BWANA ni mtu wa vita,  BWANA ndilo jina lake.(Kutoka 15:3)

BWANA ni mtu wa vita,  BWANA ndilo jina lake.(Kutoka 15:3)

SWALI: Naomba kufahamu maana ya huu mstari..Kwanini biblia imtaje Mungu kama mtu, angali maandiko yanasema yeye sio mtu.

Kutoka 15:3

[3]BWANA ni mtu wa vita,  BWANA ndilo jina lake.


JIBU: Neno hilo halimaanishi kuwa Mungu ni mtu, Bali biblia hutumia mifano halisi ya kibinadamu kuwasilisha picha Fulani Rohoni..

Kwamfano ukisoma andiko lingine linalopatikana katika Mithali 30:26, utaona mnyama anayeitwa Wibari anatajwa kama mtu..

Mithali 30:26

[26]Wibari ni watu dhaifu;  Lakini hujifanyia nyumba katika miamba.

Tunafahamu kabisa wanyama hawa wibari(Pimbi) sio watu, isipokuwa kwa wingi wa akili zao, mwandishi anawafananisha na watu, Ni kwasababu gani? Ni Kwasababu ijapokuwa ni waoga, wadhaifu, wanawindwa na kila mnyama mkali..lakini hawajengi nyumba zao katika sehemu dhaifu kama kwenye viota, au kwenye mashimo, au vichaka, ambapo ni rahisi kuvamiwa au kuharibiwa na majanga, Bali wanaweka makazi Yao katika miamba mikubwa iliyojificha sana  Mahali ambapo ni ngumu adui kuwashambilia.. wanafananishwa na watu waliojenga maisha yao juu ya MWAMBA, pekee yaani Yesu Kristo

Mathayo 7:24  “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; 25  mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba”

Hivyo tukirudi katika andiko hilo, anaposema “BWANA ni mtu wa vita”. Anajaribu kumfananisha Bwana na shujaa wa kivita, jemedari mwenye uzoefu mkubwa sana katika vita vikali, mfano wa Sauli, au Daudi, ambao walikuwa wanasimama mstari wa mbele katika vita, ili sisi tupate picha jinsi gani Mungu wetu alivyo mkuu sana, pale anapoitwa Bwana wa Majeshi, tumwelewe uweza wake wa kutupigania na kutusaidia kuangusha ngome za ibilisi jinsi ulivyomkubwa haijalishi zimekita mizizi kiasi gani.

Zaburi 24:8 “Ni nani Mfalme wa utukufu? Bwana mwenye nguvu, hodari, Bwana hodari wa vita”

Hivyo mstari huo hakumaanisha kuwa yeye ni mtu.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP

Mada Nyinginezo:

Ufunuo 12 inaelezea vita vya wakati upi?

Kati ya Unyakuo,dhiki kuu, utawala wa miaka 1000 kipi kinaanza

NIMEAZIMIA KUWAKUSANYA MATAIFA. NIPATE KUWAMWAGIA GHADHABU YANGU

Nini maana ya ombeni kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi wala siku ya sabato?

VITA DHIDI YA MAADUI

Nini maana ya mhubiri 9:11? si wenye mbio washindao katika michezo?

NA WATU WOTE WALIKUWA WAKIAMKA MAPEMA, WAENDE HEKALUNI.

Shetani anaishi wapi, Je! Amefungwa au yupo kuzimu?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments