BWANA AKAMWAMBIA SHETANI, BWANA NA AKUKEMEE EWE SHETANI;

BWANA AKAMWAMBIA SHETANI, BWANA NA AKUKEMEE EWE SHETANI;

Shalom jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tujifunze biblia.

Tunaweza kujiuliza maswali mengine ni kwanini mara nyingi malaika walipokuwa wakishindana na shetani, hawakutumia uweza wao wote kupambana naye,bali walimwachia Mungu aamue, japokuwa walikuwa na mamlaka na uwezo wa kufanya lolote juu yake..

Tunaweza kuona baadhi ya maeneo katika biblia, kwamfano kama lile tukio la Yoshua kuhani mkuu alipokuwa anahudumiwa na Yule malaika, na shetani naye akiwa pembezoni mwao kulipinga kusudi la Mungu..Utaona pale yule malaika hakutoa maneno ya kulaani , japokuwa ibilisi ni mlaaniwa sikuzote..bali alisema..

Zekaria 3:1 “Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye.

2 Bwana akamwambia Shetani, Bwana na akukemee Ewe Shetani; naam, Bwana, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je! Hiki si kinga kilichotolewa motoni”?

Unaona? Sehemu nyingine tena ni pale Mikaeli alipopewa jukumu la kuuhifadhi mwili wa Musa, lakini shetani akatokea ghafla ili kushindana naye lakini utaona hakudiriki, kumtamkia hukumu palepale, japokuwa tayari ibilisi ni mlaaniwa, badala yake alimkabidhi Mungu hukumu yote..

Yuda 1:9 “Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee’.

Kama hilo halitoshi, malaika watakatifu bado, wanapotuona tunafanya mambo yasiyompendeza Mungu, wanaporudisha ripoti mbinguni juu ya mienendo yetu duniani, wanapofika mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, hawatupelekei yale mashitaka mabaya kwa Mungu, wanajaribu kuyasitiri kwa kadiri wawezavyo, Uone jinsi wanavyoogopa hata kutoa neno la laana kwa kiumbe chochote cha Mungu kiwe ni kizuri au kibaya..

2Petro 2:11 “Wenye ushupavu, wenye kujikinai, hawatetemeki wakiyatukana matukufu; IJAPOKUWA MALAIKA AMBAO NI WAKUU ZAIDI KWA UWEZO NA NGUVU, HAWALETI MASHITAKA MABAYA JUU YAO MBELE ZA BWANA.

12 Lakini hao kama wanyama wasio na akili, ambao walizaliwa kama wanyama tu wa kukamatwa na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao”

Hiyo ni kutufundisha na sisi pia tunavyopaswa tuchukuliane na maadui zetu mbele za MUNGU, Pale wanaposhindana na sisi, Je na sisi tushindane nao kwa kuwalaani au kuwalaumu?..Pale unaposikia umesengenywa kidogo je na wewe uende kuwaombea mabaya mbele za Mungu, wapigwe? Je! wewe ni mtu wa kupeleka mashitaka tu kila siku zote mbele za Mungu..Huna lingine..?

Wapigwe, waangushwe, warudishwe nyuma, wafedheheshwe, ni hayo tu ndio tunayoweza kumwambia Mungu kwenye maombi yetu ya kila siku?, Hatuna Muda wa kumuomba Mungu ufalme wake uje juu ya roho zetu kama Bwana alivyotufundisha, sisi ni kushindana na maadui zetu ?

Yuda 1:9 “Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee.

10 Lakini watu hawa huyatukana mambo wasiyoyajua, na mambo wayatambuayo kwa asili wajiharibu kwayo kama wanyama wasio na akili.

11 Ole wao! Kwa sababu walikwenda katika njia ya Kaini, na kulifuata kosa la Balaamu pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika maasi ya Kora”.

Kaka/Dada watu watakaokwenda kinyume na wewe watakuwepo tu daima kutupinga, lakini sisi tumwachie hayo Mungu ayashughulikie kama wafanyavyo malaika, tuendelee na kusudi lililotuleta hapa duniani la kumtafuta Mungu na hiyo ndio ishara nzuri ya unyenyekevu tunayopaswa tuige kwa malaika watakatifu dhidi ya maadui zetu (wanadamu).

Mithali 24:17 “Usifurahi, adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo;

18 Bwana asije akaliona hilo, likamkasirisha; Akageuzia mbali naye hasira yake”.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

MAPAMBANO DHIDI YA SHETANI.

Ni uthibitisho upi unaoonyesha kuwa kuna MBINGUNI na KUZIMU?

FAHAMU TAFSIRI ZA NDOTO MBALIMBALI.

WANA WA MUNGU, NA BINTI ZA WANADAMU.

HISTORIA YA WILLIAM BRANHAM

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments