Akida ni nani kibiblia, na kazi yake ni ipi? (Mathayo 8:5)

Akida ni nani kibiblia, na kazi yake ni ipi? (Mathayo 8:5)

Akida ni mkuu wa majeshi ya zamani, hususani majeshi ya kirumi. Akida mmoja alikuwa anaongoza kikosi cha askari 100,. Maakida wengi walikuwa wanachaguliwa na watalawa wao wakuu moja kwa moja toka Rumi,wengine katika mabaraza, wengine kutoka kwa maliwali, na wengine moja kwa moja kwa kupandishwa vyeo, baada ya kutumika kwa muda mrefu (miaka 15-20), katika shughuli za kijeshi.

Kazi yao kubwa ilikuwa ni kusimama mstari wa mbele katika vita kuliongoza kundi lote jeshini, pia kutekeleza mauaji ya wahalifu, au washitakiwa, mfano wa hawa ni Yule akida aliye simamia mateso na mauji ya Bwana Yesu pale Kalvari

Marko 15:39 “Basi yule akida, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu”.

Pia walikuwa wanafanya kazi ya kutoa mafunzo ya kijeshi, kugawa majukumu, kusimamia ujenzi wa ngome na kuta za ulinzi za taifa. Walifanya pia kazi ya kuwalinda wafungwa na kuwahakikishia ulinzi wao pindi wasafirishwapo, Mfano wa Hawa, soma .(Matendo 23:23, 24:23, )

Pamoja na hilo, maakida wengine walikuwa ni watu wakatili, na wapenda rushwa,

Lakini ni jambo  gani Mungu anataka tujifunze nyuma ya watu hawa?

Ijapokuwa kazi hii, si kazi iliyoonekana kumrudishia Mungu utukufu, Lakini bado tunaona wapo maakida, kadha wa kadha katika biblia, waliompendeza Mungu katika utumishi wao, zaidi hata ya wayahudi wengi, waliokuwa wanajiona washika sheria na torati.

Kwamfano utaona Bwana Yesu alipokuwa katika ziara zake za kuhubiri na kufungua watu, alikutana na akida mmoja, ambaye aliustaajibisha sana moyo wake kwa imani aliyokuwa nayo, mpaka Bwana akasema hata katika Israeli,hakuna aliyekuwa na imani kubwa kama yake.

Mathayo 8:5 “Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia,

6 akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana.

7 Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye.

8 Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.

10 Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli.

11 Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;”

Utaona pia, kulikuwa na akida mwingine, aliyeitwa Kornelio, huyo alikuwa anatoa sadaka nyingi sana, na kuwasaidia watu, mpaka siku moja malaika wa Bwana anamtokea na kumpa maagizo ya kufanya ili aupokee wokovu kamili.

Matendo 10:1 “Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia,

2 mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima”.

Umeona? Ni nini Mungu anataka tujue?

Ni kwamba Mungu hatazami sana mahali unapotumika, lakini anatazama uaminifu wako, moyo wako, utakatifu wako, bidii yako kwake. Unaweza ukawa unafanya kazi serikalini, lakini ukamtumikia Mungu vema, kwa kukataa rushwa, na kutenda haki, na Mungu akapendezwa nawe..Mfano wa Danieli, Maadamu, upo mahali ambapo hapakinzani na sheria ya Mungu na taifa, usijisikie vibaya kutumika unachopaswa kufanya ni kumtumikia tu Mungu kwa uaminifu wote, kuangaza nuru yako ya wokovu kwa wale watu, na kumpenda yeye na kukataa njia zote mbaya zinazokinzana na Neno lake.

Kwa kufanya hivyo Basi Mungu atakutumia kutimiza kusudi lake, alilolikusudia juu yako, na watu wake, mfano wa Kornelio na Yule akida ambayo alidhubutu hata kuwajengea wayahudi sinagogi.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

ORODHA YA WAFALME WA ISRAELI.

KIASI NI NINI KATIKA UKRISTO?

ONDOKA YESU, TUACHIE MAPEPO.

Mshipi wa dhahabu matitini ni nini?

Neno “Mashehe” tunaliona likitajwa katika biblia(Agano la kale); Hawa mashehe ni wakina nani?

Katika (Mathayo 25:8 na Marko 16:8) Wale wanawake walitangaza kufufuka kwa Bwana au walikaa kimya?

Uchaga ni nini? (Luka 12:24)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments