HAKUVAA NGUO SIKU NYINGI.

HAKUVAA NGUO SIKU NYINGI.

Luka 8:26 “Wakafika pwani ya nchi ya Wagerasi, inayoelekea Galilaya.

27 Naye aliposhuka pwani, alikutana na mtu mmoja wa mji ule, mwenye pepo, HAKUVAA NGUO SIKU NYINGI, wala hakukaa nyumbani, ila makaburini.

28 Alipomwona Yesu alipiga kelele, akaanguka mbele yake, akasema kwa sauti kuu, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi usinitese”.

Tabia mojawapo ya mtu mwenye pepo ni KUTOKUVAA NGUO KABISA, au KUVAA NUSU UCHI!.

Ukiona unapenda kuviweka wazi viungo vya mwili wako, na hata hujisikii vibaya…fahamu kuwa hiyo ni dalili ya kuwa na Pepo ndani yako!..Na tabia nyingine ya mtu mwenye pepo ni kuwa “Anakuwa Mkali sana”..pindi anapotaka kusaidiwa..

Mathayo 8:28 “Naye alipofika ng’ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, WAKALI MNO, hata mtu asiweze kuipitia njia ile”.

Ukiona unachukia sana, unapoambiwa kwamba mavazi unayovaa si ya kujisitiri, basi hiyo ni dalili ya kwamba unalo pepo ndani yako!, ambalo linapaswa litoke.

Ukiona unakasirika au unakuwa mkali unapoambiwa kuwa vimini unavyovivaa, au suruali unazozivaa(mwanamke) ni dhambi, basi tafuta msaada wa haraka ili kusudi hayo mapepo yaweze kukutoka, kwasababu katika hali ya kawaida, mtu mwenye akili timamu hawezi kukaa nusu tupu na akatembea hivyo barabarani na akajiona yupo sawa…

Ishara ya kwanza ya Yule mtu kutokwa na mapepo ni yeye kuvaa nguo, na kuwa akili zake timamu.

Marko 5:15 “Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, AMEVAA NGUO, ana akili zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa”.

Je wewe mwanamke/mwanaume hapo kazini ulipoketi,  au hapo shuleni ulipo sasa, au hapo kanisani unaposhiriki sasa je umevaa Nguo?..umejisitiri?, je kifua chako kimefunikwa au kipo wazi?..je mgongo wako umefunikwa au upo wazi?.. Je mapaja yako yamefunikwa au yapo wazi?, je tumbo lako limefunikwa au lipo wazi?.. Kama mwili wako haujasitirika! Basi ni ishara kuwa unayo mapepo na huna akili timamu (mapepo yameondoa ufahamu wako).

Lakini kama sehemu za juu za mikono yako zipo wazi, au kifua chako au mapaja yako, au umevaa nguo lakini inachora maungo yako, kiasi kwamba hauna tofauti na mtu aliye uchi kabisa, basi fahamu kuwa UNAYO MAPEPO NA PIA HUNA AKILI TIMAMU, na zaidi sana ukiona unakasirika unapoyasikia haya maneno, basi ndio uthibitisho wa mwisho kuwa Mapepo yapo ndani yako!.. na hivyo unahitaji msaada.

Na habari njema ni kwamba, msaada huo unaweza kuanza kuupata hapo hapo ulipo.

Unachopaswa kufanya sasahivi ni kudhamiria KUTAKA MSAADA WA KUTOKANA NA HAYO MAPEPO!... Na unadhamiria kwa Kumpokea Bwana Yesu maishani mwako..(Usiseme tayari nilikuwa nimeshampokea!)…Ulikuwa bado hujampokea ndio maana ulikuwa unaona upo sawa kukaa nusu uchi!!.. Bwana Yesu angekuwa ndani yako, usingekuwa hivyo ulivyo sasa!!… Wewe sasahivi ndani yako yapo mapepo ambayo yanakufanya UKAE UCHI!!.

Kwahiyo unapaswa pale ulipo ujitenge wewe binafsi, uombe toba!, kwa kudhamiria kuacha njia mbaya…kutubu dhambi maana yake ni pamoja na kuacha vyote ulivyokuwa unavifanya, maana yake leo leo nenda kachome vimini vile, na suruali zile unazozivaa, na anza kuvaa nguo kamili, kwa kufanya hivyo utakuwa umeonyesha kwa vitendo kwamba hutaki tena mapepo ndani yako, na akili itakurudia, na utaona kweli ulikuwa vifungoni.

Baada ya kufanya hivyo nenda katafute ubatizo sahihi, ubatizwe upya, na ubatizo wa kibiblia ni ule wa jina la Yesu na wa maji mengi, baada ya hapo Roho Mtakatifu atashuka juu yako na kukusafisha kabisa..

Maran atha!

Mada Nyinginezo:

SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.

NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.

Watu wenye ulemavu wa akili, wataenda mbinguni?

Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?

ONDOKA YESU, TUACHIE MAPEPO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments