Dia ni nini katika biblia? (Mithali 13:8)

Dia ni nini katika biblia? (Mithali 13:8)

Jibu: Tusome,

Mithali 13:8 “Dia ya nafsi ya mtu ni utajiri wake; Bali mtu maskini hasikii ogofyo lo lote”.

Dia ni Kiswahili kingine cha neno “Fidia”, Kwahiyo hapo biblia inaposema “Dia” ya nafsi ya mtu ni utajiri wake, na maskini hasikii ogofyo lolote, maana yake ni kwamba “Fidia ya mtu anapokutana na matatizo ni itatoka katika vitu alivyonavyo” ikiwa na maana kuwa mtu anapokutwa na tatizo labda kasababisha hasara Fulani au kafanya kosa Fulani katika jamii, lililomsababishia apigwe faini, au kakutana na watu na kaingiliwa na wahalifu katika nyumba yake, basi Mali alizo nazo zinaweza kuwa fidia kwaajili ya uhai wake, maana yake anaweza kuwapa wale watu sehemu ya mali zake na akaisalimisha roho yake.

Lakini mtu asiye na kitu kabisa (yaani Yule maskini kikweli kweli), huwa hawezi kupokea vitisho vyovyote, hakuna jambazi yeyote anayefikiria kwenda kuvunja nyumba ya maskini akiwa na mtutu ili amwibie mali zake.. Ikiwa na maana kuwa, maskini siku zote yupo huru!.. hafuatiliwi na mtu, wala hakuna mtu ana habari na maisha yake (hapokei ogofyo lolote).

Ni hekima gani tunaipata hapo? Au ni nini tunajifunza hapo?

Ili tuelewe ni nini tunajifunza hapo, hebu tuanzie kusoma kuanzia mstari wa 7

Mithali 13:7 “Kuna mtu mwenye kujitajirisha, lakini hana kitu; Kuna ajifanyaye kuwa maskini, lakini ana mali nyingi.

8 Dia ya nafsi ya mtu ni utajiri wake; Bali mtu maskini hasikii ogofyo lo lote”

Hii ni hekima ambayo inaweza kutusaidia kuwa salama..sio lazima tuwapo na mali, tujionyeshe kuwa na mali kwa watu!, ndio maana hapo biblia inasema “kuwa maskini, lakini ana mali nyingi.”.. Unapokuwa mtu wa kujionyesha mbele za watu mali ulizo nazo, unajiweka katika hatari ya kutoa DIA (Fidia) kwaajili ya uhai wako, kwasababu kila mtu atatamani hizo mali ulizo nazo, utavutia watu waovu na wasio waovu, utavutia majambazi, utavutia wenye mamlaka na watu  wapendao rushwa n.k

Hivyo hekima ni kujiweka katika maisha ya wastani, hata kama unazo mali nyingi, si lazima ujulikane wewe ni tajiri kuliko wote.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?

Azidishaye mali yake kwa riba, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.

Nini maana ya ampokeaye Nabii atapata thawabu ya Nabii? (Mathayo 10:41).

MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
1 year ago

Hongera sana mumenieleza vizuri, kuhusu neno Dia na mantiki yake, ahsante sana, kufwata maandishi yenu nimegundua ni faida kwangu