Kiburi cha Uzima ni nini? (1Yohana 2:16)

Kiburi cha Uzima ni nini? (1Yohana 2:16)

Tusome,

1 Yohana 2:16 “Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.

17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”.

Kiburi cha Uzima ni kiburi mtu anachokipata kutokana na vitu alivyonavyo vya kidunia (hususani mali).

Watu ambao hawajamjua Mungu, uzima wao wameuweka kwenye mali, wanapokuwa na mali nyingi ndipo wanapojiona waoni watu (wanao uzima), wakikosa wanajiona wao si kitu.. hivyo inapotokea wanapata mali hizo zinawapa kiburi na kuwafanya wabadilike tabia mbele za Mungu na wanadamu.

Lakini Bwana Yesu alisema maneno haya..

Luka 12:15 “Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.

16 Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana;
17 akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu.

18 Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.

19 Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.

20 Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?

21 Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu”.

Je na wewe uzima wako umeuweka wapi?
Je ni kwenye nyumba ulizozijenga? Je ni hizo ndizo zinazokupa kiburi hata kumdharau Mungu na kuwadharau wengine?, Je ni fedha ulizonazo?, au Magari?, au Vyeo? Inazokufanya uone injili ni habari zilizopitwa na wakati?..kama ndio basi unacho kiburi cha uzima pasipo kujijua, ambacho maandiko yanasema hakitokani na Mungu, kwasababu mali ni kama maua leo ipo kesho haipo, hivyo si ya kujitumainisha nayo, kamwe isituletee kiburi.

Je umejitajirisha wapi leo? Mbinguni au duniani, umejiwekea hazina yako wapi?, Mbinguni au duniani?

Bwana atusaidie tusiwe na kiburi cha uzima.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

FANYA BIDII ZOTE ULE MATUNDA YA UZIMA.

KARAMA YA MUNGU NI UZIMA WA MILELE.

JE WEWE NI LAZARO YUPI, WA KWANZA AU WA PILI?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments