KUMJUA YESU SI KUPATA UZIMA WA MILELE.

KUMJUA YESU SI KUPATA UZIMA WA MILELE.

Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana libarikiwe… Karibu tuyatafakari maandiko pamoja.

Katika dunia hii ya siku za mwisho, ni watu wengi sana wanaomjua Yesu, na maisha yake yote, jinsi alivyokuwa kwamba alizaliwa wapi, mama yake katika mwili alikuwa ni nani, baba yake alikuwa ni nani, wanafunzi wake walikuwa ni wangapi, na sasahivi yupo wapi, na kwamba atarudi tena.. n.k N.k. Ni watu wengi sana wanamjua Bwana Yesu wanaamini kuwa katoka kwa Mungu. Ndio maana leo hii ukimwuliza mtu kama anamjua Bwana Yesu, atakuambia Ndio, ukizidi kumwuliza kama anamwamini Bwana Yesu atakuambia tena Ndio!. Ni wachache sana wanaosema kuwa hawamjua kabisa wala hawamwamini. Hiyo ndio hali ya siku hizi za mwisho.

Lakini leo napenda nikuambie au nikukumbushe kuwa “kumjua tu Yesu  peke yake, hakukufanyi wewe kuupata uzima wa milele”. Tusome maandiko yafuatayo..

Yohana 3:2 “Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye.

3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu”.

Umeona?..Nikodemo pamoja na wenzake walimjua Yesu, na waliamini kuwa katoka kwa Mungu.. na hata wanakwenda mbele zake kumwambia Imani yao hiyo kwake. Lakini tunaona jibu la Bwana Yesu lilikuwa ni tofauti..

Kikawaida nilitegemea kuwa Bwana Yesu angemsifia Nikodemo na kumwambia “heri wewe Nikodemo kwa kuyajua hayo”.. lakini kinyume chake Bwana anamjibu Nikodemu na kumwambia…”Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu”.

Akiwa na maana kuwa haijalishi mtu amfahamu kiasi gani, au amwamini kiasi gani, kama mtu huyo hatazaliwa mara ya pili, imani yake hiyo ni bure..

Haijalishi Nikodemo na wenzake wanamjua Yesu kwa viwango gani, au wanamwamini kwa viwango gani, kama hawatakubali kuzaliwa mara ya pili, hawataurithi uzima wa milele.

Sasa swali linakuja katika vichwa vyetu, Nini maana ya kuzaliwa mara ya pili?

Swali hili hata Nikodeo alimwuliza Bwana, na Bwana Yesu alitoa maana yake, katika mistari inayofuata…

Yohana 3:4 “Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?

5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, MTU ASIPOZALIWA KWA MAJI NA KWA ROHO, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu”.

Umeona hapo?.. Kumbe tafsiri ya kuzaliwa mara ya pili, ni KUZALIWA KWA MAJI na KWA ROHO.

Sasa swali lingine, tunazaliwaje kwa Maji, na kwa Roho.

Tunazaliwa kwa Maji kwa njia ya Ubatizo, pale tunapobatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa Jina la Yesu Kristo, sawasawa na Matendo 2:38, hapo ndipo tunapozaliwa kwa Maji.  Watu wengi sana wanaupuuzia Ubatizo, na kusema si wa lazima!.. na kusema ukishaamini inatosha, si lazima ubatizwe.. Kumbuka hapo!, hata Nikodemo alimwamini Bwana Yesu, na alijua ndio kashakamilika, lakini Bwana Yesu anamwambia..Usipozaliwa kwa Maji, huna uzima.. Vivyo hivyo, na mtu yeyote ambaye hatabatizwa katika ubatizo sahihi, baada ya kuujua ukweli hana Uzima wa milele, hiyo ni kulingana na mananeo ya Bwana YESU.

Na tunazaliwaje pia kwa Roho?.

Tunazaliwa kwa Roho, kwa njia ya Ubatizo wa Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ndio muhuri wa Mungu katika maisha yetu..

Waefeso 4:30 “Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye  MLITIWA MUHURI HATA SIKU YA UKOMBOZI”.

Kwahiyo mtu yeyote atakayemkataa Roho Mtakatifu, baada ya kuamini, huyo sio wa Mungu, haijalishi anamjua Bwana Yesu kwa kiwango gani!.

Warumi 8:9 “..Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake”.

Hivyo mtu anapobatizwa sahihi na kupokea Roho Mtakatifu wa kweli, hapo anakuwa kazaliwa mara ya pili, anakuwa ni kiumbe kipya, lakini si kilichokomaa bali ni kichanga, kilichozaliwa katika dunia mpya kisichojua chochote!.

Kwahiyo baada ya kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu, sio mwisho wa safari, bali ndio mwanzo wa safari, kama vile mtoto aliyezaliwa anavyopitia hatua za kukua mpaka kufikia utu uzima na kukomaa, vivyo hivyo na mtu aliyezaliwa mara ya pili, ni lazima apitia hatua za kukaa chini, kuukulia wokovu, kwa bidii zote, ili awe imara.. Lakini akiacha kuukulia wokovu, basi mtu huyo atakufa kiroho, na kazi yake itakuwa ni bure.Lakini zipo faida nyingi sana za kuzaliwa mara ya pili..Ni nyingi sana, hata katika maisha ya hapa hapa duniani, lakini faida iliyo kubwa kuliko zote ni hiyo Bwana Yesu aliyoitaja kwamba UTAUINGIA UFALME WA MUNGU.

Je umezaliwa mara ya pili?

Kama bado unangoja nini baada ya kuyajua haya yote?.. Tafuta ubatizo sahihi…wa maji mengi na kwa Jina la Bwana Yesu, na Ujazo wa Roho Mtakatifu.

Bwana akubariki.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!

KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?

NUNUA MAJI YA UZIMA.

TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.

ILI TUONEKANE SAFI MBELE ZA MUNGU TUFANYE NINI?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments