SWALI: Katika Mithali 30:24, tunaona wanatajwa wanyama wanne, wenye akili sana, lakini naomba kufahamu juu ya Yule wanne ambaye ni mjusi, Anaposema “Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme” Maana yake ni nini?
JIBU: Tusome,
Mithali 30:24 “Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana. 25 Chungu ni watu wasio na nguvu; Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari. 26 Wibari ni watu dhaifu; Lakini hujifanyia nyumba katika miamba. 27 Nzige hawana mfalme; Lakini huenda wote pamoja vikosi vikosi. 28 Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme”
Mjusi ni kiumbe ambaye ameumbiwa wepesi wa kupanda na kupita karibia sehemu zote zenye upenyo hata ule mdogo sana, uwezo wa mikono yake unamfanya aweze kusimama katika pembe yoyote ile ya ukuta, iwe ni ukuta wa juu, au wa pembeni, au wa chini, kwake vyote ni sawasawa, tofauti na wanyama wengine, ambapo pengine hutegemea kucha zao, ambazo hizo zinawasidia kupanda baadhi ya maeneo tu kama miti.
Na ndio maana utawakuta katika kila nyumba, hawazuiliki, hadi katika majumba ya wafalme biblia inasema hivyo utawakuta, mahali ambapo pana ulinzi, pana uangalizi, lakini wao wanaingia huko bila shida yoyote na kufanya makazi.
Ni kutufundisha nini katika hekima yake?
Ni kwamba, na sisi tunapokuwa ndani ya Kristo tunapewa mikono kama ya mjusi katika roho. Uwezo wa hali ya juu kupanda kila kuta ngumu, Hatuzuiliki kwa kitu chochote, popote tutakapotaka kupafikia tutapafikia, hata katika malango mazito ya ibilisi tutayamiliki.
Mwanzo 22:17 “katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; NA UZAO WAKO UTAMILIKI MLANGO WA ADUI ZAO; 18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu”
Je! Unataka uupokee uwezo huo? Kanuni ni moja tu, nayo ni kumpa Kristo maisha yako, jikane nafsi yako, simama kikamilifu na Bwana, kisha utaona jinsi Mungu anavyokupigania kuangusha kuta na kumshinda ibilisi kiwepesi, ziwe za kimaisha au za kiroho. Kwako hakuna kikwazo kitakachokuwa kigumu kukishinda.
Bwana akubariki.
Je! Utapenda kufahamu hekima iliyo nyuma ya wale watatu waliosalia?
Fungua link hizi>>>
Wibara > Wibari ni nani?(Mithali 30:26)
Nzige >TUWATAFAKARI NZIGE WA JANGWANI.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP
Mada Nyinginezo:
Nzige, Parare, madumadu na tunutu ni wadudu gani? (Yoeli 2:25)?
Biblia inapotumia neno “Bila kazi ya mikono”, ina maana gani?
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 5
Mikono iliyotakata ni mikono ya namna gani? (1Timotheo 2:8)
Ayala, Paa na Kulungu ni wanyama gani?
Je! Lewiathani ni nani?
Lumbwi ni nini katika biblia?
tofauti iliyopo kati ya Imani na ujasiri, ni ipi?
Biblia inasemaje kuhusu Kazi?
Rudi nyumbani
Print this post