Usimwache mwanamke mchawi kuishi! Biblia ilimaanisha nini?

Usimwache mwanamke mchawi kuishi! Biblia ilimaanisha nini?

SWALI: Nina swali juu ya uchawi, Biblia iliposema kuwa usimwache mwanamke mchawi kuishi ilimaanisha nini?


JIBU: Katika agano la kale Mungu aliwapa wana wa Israeli hukumu…akawaambia wazishike hizo..na hukumu hizo ni kwa wale wote watakaokwenda kinyume na Torati…Kwamfano Torati ilikataza KUZINI..Mojawapo wa zile amri kumi ilikuwa ni USIZINI.

Hivyo mwanamke/mwanamume yeyote atakayeivunja hiyo sheria..adhabu yake ilikuwa ni KIFO!..Na walioitekeleza hiyo hukumu walikuwa ni hao hao wana wa Israeli kufuatia maagizo waliyopewa na Mungu mwenyewe…Kwamfano mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, adhabu yake ilikuwa ni kupigwa mawe mpaka kufa!..aliyekamatwa vilevile analala na mnyama adhabu yake ilikuwa ni kifo,

Hebu tusome baadhi ya hukumu hizo

Walawi 20:10 “Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naam, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.

11 Na mtu mume atakayelala pamoja na mke wa baba yake amefunua utupu wa baba yake; wote wawili hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.

12 Na mtu mume akilala na mkwewe mwanamke wote wawili hakika watauawa; wamefanya yaliyo uchafuko; damu yao itakuwa juu yao.”

Kutoka 22: 19 “Mtu awaye yote alalaye na mnyama sharti atauawa”.

Na sio hizo tu!…kulikuwa na sheria zilizokuwepo za kumuua ndugu yako wa damu endapo atakwenda kuabudu miungu mingine tofauti na Mungu wa Israeli. Na zaidi ya hayo Mungu alikataza shughuli zozote za kishirikina na kichawi katika Taifa takatifu la Israeli..

Kumbukumbu 18: 9 “Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale.

10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,

11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, WALA MCHAWI, wala mtu awaombaye wafu.

12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.

13 Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako”.

Sasa yeyote Yule aliyekiuka amri hiyo Mungu aliyoitoa ya kutojihusisha na ushirikina na uchawi..hukumu yake ilikuwa ni kifo tu!..Ndio hapo Musa akaiandika hiyo hukumu katika..

Kutoka 22:18 “Usimwache mwanamke mchawi kuishi. 19 Mtu awaye yote alalaye na mnyama sharti atauawa”.

Maana yake mwanamke/mwanamume akikamatwa katika ushirikina ni kuuawa kwa aidha kupigwa kwa mawe au kwa vyovyote vile…(ilimradi afe tu)

Kwahiyo sheria ya kuwaua wachawi ilikuwepo kama tu sheria ya kumuua mwanamke aliyekamatwa katika uzinzi..

Lakini sasa katika agano jipya la Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristo..wanadamu hatujapewa tena mamlaka ya kuhukumu kutoka kwa Mungu, kama wana wa Israeli walivyopewa amri ya kuhukumu na Mungu mwenyewe. Hatuna tena hukumu ya jino kwa jino, jicho kwa jicho, mguu kwa mguu, Wakati huu wa sasa wa agano jipya, Hukumu yote amekabidhiwa Yesu Kristo.

Yohana 5:22 “Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, BALI AMEMPA MWANA HUKUMU YOTE”

Umeona hapo? Mwana (yaani Yesu Kristo) Ndio kakabidhiwa hukumu yote sasa…na ndiye atakayewahukumu walio hai na walio kufa (Kasome 2Timotheo 4:1)…hakuna tena mtu yeyote mwenye mamlaka ya kumuua mwanamke aliyeshikwa katika uzinzi, wala kumuua mtu aliyekamatwa analala na mnyama wala kumuua mwanamke/mwanamume aliyekamatwa katika uchawi. Hukumu hizo Yesu Kristo ndio kakabidhiwa na Baba, na sasa ametupa neema….Ambapo tunamkosea Mungu lakini tuna nafasi ya kutubu kabla ya kuhukumiwa…

Maasi tunayoyafanya sasa tunastahili kuhukumiwa na Bwana Yesu papo kwa hapo!!…lakini tumependelewa na kupewa nafasi ya kukimbilia msalabani na kupata msamaha kabla ya hukumu ya mwisho!…Utafika wakati hii neema itaisha na huyu Yesu Kristo tunayemwona sasa anayeturehemu bure watu tusiostahili kurehemiwa, atafunga mlango wa Neema na atasimama kwenye kiti chake cha hukumu na atawahukumu wazinzi wote, wachawi wote na watenda dhambi wote kwa kuwatupa katika ziwa la moto..Lenye adhabu kali kuliko ya kupigwa kwa mawe.

Hivyo haturuhusiwi kwa namna yoyote kuwaua wezi kwa kuwapiga kwa mawe,wala kuwaua tuliowafumania katika uzinzi wala tuliowakamata katika uchawi, wala kulaani mtu yeyote yule..kwa kuutumia huo mstari wa “usimwache mwanamke mchawi kuishi”..Wasiolielewa Neno ndio wanaoutumia huo mstari kwa kukosa maarifa…lakini mimi na wewe tusikose hayo maarifa…Kwasababu hakuna astahiliye kuhukumu sasa isipokuwa Mwana wa Mungu pekee.

Jukumu letu ni sisi kuomba kwa bidii dhidi ya nguvu zote za giza, kwamba zisiwe na nguvu juu yetu, wala juu ya watu wetu na familia yetu, na vitu vyetu…na kumwomba Mungu awaokoe ndugu zetu waliozama katika nguvu za giza, ambao wanatumika na mamlaka ya giza aidha kwa kujua au kwa kutokujua, kwasababu nao pia ni watu kama sisi wanaohitaji wokovu, na sio kutafuta njama za kuwaua,au kuwaombea vifo ni kinyume na maandiko…

Bwana atubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Nini tofauti kati ya Amri, sheria na Hukumu?

UTUKUFU NA HESHIMA.

Kwanini Bwana aliongea na Abramu baada ya kutengeana na Lutu?

UNATAKA KUBARIKIWA? BASI USIKWEPE GHARAMA ZAKE.

Uasherati wa Kiroho maana yake nini?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
10 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Saimon amoss
Saimon amoss
1 year ago

Amina ubarikiwe mtumish kw mafundisho yako mazur ymenivusha from one stage to another

Pastor Charles Mwaihojo
Pastor Charles Mwaihojo
1 year ago

ubarikiwe mtumishi kwa mtazamo wako, umewasaidia wengi lakini KWA MIMI SITAMWACHA AISHI,nadhani tafsri na muongozo tu wa roho mtakatifu ni bora zaidi,. Kwa wale waliovitani dhini ya wachawi watanielewa. sasa Kwa nini usimwache mchawi aishi? Zipo sababu kadhaa lakini lililo la msingi ni kwamba kila mtu aitwaye mchawi ni wakala wa Shetani asilimia 100. Kwa kuwa hakuna mchawi asiyefanya mapatano ya kima-agano na kuzimu (ufalme wa giza); kwa ridhaa yake mwenyewe.
….,”Tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu;”… { ISAYA 28:15 }
“Naam, walitoa wana wao na binti zao Kuwa dhabihu kwa mashetani.
Wakamwaga damu isiyo na hatia, Damu ya wana wao na binti zao,”….{ ZABURI 106: 37-38a}
”ADUI YANGU KUFA BADALA YANGU”

Victoria Msigwa
Victoria Msigwa
1 year ago

Nashukuru sana nimefumbuliwa macho ya rohoni maana maombi ya kuwaua wachawi yameshika Kasi katika nyumba za ibada kumbe tunakosea sana

George
George
2 years ago

Asante sana nimebarikiwa kwa somo hili

Emmanuel Kitengule
Emmanuel Kitengule
2 years ago

Asante sana kwa somo hili limenifungua, katika kanisa nililokuwa naabudu kulikuwa na kuua wachawi katika maombi kwa kutumia hili andiko kumbe sio sahihi.Sasa nimeelewa.

Ibrahim gurth
Ibrahim gurth
2 years ago

Nimebarikiwa mtakuwa mnanitumia I

Gideon Kwalazi
Gideon Kwalazi
3 years ago

NIMEBARIKIWA!!