SWALI: Nini maana ya huu mstari;
Mithali 28:8 “Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.
JIBU: Huyo anayezungumziwa azidishiye mali zake kwa riba na faida ni mtu ajipatiaye mali kwa njia zisizo za haki, kuwadhulumu wanyonge.
Kwamfano katika biblia Mungu aliwaangiza wana wa Israeli, wasiwatoze riba maskini, pindi wawakopeshapo, na pia wasichukue faida kutoka kwa ndugu zao, isipokuwa kwa wageni tu.
Kutoka 22:25
“Ukimkopesha mtu aliye maskini, katika watu wangu walio pamoja nawe; usiwe kwake mfano wa mwenye kumdai; wala hutamwandikia faida”.
Soma pia, Walawi 25: 35-37, kumb 23
Hivyo kulikuwa na kundi kubwa la matajiri walioihasi hii sheria ya Mungu, wakawa wanawatoza riba na kujipatia faida isivyo haki, Matokeo yake Wakafanikiwa kujikusanyia mali nyingi kama mavumbi ya ardhini.
(Ayubu 27: 13-16 )
Lakini bado maandiko, yanatoa matokeo au hatma ya watu kama hawa. Mwisho wa siku Mungu anawapokonya na kuligawia kundi lingine la watu lenye kuwahurumia maskini.
Utajiuliza inawezekanikaje..biblia inasema mali ina mbawa, inaweza kupaa ghafla, au ikatumiwa kwa matumizi yasiyo ya muhimu ikapukutika yote, au wewe ukafa ukamwachia mwingine. Lakini kule inapoelekea, sio popote tu ilimradi, hapana, bali ni kwa mtu yule ambaye anawahurumia maskini.
Ndio Mungu anaweza kufanya hivyo..usipoitumia talanta yako vema. Anasema mnyanganyeni yule mwenye moja mkampe yule mwenye 10 (Mathayo 25:28),.Bwana anaweza kukunyang’anya ulichonacho.
Tukiwa watu wa kutenda haki na kuwahurumia maskini, kwa kuwapa vitu, basi tujue kuwa tayari kuna watu wameshaandaliwa kwa ajili ya kutuletea hazina hizo, na watu wenyewe ndio hao waovu, wanaojilimbikizia mabilioni ya pesa katika akaunti zao za benki kwa dhuluma, na hila, na biashara haramu, na sio kwa njia halali.
Hii ni kuonyesha kuwa watu wanaopenda kuwapa wengine vitu, wanayo hazina kubwa sana hapa dunia.
Bwana atusaidie kuzifahamu hekima hizi tupende kuwasaidia watu wanyonge.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Kiburi cha Uzima ni nini? (1Yohana 2:16)
Biblia ina maana gani inaposema akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko?
UBATILI.
Je Malaika Mikaeli ndiye Yesu mwenyewe?
SHINA LA UCHUNGU, LISICHIPUKE NDANI YETU.
DORKASI AITWAYE PAA.
Rudi nyumbani
Print this post