SWALI: Naomba kufahamu ni hekima gani tunaipata nyuma ya vifungu hivi, vinavyosema “Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza, Naam, wanne walio na mwendo mzuri”.
JIBU: Mithali 30:29 “Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza, Naam, wanne walio na mwendo mzuri. 30 Simba aliye hodari kupita wanyama wote; Wala hajiepushi na aliye yote; 31 Jimbi aendaye tambo; na beberu; Na mfalme ambaye haasiki”.
Swali la kujiuliza ni kwanini wameonekana wana mwendo mzuri na wa kupendeza, jibu ni kwasababu ya tabia yao ya ujasiri na kuamini kuwa wao ni wamiliki.
kwamfano Simba ni mfalme wa pori, kila kitu kilicho mbele yake anakiona ni chakula, hivyo hana uoga na lolote. Anamiliki wanyama wote , hata wale wanaoonekana ni wakubwa na wenye nguvu kuliko yeye. Wote wanamkimbia.
Anamtaja pia jimbi/jogoo, ambaye na yeye ni mfalme wa shamba, usemi wa “kutanua mbawa” umeanzia kwake. Yeye anaamini anaweza kumiliki mitetea yote na kundi lote la kuku. Watafiti wanasema kule kuwika kwa jogoo, sio bila sababu tu. Hapana, bali ni anatuma ujumbe kwa majogoo wengine wasimsogelee kwenye miliki yake na kutafiti kama yupo ambaye anamkaribia, ajiandae kwa mapambano. Tofauti na ndege wengine walio madume, hawana tabia za kujimilikisha kama Jogoo, au kupigana ili kumiliki shamba.
Anamtaja pia Beberu,(Mfalme wa zizi) katika kundi, beberu utamtambua tu kwa tabia zake, hujiaminisha sana, muda wote hatulii, analimiliki kundi lote kana kwamba yeye ndio mchungaji-msaidizi (Zekaria 10:3). Katika Historia unabii wa Aleksanda mkuu aliyetawala Ugiriki ya kale, ambaye aliteka ngome nyingi sana, kila alipopatamani alikwenda na akashinda alifananishwa na beberu katika maandiko Kutokana na Tabia zake hizo (Danieli 8:5). Hata sasa mataifa yanayotaka kumiliki mataifa mengine kwasababu ya nguvu zao za kijeshi, au kiuchumi au kisiasi, hujulikana kama mataifa ya kibeberu.
hiyo ni kufuatana na Tabia ya beberu ya kupenda kumiliki zizi.
Lakini wa mwisho anamtaja pia, Mfalme asiyeasika. Ambaye ni mtawala wa Nchi. Kama tunavyojua wafalme ndio viongozi wa taifa, humiliki vyote, na yoyote atakayekatiza mbele yake kujaribu kuuangusha ufalme wake, humuua. Mfalme ni zaidi ya raisi, Wafalme wengi waliteka ngome kwa vita, sio kwa kuchaguliwa, Ujasiri na misimamo yao huwamilikisha.
Ni hekima gani tunaipata?
Hivyo mwandishi wa mithali anajaribu kuonyesha , ujasiri na ushujaa ambao na sisi tunaweza kuupata endapo tutakuwa ndani ya Kristo. Bwana atatufanya tuwe na roho kama za wanyama hawa, mienendo yetu itakuwa bila WOGA sikuzote. Tutaishi kama watu wasio na mashaka kwa lolote. Hatutaogopa wanadamu, wala matatizo, wala wachawi, wala magonjwa, wala shida yoyote. Kwasababu tunajua uwezo wa kuyashinda hayo na kuyamiliki tunao mfano wa Simba na mfalme.
Bwana Yesu aliye mfalme wetu, anayemiliki sasa mbinguni na duniani, Simba wa Yuda, aliyashinda na sisi pia tutayashinda endapo tutakuwa ndani yake alisema hivyo.
Yohana 16:33 “…jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu”.
Je! Utapenda kumpa leo Yesu maisha yako? Ili aanze upya na wewe, akupe tumaini jipya la uzima wa milele? Na ujasiri wa kuishi hapa duniani bila woga?
Kama jibu ni ndio basi fuatiliza mwongozo huu, na Leo Leo utaupokea wokovu >> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP
Mada Nyinginezo:
MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!
NI NINI KITAKACHOTUFANYA TUPIGE MBIO BILA KUPUNGUZA MWENDO?
Biblia inamaana gani kusema “vipo sita, naam saba”?
Ni kwa namna gani Yesu ni Simba wa Yuda?
Je ni kweli Isaka alifarijika kwa kifo cha mamaye? (Mwanzo 24:67)
Kupwelewa maana yake nini? (Matendo 27:26).
YATAMBUE MAJIRA YA KUJILIWA KWAKO.
INAYOENDELEA SASA NI HUDUMA YA RUTHU.
Rudi nyumbani
Print this post
Mungu amibariki latina jina la bwana wetu yesu kristo