Swali: Kile KIWI, kilichomwangukia yule Elima mchawi ni kitu gani?.
Jibu: Tuanzie ule mstari wa nane (8) ili tuelewe vizuri..
Matendo 13:8 “Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. 9 Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, 10 akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? 11 Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. MARA KIWI kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza”.
Matendo 13:8 “Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani.
9 Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho,
10 akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?
11 Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. MARA KIWI kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza”.
Kiwi kinachozungumziwa hapo si rangi ya viatu bali ni “ukungu mweusi” unaotokea katika macho, aidha kutokana na ugonjwa au mwanga mkali unapomulika macho kwa ghafla!.
Ukungu huu unapompata mtu unamfanya asione kwa muda au moja kwa moja.
Mfano kwa watu waliopatwa na kiwi ndiye huyo Elima mchawi aliyekuwa anashindana na kweli ya Mungu, na huku akitaka kumtia yule liwali Sergio moyo wa kuiacha ile imani.
Vile vile mtu mwigine aliyeangukiwa na “KIWI” ni Paulo mwenyewe alipokuwa anaelekea Dameski, akipokutana na Bwana na mwanga ule mkali wa Bwana, ukatia macho yake KIWI kama ilivyomtokea huyu Elima, mchawi….na Sauli (ambaye ndiye Paulo) akawa kipofu kwa muda wa siku tatu.
Matendo 9:8 “Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. 9 Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi”.
Matendo 9:8 “Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski.
9 Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi”.
Mistari mingine ya biblia inayozungumzia “KIWI” ni pamoja na Ayubu 17:5, Ayubu 31:16, Isaya 32:3, Isaya 58:10 na Zekaria 14:6.
Vile vile na leo kuna watu wanashukiwa na Kiwi cha kiroho wanapoenda kinyume na Mwanga wa Neno la Mungu.
Inapopingana na kweli, maana yake inakabiliana na Nuru na hivyo itakupofusha macho.
Ayubu 11:20 “Lakini macho ya waovu yataingia kiwi, Nao hawatakuwa na njia ya kukimbilia, Na matumaini yao yatakuwa ni kutoa roho”
Na hiyo ndio sababu ya Bwana YESU kusema..
Yohana 9:39 “Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu”.
Sasa wanaoona na kufanywa vipofu ni jamii ya hao watu waendao kinyume na nuru, na wale wasioona wapewe kuona ni wale wanaotembea katika uelekeo wa nuru inapomulika.
Kwa urefu kuhusiana maneno hayo basi fungua hapa 》》》Ni kwa namna gani Bwana amekuja kuwafanya wanaoona wawe vipofu?
Je umempokea Bwana YESU?…Je unaenda katika Nuru yake au kinyume na Nuru.
Kama bado hujaokoka, ni vyema ukafanya maamuzi leo kabla ule mlango wa Neema kufungwa.
Kama utahitaji msaada huo wa kjmpokea Bwana YESU maishani mwako basi wasiliana nasi kwa namba zetu..
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
ELIMA MCHAWI, ANAFANYA KAZI HADI SASA.
BUSTANI YA NEEMA.
UJUE UCHAWI WA MANABII WA UONGO?.
Usimwache mwanamke mchawi kuishi! Biblia ilimaanisha nini?
MAMBO MANNE(4) YAFANYAYO NENO LA MUNGU.
Rudi Nyumbani
Print this post