Wanikolai ni watu gani? Katika biblia?

Wanikolai ni watu gani? Katika biblia?

“Nikolai” ni neno la kigiriki lenye maana ya “Kuteka madhabahu”.

Katika kanisa la kwanza kulikuwa na kundi dogo la watu lililonyanyuka, ambalo lilikuwa linateka madhabahu.

Na kuteka madhabahu kunakozungumziwa sio kuteka nyara vitu vya madhabahuni au watu wanaosimama madhabahuni, hapana!.

Bali kuteka kunakozungumziwa hapo, ni kusimamisha mfumo ambao unaondoa uongozi wa Roho Mtakatifu ndani ya kanisa, na kusimamisha uongozi wa wanadamu.

Kikawaida kanisa linapaswa liongozwekwa karama za Roho Mtakatifu, yaani Uinjilisti, uchungaji, unabii, aualimu, karama za lugha, miujiza, imani n.k (1Wakorintho 12).

Hizo ndizo zinazoliongoza kanisa, na ndizo zinazojenga mwili wa Kristo,lakini enzi za kanisa la kwanza liliinuka kundi la watu wasio na Roho, na kutaka kuliongoza kanisa kibinadamu.

Maana yake badala Roho Mtakatifu anene, apange, afundishe, aamue, na afanye jambo kupitia karama alizoziweka ndani ya watu wake..kinyume chake wakainuka watu wakawa wao ndio  wanapanga, wananena, wanafundisha na wanaamua kupitia falsafa zao, hekima zao, vyeo vyao, heshima zao katika jamii, umaarufu wao, elimu zao, ujuzi wao, mwonekano wao, na si tena kupitia karama za Roho.

Ratiba za masomo ya kufundisha zikawa zinapangwa na wanadamu, inaweza kutolewa kalenda hata ya mwaka mzima, masomo ya kufundisha tayari yameshaandaliwa.

Hivyo ubinadamu ukawa umeteka madhabahu ya Bwana badala ya Roho Mtakatifu. Huo ndio “Unikolai”.

Na katika kanisa la kwanza maandiko yanasema unikolai ulianza kama Matendo tu, Yaani watu hao ambao yalikuwa ni mapando ya adui shetani, walikuwa wanafanya hayo lakini sio kuwafundisha watu.

Ufunuo 2:6 “Lakini unalo neno hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo na mimi nayachukia”.

Lakinibaadaye unikolai ulikuja kubadilika na kuwa “Mafundisho”, yaani watu wakawa sio tu wanatenda unikolai, bali wakawa  wanafundisha wengine kuutenda unikolai, (yaani kuunyanyua uongozi wa kibinadamu na kuushusha chini uongozi wa Roho Mtakatifu).

Ufunuo  2:15 “Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile.

16 Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu”.

Matendo na mafundisho ya Wanikolai katika nyakati hizi za mwisho ndio yameshika hatamu.

Leo hii hakuna tena uongozo wa Roho mtakatifu ndani ya kanisa, ni Liturjia, na malokeo ndio yanayoongoza… kiasi kwamba hata ikitokea mtu kafunuliwa jambo jipya na Roho Mtakatifu la kwenda kufundisha, hawezi kupata nafasi kwasababu tayari kalenda ya nini cha kufundisha mwaka mzima imeshawekwa, na lazima aifuate hiyo!.

Leo hii ili uaminike kuwa wewe mchungaji au mtumishi wa Mungu ni lazima uwe umepitia chuo cha biblia na theolojia, ukisema unao wito wa Roho Mtakatifu bila kupitia mambo hayo huwezi kueleweka. (Huo ni unikolai), ambao Bwana Yesu kasema anauchukia!!!.

Unikolai hautaki kabisa Uongozo wa Roho Mtakatifu, unampinga Roho Mtakatifu siku zote.

Na shetani anajua kanisa linaloongozwa na Roho Mtakatifu ni hatari sana katika ufalme wake. Na yeye hataki watu waende mbinguni.

 Hivyo atafanya juu chini kumzimisha Roho ndani ya kanisa, lakini ashukuriwe Mungu, katikati ya giza nene ipo Nuru mahali.

Bwana anao watu wake mahali fulani katika kila Taifa, ambao hawajamzimisha Roho.

Bwana atusaidie na sisi tuwe miongoni mwa hao ambao hawajamzimisha Roho.

1 Wathesalonike 5:19 “Msimzimishe Roho”

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?

Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?

AHADI YA ROHO ILIYOSALIA SASA KWA KIPINDI CHETU.

UFUNUO: Mlango wa 3 part 3

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
1 year ago

Asante

Moses njagi
Moses njagi
1 year ago

All is okay

Anonymous
Anonymous
1 year ago

Hello mubarikiwe sana