Liwali ni nani?

Liwali ni nani?

Liwali ni mkuu wa mji au jimbo Fulani. (Gavana).

Kwamfano katika biblia tunaona, Pontio Pilato anatajwa kama Liwali wa Uyahudi sehemu ya kusini mwa Israeli,. Hivyo eneo lote la uyahudi yeye ndiye alikuwa kama mkuu wa majimbo hayo.

Mwingine ni Yusufu, biblia inasema, Farao alimweka kama Liwali wa nchi yote ya Misri.

Mwanzo 42:6 “Naye Yusufu alikuwa ni liwali juu ya nchi, ndiye aliyewauzia watu wote wa nchi. Nao ndugu zake Yusufu wakaja, wakainama kifudifudi mbele yake”.

Hivyo kazi yao haswaa ilikuwa ni sawa na ya wakuu wa mikoa wa sasa, au majimbo, ambapo kimsingi wanakuwa na mamlaka ya kuongoza shughuli zote za jimbo hilo kwa amri yao, wala hakuna chochote kinachoweza kufanyika bila idhini yao.

Hivi ni baadhi ya vifungu vya Zaida ambavyo utaweza kukutana na hilo neno;

Mathayo 27:1 “Na ilipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumwua;

2 wakamfunga, wakamchukua, wakampeleka kwa Pilato aliyekuwa liwali.

Mathayo 28:14 “Na neno hili likisikilikana kwa liwali, sisi tutasema naye, nanyi tutawaondolea wasiwasi.

15 Basi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo”.

Matendo 13:6 “Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu;

7 mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu”.

Matendo 18:12, 23:24, 26:30

Ni nini twaweza zingatia  kuhusu hawa maliwali?

Bwana Yesu alisema, katika utumishi wetu, utafika wakati, tutaitishwa mbele ya mabaraza ya wafalme, na maliwali, kushitakiwa.Hivyo tukijikuta  katika mazingira kama hayo hatupaswi kuogopa, kwasababu Kristo ameahidi kuwa atakuwa na sisi katika mapito yetu yote.

Mathayo 10:18 “nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa”.

19 Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema.

20 Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu”.

Bwana akubariki.

Je! Umeshamkabidhi Kristo Maisha yako?. Kama jibu ni hapana, na upo tayari kuokoka leo. Basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya toba, >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Au tutafute kwa namba zetu hapo chini, kwa msaada huo.

+255693036618/+255789001312

Mada Nyinginezo:

Akida ni nani kibiblia, na kazi yake ni ipi? (Mathayo 8:5)

Je mwanamke Fibi, alikuwa ni askofu wa makanisa, kama mitume?

Mjoli ni nini/ ni nani katika biblia?

Mharabu ni nani katika biblia?

Bawabu ni nani/nini?

Mapooza ni nini? Na je! Twawezaje kuepukana nayo?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments