Ni kwa namna gani Kristo analitakasa kanisa kwa Maji katika Neno? (Waefeso 5:26)

Ni kwa namna gani Kristo analitakasa kanisa kwa Maji katika Neno? (Waefeso 5:26)

Jibu: Turejee..

Waefeso 5:25  “……kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;

26  ili makusudi alitakase na KULISAFISHA KWA MAJI KATIKA NENO;

27  apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa”..

Siri ya kanisa kutakaswa kwa “Maji” inaanzia pale Msalabani, wakati Yule Askari anamchoma Bwana mkuki ubavuni, biblia inaonyesha kuwa palitoka “Maji na Damu”. Ikifunua kuwa Maji ni lazima yahusike katika hatua za utakaso wetu, ndipo damu ya Yesu iweze kututakasa kabisa. Utauliza tunazidi kulithibitisha vipi hilo? Tusome Matendo 2:37-38

Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38  Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”

Umeona hapo?.. Anasema tubuni mkabatizwe, mpate ondoleo la dhambi.. kwahiyo kumbe ubatizo unahusika sana katika kusafika utu wa ndani.. maana yake utakaso wa  Damu, unategemea ubatizo wa Maji, ili  Roho Mtakatifu aweze kukaa ndani ya mtu.  

Vitu hivi vitatu vinaenda pamoja (DAMU, MAJI na ROHO Mtakatifu). Huwezi kukichukua kimoja na kukiacha kingine!… Wala kusema kimoja kina umuhimu kuliko kingine… Vyote hivi vitatu vina umuhimu na maandiko yanasema vinapatana katika UMOJA!

1Yohana 5:9  “Kisha wako watatu washuhudiao duniani], ROHO, NA MAJI, NA DAMU; na watatu hawa hupatana kwa habari moja”.

Hiyo ndio sababu pia kwanini tunapaswa tubatizwe!.. Wengi leo wanaupuuzia ubatizo wa maji wanasema hauna umuhimu sana, ubatizo wa Roho Mtakatifu ndio wa muhimu.. Pasipo kujua kuwa Roho, na Maji na Damu vinapatana katika Umoja, ndio maana Bwana Yesu alimwambia Nikodemo kuwa kama hatazaliwa kwa MAJI (maana yake kwa ubatizo wa maji) na kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu, hatauona ufalme wa mbinguni, na huko ndiko kuzaliwa mara ya pili.

Maana ya kuzaliwa mara ya pili ni kubatizwa katika maji na katika Roho Mtakatifu.

Yohana 3:4  “Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?

5  Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa MAJI NA KWA ROHO, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.

6  Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.

7  Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili”.

Na ubatizo ulio sahihi ni ule wa maji Tele (Yohana 3:23) na kwa jina la Bwana Yesu (Matendo 2:38, Matendo 8:16, Matendo 10:48 na Matendo 19:5)

Bwana akubariki.

Ikiwa bado hujapata ubatizo sahihi, basi unaweza kuwasiliana nasi, tutakusaidia juu ya hilo, kwa Neema ya Bwana.

Shalom

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Mada Nyinginezo:

MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.

TOFAUTI YA UBATIZO WA YOHANA NA UBATIZO WA BWANA YESU

NUNUA MAJI YA UZIMA.

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

MAAGIZO YA BWANA YESU NI BORA KULIKO MAAGIZO YA DAKTARI

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Tito bruno
Tito bruno
1 year ago

Ninazidi kubarikiwa na kufunguka kwa mafundisho yenu asante sana