Biblia inamaana gani kusema “vipo sita, naam saba”?

Biblia inamaana gani kusema “vipo sita, naam saba”?

SWALI: Biblia inamaana gani kusema “vipo sita, naam saba”. Kwanini isingesema tu mara moja saba, mpaka ianze sita,halafu tena saba?


JIBU: Ni lugha ya zamani, iliyotumika kuwekea msisitizo kitu hususani kile cha mwisho, yaani, kama inadhaniwa ni sita, basi kipo na cha saba ambacho ndio zaidi.

Kwa mfano ukisoma ile Mithali 6:16  inayozungumzia mambo sita ambayo Mungu anayachukia utaona anaongezea na kingine cha saba, ambacho  ni “kupanda mbegu ya fitina katika ya ndugu” ikiwa na maana hicho ndio kibaya zaidi..

Mithali 6:16 “Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.

17 Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;

18 Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu;

19 Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu”.

Ukisoma pia  Mithali 30:18 “utaona Sulemani anasema tena kati ya mambo ambayo yanamshangaza mienendo yao, yapo matatu lakini lile la nne ndio zaidi, ambalo ni mwendo wa kijana pamoja na msichana.

Mithali 30:18 “Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu, Naam, kuna manne nisiyoyafahamu.

19 Mwendo wa tai katika hewa; Na mwendo wa nyoka juu ya mwamba; Mwendo wa merikebu katikati ya bahari; Na mwendo wa mtu pamoja na msichana”.

Vivyo hivyo, ukisoma Mithali 30:29, Sulemani anasema pia vipo vitu vitatu vyenye mwendo wa kupendeza lakini akakiongezea na cha nne chenye mwendo wa kupendeza zaidi nacho ni mfalme asiyehasika.

Mithali 30:29 “Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza, Naam, wanne walio na mwendo mzuri.

30 Simba aliye hodari kupita wanyama wote; Wala hajiepushi na aliye yote;

31 Jimbi aendaye tambo; na beberu; Na mfalme ambaye haasiki”.

Soma, pia vifungu hivi;

Mithali 30:15 “Mruba anao binti wawili, Waliao, Nipe! Nipe! Kuna vitu vitatu visivyoshiba kamwe, Naam, vinne visivyosema, Basi!

16 Kuzimu; na tumbo lisilozaa; Nchi isiyoshiba maji; na moto usiosema, Basi!”

Ayubu 5:19 “Yeye atakuokoa na mateso sita; Naam, hata katika saba hapana uovu utakaokugusa.

Amosi 1:3 “Haya ndiyo asemayo Bwana; Kwa makosa matatu ya Dameski, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameipura Gileadi kwa vyombo vya kupuria vya chuma”;

Soma pia Amosi 1:4.

Na hata sasa, katika mambo saba(7) ambayo  biblia inasema yanamkamilisha mwanadamu, lipo la nane(8) ambalo ndio kuu zaidi linaloitwa UPENDO.

Tusome.

2Petro 1:5 “Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa,

6 na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa,

7 na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, UPENDO.

8 Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.

Ni vizuri tukawa na hayo mengine yote, lakini tukikosa upendo wa Ki-Mungu, basi bado hatujakamilishwa.

Je! Upendo wa AGAPE upo ndani yako?

Ili kufahamu tunaupate upendo wa namna hii, fungua link hii>>

https://wingulamashahidi.org/2020/12/21/nitaupataje-upendo-wa-ki-mungu-ndani-yangu/ 

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?

NI NINI KITAKACHOTUFANYA TUPIGE MBIO BILA KUPUNGUZA MWENDO?

UFUNUO: Mlango wa 1

Je! kuna madhara kuchukiwa na kila mtu kwasababu huna mali?. Kama biblia inavyosema katika Mithali 14:20?.

Mpumbavu ni nani katika biblia? (Zaburi 14:1, Mithali 10:14)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments