Kama kuua ni dhambi kwanini Mungu aruhusu mauaji katika Kumbukumbu 13:6-10?

Kama kuua ni dhambi kwanini Mungu aruhusu mauaji katika Kumbukumbu 13:6-10?

Bwana alisema “Usiue” (Kutoka 20:6) lakini tunaona anawapa wana wa Israeli maagizo ya kuua wale wote wanaoabudu miungu? Je Hii inakaaje? (Kumbukumbu 13:6).

Jibu: Tusome,

Kumbukumbu 13:6 “Atakapokushawishi kwa siri ndugu yako, mwana wa mamaako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa kifuani mwako, au rafiki yako aliye kama moyo wako, akikuambia, Twende tukaabudu miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako; 7 katika miungu ya mataifa yaliyo kando-kando yenu karibu nawe au mbali nawe, tokea ncha moja ya dunia hata ncha ya pili ya dunia;8 usimkubalie wala usimsikize; wala jicho lako lisimwonee huruma, wala usimwache, wala usimfiche;9 MWUE KWELI; mkono wako na uwe wa kwanza juu yake katika kumwua, na baadaye mikono ya watu wote.10 NAWE MTUPIE MAWE HATA AFE; kwa kuwa alitaka kukupotoa na Bwana, Mungu wako aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.11 Na Israeli wote watasikia na kuogopa, wasifanye tena uovu mfano wa huo katikati yako”

Ni kweli Mungu alikataza “Kuua” lakini pia kuna mahali pengine aliruhusu “kuua”, sasa ni rahisi kuhisi kuwa biblia inajichanganya, lakini kiuhalisia haijichaganyi.

Katika biblia zilikuwepo sheria za mtu binafsi lakini pia zilikuwepo sheria za Nchi/Taifa. Ikumbukwe kuwa Israeli lilikuwa ni Taifa la kidini, hivyo baadhi ya Amri na sheria zilikuwa ni za kitaifa. Kwahiyo mtu akiivunja sheria Fulani iliyoandikwa kwenye torati basi alikuwa amevunja sheria ya kitaifa.

Ili tuelewe vizuri tuchukue mfano wa mataifa ya sasa, katika mataifa mengi, (karibia yote) kuna sheria ya “kutoua” yaani raia haruhusiwi kumuua mwenzake kwa kosa lolote lile!!, lakini katika Taifa hilo hilo tunaona kuna sheria ya “kunyongwa” endapo mtu akikutwa na hatia iliyo kubwa sana..

Sasa Yule askari aliyetumwa kumweka kitanzi Yule mtuhumiwa, tayari kashafanya tendo la mauaji, lakini kwa kumnyonga Yule mhalifu, bado anakuwa hajavunja sheria ya “kuua”.. Kwasababu yeye kapewa amri ya kuua na mamlaka, lakini haja ua kwa matakwa yake yeye. Lakini kama ingekuwa kajichukulia sheria mkononi ya kuua basi angehesabika ni muuaji, na angekuwa amevunja sheria ya nchi. Na pia Nchi kuweka sheria ya Kuwaua wale waalifu sugu, haijamaanisha kuwa imeruhusu sheria ya watu kuuana huko uraiani.

Vivyo hivyo katika Israeli, Mungu alikataza mtu kujichukulia sheria mkononi za kuua, lakini pia aliruhusu mauaji kwa watu ambao watathibitika kisheria (yaani kitaifa) kuwa wamestahili kifo!.  Na mamlaka hayo aliwapa watu wote, tofauti na sasa ambapo wanapewa tu wale askari walioteuliwa kwa kazi hiyo.

Kwahiyo biblia haijichanganyi, lakini pia tunachoweza kujifunza ni kuwa Lile baya mtu analolifanya litamrudia hata kwa njia nyingine, mtu aliye muuaji naye pia atauawa, mtu anayefanya ubaya ule ubaya utampata na yeye siku za baadae.

Mathayo 26:51  “Na tazama, mmoja wao waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.

52  Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga”.

Soma pia Ufunuo 13:10.

Kwahiyo tujihadhari na dhambi tuwafanyiazo watu au tuzifanyazo mbele za Mungu, kwasababu yale tunayoyafanya tutapata malipo yake hapa hapa, kama ni mema au kama ni mabaya.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Mada Nyinginezo:

NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?

MJUMBE WA AGANO.

Je! sheria ilikuwaje dhaifu kwasababu ya mwili? (Warumi 8:3)

Je! Watu ambao hawajawahi kusikia injili kabisa siku ya mwisho watahukumiwa?

IMANI NI KUWA NA UHAKIKA WA MAMBO YATARAJIWAYO.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments