Yeremia alikuwa na umri gani alipoitwa?

Yeremia alikuwa na umri gani alipoitwa?

JIBU: Maandiko hayaweki wazi ni katika umri gani Yeremia aliitwa isipokuwa watafiti wengi ya Biblia wanakadiria Yeremia aliitwa katika umri wa miaka 20, au chini kidogo ya hapo, pengine 17

Biblia inachosema tu..alipoitwa aliitikia kwa kusema mimi ni MTOTO…Ikiwa na maana kuwa alijiona  umri wake ulikuwa bado haujakidhi vigezo vya kumtumikia Mungu..

Yeremia 1:4 “Neno la Bwana lilinijia, kusema,  5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.  6 Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto.  7 Lakini Bwana akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru”.

Na hiyo pengine kwasababu aliona historia ya manabii wengi walioitwa walikuwa tayari ni watu wazima,

Pili Yeremia yeye alizaliwa katika familia ya kikuhani, na alijua umri wa kuhani kutumika Mungu ni kuanzia miaka 25 na kuendelea sawasawa na (Hesabu 8:24). Hivyo huwenda yeye hakuwa katika umri huo, ndio maana akawa na ujasiri wa kumwambia Mungu mimi bado ni mtoto.

Hivyo na sisi tunajifunza nini?

Kwa Bwana hakuna umri maalumu au  wakati maalumu wa kuitwa..Uonapo unavutwa umwamini Yesu, saa hiyo hiyo itikia wito huo, kama Yeremia, neema hiyo haitadumu milele. Ikiwa utapuuzia kwa kusema Aah, Muda bado ngoja kwanza nifikishe umri Fulani, ngoja kwanza nijenge nyumba, ngoja kwanza nipate kazi, ngoja kwanza niondoke kwa wazazi. Fahamu kuwa una dalili kubwa ya kuipoteza neema ya Mungu. Saa ya wokovu ni sasa, wakati uliokubalika ndio huu. Maneno ya Mungu yanapokuchoma, tambua huo ndio wakati wako. Itikia sauti hiyo, badilika, tumika, tii. Na Bwana atayashughulikia hayo yaliyosalia.

Bwana akubariki

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Wana wa Manabii walikuwa ni watu gani?

Raheli aliwalilia vipi watoto wake?

Matowashi ni wakina nani?

Historia ya wimbo wa tenzi – Ndio dhamana Yesu wangu

Je ni kweli miaka yetu ya kuishi ni 80 tu (kulingana na Zaburi 90:10).

Nabii Elisha alikuwa ana maana gani kulia na kusema”Gari la Israeli na wapanda farasi wake”?

Maswali na Majibu

HISTORIA YA ISRAELI.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Mboya Anangwe
Mboya Anangwe
1 year ago

Am always aprouud with you people…for real nilikuwa nimepotea..