Watu wa nyumbani mwa Kaisari ni watu gani? (Wafilipi 4:22).

Watu wa nyumbani mwa Kaisari ni watu gani? (Wafilipi 4:22).

Swali: Watu wa nyumbani mwa Kaisari wanaotajwa na Mtume Paulo katika Wafilipi 4:22 walikuwa ni watu wa aina gani?


Jibu: Turejee…

Wafilipi 4:21 “Mnisalimie kila mtakatifu katika Kristo Yesu. Ndugu walio pamoja nami wawasalimu. 

22 Watakatifu wote wawasalimu, hasa wao walio wa NYUMBANI MWA KAISARI”

Kaisari anayezungumziwa hapo ni yule mfalme mkuu wa Rumi (ambaye ndiye aliyekuwa mfalme wa dunia wakati ule).

Sasa watu wwa nyumbani mwake wanaozungumziwa hapo si watoto wake, bali ni watu waliokuwa wanatumika katika nyumba yake.

Katika enzi yake walikuwepo wengi (maskini na matajiri, wanaume kwa wanawake) waliokuwa wanatumika katika nyumba yake, sasa miongoni mwa hao ambao Paulo hajawataja majina yao, walimwamini Bwana YESU na kuokoka.

Na ndio hao Paulo anafikisha salamu zao kwa kanisa la Filipi.

Hii ikifunua kwamba injili ya Bwana YESU ilipenya hata katika majumba ya wafalme wa dunia.

Na si Kaisari tu! Utaona pia hata aliyekuwa mke wa wakili wa Herode aliyeitwa Yoana alikuwa mfuasi wa Bwana YESU, na ndiye aliyekuwa anamhudumia Bwana kwa mali zake pamoja na baadhi ya wanawake, huyu naye alikuwa miongoni mwa watu wa nyumba ya Herode.

Luka 8:2 “na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba, 

3 na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao”.

Na sisi hatupaswi kuionea haya injili, wala kubagua watu wa kuwahubiria, bali injili inawastahili watu wote (maskini na matajiri, wenye cheo na wasio na cheo), kwa maana ni uweza wa Mungu uletao wokovu kama maandiko yasemavyo..

Warumi 1:16 “Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia”

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618.

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

VYA MUNGU MPENI MUNGU.

Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

FUNDISHA NENO KANISANI NA NYUMBANI.

TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI.

MAASI KUONGEZEKA NI ISHARA YA NINI?.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments