Title 2024

Fahamu mana ya Zaburi 48:14 Yeye ndiye atakayetuongoza

SWALI: Ipi tafsiri ya Zaburi 48:14 ?

[14]Kwa maana ndivyo alivyo MUNGU, Mungu wetu. Milele na milele  Yeye ndiye atakayetuongoza.


JIBU: Mwandishi anajivunia sifa ya Mungu wao wa milele. kwamba ndiye atakayewaongoza.

Akiwa na maana atayewaongoza katika mambo yao yote, kwamba kamwe hawezi kuwaacha, atakayewaongoza njia sahihi ya uzima, njia sahihi ya kupigana vita, ya kujenga na kupanda.

Ndivyo ilivyokuwa kwa wana wa Israeli. Mungu alikuwa nao jangwani kwa nguzo ya moto na wingu kuwaongoza, aliwapelekea malaika wake kuwalinda, aliwafundisha namna ya kupata faida katika shughuli zao, akawainulia na waamuzi, pamoja na wafalme na manabii kuwachunga na mwisho akawaletea mkombozi, ambaye ndio ukamilifu wa yote. Kuonyesha wema wake na kiu yake ya kuwaongoza  watu wake.

Hata sasa, sifa yake ndio hiyo hiyo, ndio maana na sisi tuna ujasiri wa kusema…

‘Yeye ndiye atakayetuongoza’.Sio tu kwa wakati huo, bali mpaka siku ya kufa kwetu.

Alipokuja mwokozi hakutuacha hivi hivi kama mayatima, bali alituachia msaidizi ambaye anatuongoza na kututia katika kweli yote, ndiye Roho Mtakatifu.

Yohana 16:13

[13]Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.

Bwana akubariki.

Je umempokea Yesu?  Kama bado ni nini unasubiri ? Fungua hapa kwa mwongozo wa sala  ya toba ya imani. >>>>KUONGOZWA SALA YA TOBA

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MANA ILIYOSHUSHWA KUTOKA MBINGUNI.

Fahamu maana ya Mhubiri 10:9 Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo;

Kwanini Yesu Kristo ni mwana wa Adamu?

Rudi Nyumbani

Print this post

‘Waibao watu ‘ sawasawa na 1Timotheo 1:10 humaanisha nini?

SWALI: Biblia inapowataja ‘waibao watu ‘ sawasawa na 1Timotheo 1:10 humaanisha nini?


JIBU: Tusome;

1 Timotheo 1:8-10

[8]Lakini twajua ya kuwa sheria ni njema, kama mtu akiitumia kwa njia iliyo halali;

[9]akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu wa haki, bali waasi, na wasio wataratibu, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji,

[10]na wazinifu, na wafiraji, na WAIBAO WATU, na waongo, nao waapao kwa uongo; na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;

Tangu zamani dhambi ya wizi, haikuwa tu katika vitu na mali, bali ilikuwa hata katika watu. Ndio kilele cha juu kabisa cha wizi.

Wizi huu ulikuwa na  malengo mbalimbali mojawapo ilikuwa ni kuwapeleka vitani, lakini pia kuwauza kama watumwa. Kama tunavyofahamu katika historia bara la Afrika lilikumbwa na tatizo hili, katika karne ya 17, waafrika wengi waliibiwa, na kuuza katika mabara ya ulaya.

Lakini kwa nyakati hizi wizi huu, umekuwa mbaya zaidi, kwasababu watu hawaibi tena watu kwa lengo la kuwatumikisha, bali kwa lengo la kuwafanyisha biashara ya kikahaba, wengine kuwaua ili wachukue viungo vyao kwa kazi za kishirikina, wengine wauze viungo vyao vya ndani kama vile figo, ili wapate fedha.

Jambo ambalo ni baya sana, ndio maana kwenye maandiko katika enzi za agano la kale adhabu ya wizi wa watu  haikuwa ndogo bali kifo.

Kumbukumbu la Torati 24:7

[7]Mtu akionekana anamwiba nduguze mmojawapo katika wana wa Israeli, akamfanya kama mtumwa, au kumwuza; na afe mwivi huyo; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.

Lakini sisi katika agano jipya, hatuna ruhusa ya kuua watu wa namna hiyo, isipokuwa tuonapo vitendo kama hivyo vikitokea ni ripoti katika vyombo vya dola, hapo utaisaidia jamii, kudhibiti uovu kama huo Lakini pia kumwomba Mungu, aiondoe roho hii chafu isiwepo katikati ya  jamii zetu, ili kuiponya kuiponya jamii.

Na Mungu atakubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea. Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

ALIJARIBIWA SAWASAWA NA SISI KATIKA MAMBO YOTE.

Je! Malaika wanazaliana?

USIZISHIRIKI DHAMBI ZA WATU WENGINE.

Mikono iliyotakata ni mikono ya namna gani? (1Timotheo 2:8).

Rudi Nyumbani

Print this post

Marimari ni nini? (Luka 7:37)

Jibu: Tureje..

Luka 7:37  “Na tazama, mwanamke mmoja wa mji ule, aliyekuwa mwenye dhambi, alipopata habari ya kuwa ameketi chakulani katika nyumba ya yule Farisayo, alileta chupa ya MARIMARI yenye marhamu”.

 “Marimari” ni jina lingine la “Marumaru”, kwahiyo popote katika biblia palipotajwa Marimari ni sawasawa na Marumaru. Na marimari ni mawe ya kaboni, ambayo yanatumika katika urembo wa ujenzi, mawe haya ni maarufu sana kwa kutengenezea Tiles za ukutani au chini.

Vile vile yanatumika kutengenezea baadhi ya vyombo vya kinakshi mfano wa cha hicho cha mwanamke katika Luka 7:37 n.k

Maandiko mengine yanayotaja Marimari ni pamoja na 1Nyakati 29:2, Wimbo ulio bora 5:15 na Ufunuo 18:12… lakini andiko lililotaja Marimari kama Marumaru ni Esta 1:6.

Je umempokea BWANA YESU, na kubatizwa katika ubatizo sahihi?.. Je unatambua kuwa tunaishi katika majira ya kurudi kwa YESU mara ya pili, na wakati wowote parapanda ya mwisho inalia?

Je macho yako yanaona hayo yote?.. kama huyaoni hayo basi fahamu kuwa upo gizani na yule mkuu wa giza (shetani) amekupofusha macho ili usione, Leo harakisha kupokea msaada kutoka kwa YESU.

Ikiwa utahitaji kumpokea YESU leo, basi fuatiliza sala hii hapa >>KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Sala ya baraka (Hesabu 6:24-26).

NINI MAANA YA KUWA MKRISTO?

Ni lazima mtu aongozwe sala ya toba ili awe ameokoka?

SI KILA KILICHO HALALI KINAFAA.

TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.

Rudi Nyumbani

Print this post

Je ni sawa kuukubali udhaifu kama mtume Paulo alivyojisifia kwa huo? (2Wakorintho 12:9-10)

SWALI: Je udhaifu ni jambo la kulikubali? Kama tunavyoona mtume Paulo akiusifia katika;

2 Wakorintho 12:9-10
[9]Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juuyangu.

[10]Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.

Paulo Hajisifii udhaufu, kana kwamba ni mzuri wa kuvutia, hapana hakuna udhaifu ulio mzuri umfanyao mtu ajiivunie huo……lakini linapokuja eneo la Mungu, udhaifu humnyenyekesha mtu, na hivyo humfanya mtu huyo kutegemea zaidi nguvu za Mungu, kuliko uweza wake mwenyewe ndicho kilichokuwa kwa Paulo.

Anasema hakuwa mtu mwenye ujuzi wa maneno, au utashi mwingi wa kitume kama wanavyodhaniwa watumishi wa Mungu wote kuwa nao.

2 Wakorintho 10:10

[10]Maana wasema, Nyaraka zake ni nzito, hodari; bali akiwapo mwenyewe mwilini ni dhaifu, na maneno yake si kitu.

Lakini katika udhaifu huo wa kunena, maelfu ya watu walikuja kwa Kristo, katika udhaifu huo wa kimwili miujiza mikubwa ilifanyika kwa mikono yake. Hivyo akamshukuru Mungu kwa hilo, ili watu wasidhani ni kwa uwezo wake au kipawa chake fulani maalumu aliweza kuyafanikisha hayo.

Ndivyo tunavyojifunza hata kwa Musa, Mungu kumtumia kwa viwango vile haikuwa katika uweza wake wowote, kwasababu alikiri mbele za Mungu yeye sio mnenaji.(Kutoka 4:10), lakini pia Mungu alimshuhudia kuwa ni mpole kuliko watu wote waliokuwa duniani kipindi kile. Tofauti labda na makuhani wengine au manabii waliokuja au kuwepo kabla yake.(Hesabu 12:3)

hata leo, pale tunapojiona ni wadhaifu fulani mbele za Mungu kimaumbile au kiusemi, au kihali, hapo ndipo mahali pazuri pa kitumiwa na yeye. Usifadhaike wala usife moyo ukasema mimi siwezi, amini tu, kwasababu yeye hategemei ulichonacho, bali Neno lake moyoni mwako, ukiliweka yote yawezekana kwako. Amini tu.

1 Wakorintho 1:26-29

[26]Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;

[27]bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;

[28]tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; [29]mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. 

fuatilia ushuhuda hizi zitakujenga..

USHUHUDA WA RICKY:

JE UDHAIFU WANGU UNAWEZA KUZUIA INJILI?

Lakini hilo halimaanishi kwamba udhaifu wowote ni mzuri, kwamba tujivunie katika hayo, hapana hakuna raha katika ulemavu, au katika ububu, au katika upofu..Lakini tujapo kwa Kristo ni mtaji mzuri wa Mungu kututumia. Hiyo ni kutudhuhirishia kuwa kwa Mungu hakuna kiungo hata kimoja ambacho hakiwezi kumtumikie yeye. Sote kwa pamoja tuwe na elimu tusiwe na elimu, tuwe na afya tusiwe na afya, tuwe na vijijini tuwe mijini, tunajukumu la kumtumikia Mungu, na kufanya vema kabisa.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.


Mafundisho mengine:

MUNGU ALIVICHAGUA VITU AMBAVYO HAVIKO.

USIMLAANI KIZIWI, WALA USITIE KWAZO MBELE YA KIPOFU.

Ipi tofuati ya “Kutakabari” na “kutakabali”?

Rudi Nyumbani

Print this post

Nini maana ya hekima ya maskini haisikilizwi? (Mhubiri 9:16)

Swali: Katika Mhubiri 9:16, neno la Mungu linasema kuwa hekima ya maskini haisikilizwi, je na sisi tunapaswa tusizisikilize hekima/mashauri ya watu wasio na kitu, ili kujinusuru..au andiko lina maana gani?


Jibu: Turejee..

Mhubiri 9:16 “Ndipo niliposema, Bora hekima kuliko nguvu; WALAKINI HEKIMA YA MASKINI HUDHARAULIWA, WALA MANENO YAKE HAYASIKILIZWI”.

Tukiusoma huo mstari peke yake ni rahisi kuona au kujifunza kuwa “hatupaswi kusikiliza watu maskini” hususani wanapopendekeza mambo.. (na watu maskini ni pamoja na kundi la watu wasio na elimu kabisa).. Lakini hebu tuanzie ule mstari wa 13, tuone kama hiyo ndio maana yake.

Mhubiri 9:13 “Pia nimeona hekima chini ya jua, nayo ni kama hivi, tena kwangu mimi ilionekana kuwa ni neno kubwa.

14 Palikuwa na mji mdogo, na watu ndani yake walikuwa wachache; akaja mfalme mkuu juu yake, akauhusuru, akajenga ngome kubwa ili kuupiga.

15 BASI, KULIONEKANA HUMO MTU MASKINI MWENYE HEKIMA, naye kwa hekima yake akauokoa mji ule lakini hata hivyo hapakuwa na mtu ye yote aliyemkumbuka yule mtu maskini.

16 Ndipo niliposema, BORA HEKIMA KULIKO NGUVU; walakini hekima ya maskini hudharauliwa, wala maneno yake hayasikilizwi”.

Huyu Maskini alikuwa na Hekima ya kuuokoa mji, ijapokuwa hakuwa na elimu, wala ujuzi mwingi, pengine wala hakuwa katika siasa ya nchi, lakini alitoa wazo bora, na kufanya nchi isiingie katika vita. Lakini baada ya mji kuokoka na kuwa na Amani, hawakumkumbuka yule maskini kwa kumpa thawabu.

Hilo halikumshangaza sana Sulemani, lililomshangaza Zaidi ni kuona  kuwa “KWANINI HEKIMA ZA MASKINI HAZISIKILIZWI”.. na wakati hao wanazo hekima za kuweza hata kuunusuru mji usiangamie!!!, kama mfano wa huyo tuliyemsoma hapo juu.

Hilo likamshangaza sana Sulemani, na ushauri wake ni kwamba tuwatafute hao (maskini) na kujaribu kusikiliza mashauri yao na tusiwadharau kwani baadhi yao wamebeba vitu vikubwa…

Na ndipo akasema Bora kuwa na hekima kama huyu kijana maskini kuliko kuwa na nguvu (za kimwili na kifedha na kielimu) na kukosa hekima.

Mhubiri 9:16 “Ndipo niliposema, Bora hekima kuliko nguvu; WALAKINI HEKIMA YA MASKINI HUDHARAULIWA, WALA MANENO YAKE HAYASIKILIZWI”.

Hivyo kwa tafakari hiyo tutakuwa tumeshapata jibu kuwa sio kwamba Biblia inatufundisha kutowasikiliza maskini au kuwadharau…bali kinyume chake inatufundisha “tusiwe na dharau nao, kwani kwa sehemu moja, wapo baadhi wenye hekima hata za kuweza kuokoa Taifa, mfano wa huyo tuliyemsoma hapo juu”.

Hivyo ndugu usimdharau mtu ambaye unaona ni mnyonge kuliko wewe, ambaye unaona pengine hana mali kama ulizonazo wewe, au hana uwezo kama ulionao wewe, au hana elimu kama uliyo nayo wewe… Watu hao unaowadharau wewe baadhi yao wamebeba vitu vikubwa sana kwaajili yako, ambavyo vinaweza kukusaidia wewe au watu wako!.

Hivyo sikiliza watu wote, na chuja mambo yote. Si wote walio maskini ni wajinga, na pia si maskini wote wana hekima… vile vile si wote walio matajiri wanazo akili, wengi hawana akili wala hekima ingawa mbele za watu wanaweza kusifika..

Biblia inasema heri kijana maskini mwenye hekima, kuliko mfalme mzee halafu mpumbavu (Soma Mhubiri 4:13).

Hivyo hatuna budi kuwa watu wanyenyekevu daima na wenye kusikiliza.

Bwana atusidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 1)

NGUVU YA HEKIMA NA AKILI

HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?

TOA HUDUMA ILIYO BORA.

Rudi Nyumbani

Print this post

Kwa namna gani Bwana YESU atagawiwa sehemu pamoja na wakuu? (Isaya 53:12)

Swali: Katika Isaya 53:13 tunausoma unabii wa Masihi (yaani YESU), Kwamba atakuja kugawiwa sehemu pamoja na wakuu…je! hawa wakuu ni akina nani atakaokuja kugawiwa nao sehemu?…na nini kinagawiwa hapo?


Jibu: Turejee…

Isaya 53:12 “Kwa hiyo nitamgawia sehemu PAMOJA NA WAKUU, Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini ALICHUKUA DHAMBI ZA WATU WENGI, Na kuwaombea wakosaji”.

Mstari huo ni kweli unamhusu BWANA YESU (Aliye Masihi) na ni  rahisi kutafsirika hivi “kwamba kuna wakuu wanaoishi ambao Bwana YESU naye atakuja kupewa sehemu pamoja nao”.

Tafakari hii sio sahihi, na wala sio maana ya maandiko hayo…kwani hakuna mwanadamu yoyote anayeweza kulinganishwa na YESU wakati huu wa sasa na hata baada ya maisha.

Sasa maana halisi ya mstari huo ni ipi?.

Maana ya mstari huo ni hii… “Mungu atamgawia sehemu Bwana YESU na pia atawagawia sehemu WAKUU”…Maana yake Bwana ana sehemu yake na hao wakuu wana sehemu yao..lakini wote watakuwa na sehemu.

Ndio tukiunganisha maneno hayo mawili tunapata sentensi hiyo “ Mungu atamgawia  sehemu pamoja na WAKUU”...

Sasa hiyo sehemu ni ipi na hao wakuu ni akina nani?

“Sehemu” inayozungumziwa hapo ni “Mji wa kimbuinguni, Yerusalemu Mpya” (Soma Ufunuo 22:19).

Na “Wakuu” wanaozungumziwa hapo ni watakatifu watakaoshinda siku ile,  hao ndio wanaoitwa “wakuu”. (Wale watu wote walioishi maisha ya kujinyenyekeza kama watoto walipokuwa duniani) sawasawa na Mathayo 18:2-3.

Mathayo 18:2 “Ni nani basi aliye MKUU katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao,

3 akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni”

Soma pia Luka 7:28 utaliona jambo hilo hilo.

Kwahiyo sehemu ya BWANA YESU ni KITI CHA ENZI CHA DAIMA… na sehemu ya watakatifu watakaoshinda, ambao wataitwa wakuu ni YERUSALEMU MPYA.

Na wanadamu wengine ambao hawatakuwepo katika hilo kundi la ‘wakuu’, basi hawana sehemu yoyote katika mji mtakatifu, bali biblia inasema sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti.

Ufunuo wa Yohana 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, SEHEMU YAO NI KATIKA LILE ZIWA LIWAKALO MOTO NA KIBERITI. HII NDIYO MAUTI YA PILI”.

Tujitahidi tukapate sehemu pamoja na Bwana WETU.

Tujinyenyekeze kama watoto, tukatae udunia na kumwamini YESU, tuache dhambi na tuichukie, tutafute haki na kusimama imara.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MKUU WA ANGA.

Nini maana ya Mhubiri 10:16, inaposema Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana?

Mbari ni nini kibiblia?

Mbinguni ni sehemu gani?

Fahamu Namna ya Kuomba.

Rudi Nyumbani

Print this post

Maana ya Mhubiri 10:15 Kazi yao wapumbavu huwachosha kila mmoja,

SWALI: Je, mstari huu tunaousoma kwenye Mhubiri 10:15 una maana gani?

Mhubiri 10:15

[15]Kazi yao wapumbavu huwachosha kila mmoja, Maana hajui hata njia ya kuuendea mji.


JIBU: Kwa namna ya kawaida ya kibinadamu tunajua watu wengi hutamani kuishi mijini kuliko mashambani. Kwasababu mijini huduma zote hupatikana, na ni mahali pa raha. Hata kazi, mtu anazozifanya mashambani, wengi wao ni ili matunda yake wakayafurahie mjini, Au wakaziuze bidhaa zao huko wawe matajiri.

lakini tengeneza picha mtu, ambaye anajitaabiisha kufanya kazi kwa lengo la kuzifurahia mjini, halafu hajui njia ya kufika huko, kinyume chake ndio anakwenda mbali zaidi na mji, anaelekea majangwani au mabondeni?  ni wazi kuwa mtu kama huyo  hawezi kuwa na raha katika kazi yake, kwasababu taabu yake haina faida, alikosa malengo au hakuwa na maarifa sahihi.

Ni ufunuo gani upo nyuma yake?

Na sisi pia tuliomwamini Kristo. Tuna mji ambao tunatarajia kuungia, ndio ule Yerusalemu mpya ishukayo kutoka mbinguni kwa Baba..

Ufunuo  21:2-3

[2]Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. 

 [3]Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. 

Anaendelea kusema…

Ufunuo  22:14-15

[14]Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. 

[15]Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.

Huo ndio ule mji halisi ambao hata Ibrahimu aliona, ikamfanya aishi maisha kama ya mpitaji hapa duniani.

Waebrania 11:8-10

[8]Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. 

 [9]Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. 

 [10]Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu. 

Umeona na sisi ili tuweze kuonekana tumestahili kuuingia katika mji huo wa mbinguni hatuna budi tuwe tumeokolewa na YESU KRISTO. Kwasababu yeye ndio NJIA ya kuuingia mji.

Ukiwa nje ya Kristo tafsiri yake wewe ni mpumbavu, kwasababu taabu yako yote ya hapa duniani, haikufikishi popote haikuepeki mjini mwa Mungu, itakuchosha tu, utakuwa na magorofa, utaijaza akaunti fedha, utakuwa ni miradi mikubwa lakini mwisho utakufa, na kwenda kaburini. Lakini ukiiona njia na kuifuata Yerusalemu basi hufanyi kazi ya bure, unapojiwekea hazina kule hufanya kazi ya kushosha, ni uzima baada ya kifo. Utafaidi matunda yake

Je umeokoka?

Ikiwa bado na unatamani kufanya hivyo, basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala hiyo >>>  KUONGOZWA SALA YA TOBA

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Yerusalemu ni nini?

KWANINI KILA MWAMINI ANAPASWA AWE MHUBIRI WA INJILI

(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)Maana ya Mhubiri 1:9 “wala jambo jipya hakuna chini ya jua”. (Opens in a new browser tab)

MJI WENYE MISINGI.(Opens in a new browser tab)

Rudi Nyumbani

Print this post

Nini maana ya “Naliazimu nisijue neno lolote kwenu?” (1Wakorintho 2:2).

Jibu: Turejee..

1Wakorintho 2:2 “Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa”

Haya ni maneno ya Mtume Paulo aliyowaambia watu wa kanisa la Korintho… sasa tunaweza kuyaweka katika lugha rahisi namna hii…. “Nilipokuja kwenu (ninyi Watu wa Korintho) nilikusudia kufahamu yale mnayoyajua kumhusu YESU KRISTO, ambaye amesulubiwa na si jambo lingine lolote”.

Maana yake Paulo alitaka kuelewa ni nini Wakorintho wanaelewa kumhusu YESU aliyesulubiwa, hicho tu ndicho alicholenga kujua, na hakutaka kujua mambo mengine..

Kwanini alitaka kujua ufahamu wao kuhusu YESU?…

Ni kwasababu alijua kama wakimfahamu YESU kama inavyopaswa kufahamika, basi Imani yao itakuwa katika msingi thabiti.. Lakini kama wakimfahamu Yesu kwa ushawishi wa Maneno, basi Imani yao itakuwa katika hekima za kibinadamu.

1Wakorintho 2:1 “Basi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima.

2  Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa.”

Vile vile kama watamfahamu YESU wa ishara na miujiza tu, basi Imani yao itakuwa katika miujiza  na ishara kama wale Wasamaria (Yohana 6:26) na si katika Imani thabiti ya YESU ALIYESULIBIWA

Lakini kama wakimfahamu YESU kama Mwokozi aliyesulibiwa kwaajili ya makosa yao na dhambi zao, basi Imani yao itakuwa thabiti, na yenye uhakika.. Itakayowapelekea kuungama dhambi, na kutafuta kuyafanya mapenzi ya Mungu, jambo ambalo ni msingi sana, na ambalo ndio tiketi ya kumwona Mungu (Mathayo 7:21-23)

Hivyo na sisi kilicho kikubwa na cha Msingi ni kuishikilia ile Imani ya Msingi (ambayo ndio Imani mama), ambayo inatupeleka/kutusukuma kujitakasa na kujiepusha na uchafu(dhambi).

Bwana atusaidie, na Bwana atubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je! Kiongozi wa dini anaouwezo wa kusamehe dhambi?

LAKINI HAITAKUWA HIVYO KWENU.

MSIJISUMBUE KWA NENO LOLOTE.

Je! dhambi zote ni sawa Kuna dhambi kubwa na ndogo?

MSINGI WA NYUMBA YA MUNGU, NI JINA LA MUNGU.

Rudi Nyumbani

Print this post

NDOA TAKATIFU NI MKE MMOJA/MUME MMOJA.

Ndoa za wake wengi ni za ibilisi!..ndoa za wake wengi ni za ibilisi!!… ndoa za wake wengi ni za ibilisi!!!. Hali kadhalika ndoa za waume wengi ni za ibilisi, kama tu zilivyo za jinsi moja (zote ni zao la ibilisi).

Zipo hoja kuwa kwasababu Daudi, Sulemani na manabii wengine wakale walioa wake wengi, basi hata leo ni halali kuoa wake wengi.. tena zipo hoja zifananishazo wanyama wa porini na wa kufungwa na uhalali wa kuoa wake wengi.

Hoja zote hizi ni za ibilisi… Ndugu, usiongeze wake, wala wala usiongezee waume.

Bwana YESU alipokutana na yule mwanamke Msamaria kisimani hakumwambia akawalete WAUME ZAKE!.. Ingawa alikuwa ana wanaume wengi (na Bwana alilijua hilo), lakini alimwambia nenda “kamlete mumeo”… ikimaanisha kuwa ndoa halali na takatifu ni ya mume mmoja na mke mmoja.

Sasa Kristo alikuwa anamjua Sulemani, na Daudi..

Yohana 4:15 “Yule mwanamke akamwambia, Bwana, unipe maji hayo, nisione kiu, wala nisije hapa kuteka.

16  Yesu akamwambia, NENDA KAMWITE MUMEO, uje naye hapa.

17  Yule mwanamke akajibu, akasema, Sina mume. Yesu akamwambia, Umesema vema, Sina mume;

18  kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako; hapo umesema kweli”.

Bwana YESU kabla ya kukutana na huyu mama, alikuwa anamjua Daudi pamoja na Sulemani na idadi ya wake wake waliooa!.. Lakini tunaona hakumwambia huyu mwanamke Msamaria, kwamba akawalete waume zake!!.. Bali alimwambia kamlete mumeo! (maana yake mmoja tu).. bado huoni tu, kuwa ndoa za mitara ni batili na za ibilisi!.

Na tena biblia inasema hapo Mwanzo Mungu alimwumba mwanaume na mwanamke, na si mwanaume na wanawake, au mwanamke na wanaume (soma Mwanzo 1:27 na Mathayo 19:4).

Huoni kuwa ndoa hizo za wake wengi zitakukosesha maji ya uzima!.. Na pia fahamu kuwa ndoa za wake wengi sio zile tu zinazohusisha mtu kuwa na wake wengi katika boma moja kwa wakati mmoja…la! Hata zile za kuacha na kuoa mwingine ilihali yule wa kwanza bado yupo hai.. hiyo ni mitara! Ndicho kilichokuwa kwa huyu mwanamke Msamaria.

Huyu mwanamke msamaria alikuwa na wanaume watano kulingana na darubini ya kimbingu! Ingawa haishi nao, lakini alikuwa nao watano, na anayeishi naye ni wa 6, vile vile kuna watu leo hii wamecha wake zao na kuoa wengine, na kuacha tena na kuoa wengine, (hawa hawana tofauti na wale waliooa wake wawili na kuishi nao wote kwa pamoja).

Na madhara ya ndoa za mitara ni “KUKOSA MAJI YA UZIMA”..

Yapo maji ya Uzima tuyanywayo hapa Duniani, na yapo yale tutakayoyanywa katika mbingu mpya na nchi mpya.

Maji ya Uzima duniani ni YESU KRISTO, tumpatapo yeye tunapata uzima wa milele (Yohana 4:14), lakini ukijiunganisha na hizi ndoa za mitara hawezi kuingia ndani yako!.. vile vile maji ya uzima baada ya maisha haya tutayanywa kutoka katika ule mto wa maji ya Uzima katika mbingu mpya na nchi mpya.

Ufunuo 22:1 “Kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo,

2  katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.

3  Wala hapatakuwa na laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumwa wake watamtumikia;

4  nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao.

5  Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele”.

Neema ya Bwana YESU itufunike.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MAFUNDISHO YA NDOA.

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU NDOA.

VIGEZO VYA KUWA KARIBU NA YESU KRISTO KATIKA ULIMWENGU UJAO.

NDOA NI NINI?

KUWA NA  MAFUTA YOTE YA ROHO MTAKATIFU NDANI YAKO.

Rudi Nyumbani

Print this post

Je! Malaika wanazaliana?

Wapo wanaodhani kuwa malaika wanao uwezo wa kuzaliana sawasawa na habari ya wana wa Mungu na binti za wanadamu inayozungumzwa  katika kitabu cha Mwanzo.

Mwanzo 6:1-3,  Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,

2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.

3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.

Kwa habari hiyo wengi hufikiri, hao wana wa Mungu walikuwa ni malaika, ukweli ni kwamba hawakuwa malaika bali wanadamu. Yesu alisema, tutakapofika mbinguni, hatutaoa wala kuolewa, tutafanana na malaika, Kuonyesha kuwa malaika hawazaliani. (Mathayo 22:30)

Vilevile katika habari hiyo hatuoni kwamba malaika wakiadhibiwa, bali wanadamu, kuonyesha kuwa ni jambo la kibinadamu. Kwa urefu wa fundisho hilo, fungua hapa >>> WANA WA MUNGU, NA BINTI ZA WANADAMU.

Viungo vya uzazi viliumbwa mahususi kwa viumbe wa ulimwenguni, kwa lengo la kuijaza nchi. Lakini vya mbinguni havikuumbwa kwa utaratibu kama huu wa kwetu.

Hivyo kwa hitimishi ni kuwa malaika watakatifu hawazaliani. Kwasababu wao ni viumbe vya rohoni, waishio milele. Hivyo hawahitaji kuzaliana.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je! mbinguni kuna malaika wa kike?. Na je! tukifika mbinguni tutafanana wote?

Je malaika wote wana wabawa?

KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA.

Rudi Nyumbani

Print this post