbele ya ulimwengu!. Ni heri uonekane mshamba lakini unakwenda mbinguni kuliko kuonekana wa kisasa lakini sehemu yako ni katika lile ziwa la moto!.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
USIYAACHE MAVAZI YAKO NA KWENDA UCHI!
Kwanini wale dubu waliowauwa vijana wa Elisha walikuwa wa kike?
PINDO LA VAZI LAKE SASA LIMEREFUSHWA.
VAZI LA YESU HALIGAWANYWI.
Rudi nyumbani
Print this post
Barikiwa sana, mafundisho ni mazuri sana yaliyojaa KWELI.
Ubalikiwe mtumishi,Mungu azid kukupa nguvu ya kusonga mbele huduma yako iko vizuri yesu kristo wa Nazareth akupe hitaji la moyo wako
Amen Bwana azidi kutubariki sote..
Vile vile usisahau kushare na wengine facebook na whatsapp katika kila mwisho wa somo..