Kwanini jiwe la kusagia Mungu alikataza lisiwekwe rehani? (Kumbukumbu 24:6).

by Admin | 30 March 2023 08:46 pm03

Jibu: Turejee,

Kumbukumbu 24:6 “Mtu awaye yote asitwae jiwe la kusagia, la juu wala la chini, kuwa rehani; kwani hivi ni kutwaa maisha ya mtu kuwa rehani”.

Jiwe la kusagia lilikuwa ni jiwe lililotumika katika kusagia nafaka enzi za zamani, na hata sasa katika baadhi ya jamii.. Lilikuwa ni jiwe kubwa ambapo nafaka kama ngano inawekwa juu yake, na kisha jiwe lingine dogo linawezwa juu yake na kusaga nafaka hiyo.

Lilikuwa pia ni jiwe ambalo linapatikana karibia katika kila nyumba.. ni kama vile leo, jiko ilivyo zana ya msingi karibia katika kila nyumba, hata yule maskini kabisa hawezi kukosa jiko, vile vile na hili jiwe lilikuwa ni zana ya msingi sana.

Sasa Mungu alikatakaza Jiwe hilo (liwe la juu au la chini) lisiwekwe rehani kwa vyovyote vile, Maana yake kama mtu kamkopesha maskini, hapaswi kukubali rehani iwe jiwe la kusagia, kwasababu endapo Yule maskini kashindwa kulipa mkopo ule, basi jiwe lile jiwe la kusagia litachukuliwa na kwenda kuuzwa ili deni lile lilipwe, na hivyo Yule maskini atabaki hana hilo jiwe, na hivyo atashindwa kusaga nafaka zake kwaajili ya chakula chake cha kila siku, hata nafaka zile chache ambazo atazipata katika shamba lake, atashindwa kuzisaga kama riziki, na hivyo anaweza kufa kwa njaa.

Lakini rehani ya vitu vingine kama vyombo, au mashaba iliruhusiwa, kwasababu mtu angeweza kuishi bila hivyo vitu,  lakini si bila jiwe hilo la kusagia.

Jambo hilo linatufunza nini?

Tunajifunza kuwa na huruma kwa watu wa hali ya chini, Ni vizuri kutoa mkopo lakini si kila mkopo ni lazima tupate rehani, mikopo mingine tunaweza kuitoa tu bila kumweka mtu rehani, (hususani kwa wale watu ambao ni hali ya chini sana kiuchumi), hiyo itaonyesha upendo wetu na wema kwa watu na hata kuwafanya wavutiwe na imani yetu na kumfuata Mungu wetu.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

JIWE LILILO HAI.

JIWE LA KUSAGIA

Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika..

Biblia inapotumia neno “Bila kazi ya mikono”, ina maana gani?

LIONDOE JIWE.

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2023/03/30/kwanini-jiwe-la-kusagia-mungu-alikataza-lisiwekwe-rehani-kumbukumbu-246/