MAPAMBANO DHIDI YA SHETANI.

MAPAMBANO DHIDI YA SHETANI.

Mapambano dhidi ya shetani.

Katika vita siku zote wanaopambana ni wanajeshi dhidi ya wanajeshi..na si raia dhidi ya wanajeshi…Na ndio maana vita huwa vinakuwa ni vigumu sana na vikali…hiyo yote ni kwasababu mwanajeshi anafundishwa kwenda kupambana na mwanajeshi mwenzake ambaye anautaalamu kama yeye, ambaye ni mjuzi wa silaha kama yeye, ambaye anavaa dirii ya kuzuia risasi kifuani kama yeye anavyovaa..ambaye anavaa chepeo kichwani ambayo ni ngumu isiyoweza kuingia risasi kama yeye anavyovaa…ambaye anasilaha na vifaa vya kijeshi kama vya kwake…

Ndio maana unaweza kuona Taifa moja linajiongezea uwezo wa silaha za kijeshi kila kukicha ni kwanini?….Ni kwasababu wanajeshi wanapokwenda vitani wanakwenda kupambana na watu wanaotumia vifaru kama wao…wanakwenda kupambana na watu wenye ujuzi kama wao…Kwa ufupi wanakwenda kupambana na watu wanaofanana na wao karibia kila kitu..na hawaendi kupambana na raia.

Na wakishafanikiwa kumaliza jeshi la maadui basi huwa hawana muda ya kuwaua raia,.. wanachokifanya ni kuchukua tu rasilimali zao, na kuwachukua raia mateka au kuwafanya watumwa wao basii…hawana muda wa kuwaua…kwasababu vile vifaru walivyokuwa wanavitumia vitani havikuwa kwaajili yao bali kwaajili ya wanajeshi wao…

Sasa na sisi wakristo tunafananishwa na wanajeshi waendao vitani…na Biblia inatuambia “Tutwae silaha zote za Mungu”

Waefeso 6:11  “Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani

12  Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.

14  Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,

15  na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;

16  zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.

17  Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;

18  kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;”

Kumbuka na sisi hatuendi kupigana na watu wa shetani…bali tunakwenda kupambana na Adui yetu Shetani mwenyewe na mapepo yake. Na kama sisi tulivyo ndivyo na yeye alivyo…kama na sisi tulivyo na upanga mkononi na yeye anao upanga mkononi..kama sisi tulivyo na ngao na yeye pia anayo ngao ya kuzuia mishale kutoka kwetu..kama sisi tulivyo na chepeo kichwani mwetu na yeye ni hivyo hivyo anayo ya kwake…Kwahiyo hapo vita ni lazima viwe vikali tu..kinachohitajika ni kuwa na uwezo wa kuutumia upanga kuliko yeye, kuwa na uwezo wa kuitumia ngao kuliko anavyoitumia yeye, kuwa na uwezo wa kutumia chepeo kuliko anavyoitumia yeye..hiyo ndio njia tu ya kumshinda Adui shetani. Lakini kama yeye anauwezo mkubwa wa kutumia silaha zake kuliko wewe basi atakushinda tu, haijalishi una upanga mkononi, au ngao au chepeo….

Sasa Kwanini tunashika upanga wa Roho mkononi ambao ni Neno la Mungu?..Ni kwasababu Adui yetu na yeye ameshika upanga mkononi…kutupinga sisi…Ndugu usifikiri shetani halijui Neno?…. Analifahamu vizuri sana..na kama biblia inavyosema Neno la Mungu ni upanga ukatao kuwili…maana yake adui akiupata anaweza kuutumia kukuua hata wewe…Hivyo shetani naye ameshikilia upanga wa Neno la Mungu akipambana dhidi yetu…

Kama alivyopambana na Bwana Yesu akiwa kule jangwani…alimwambia Bwana Yesu “imeandikwa hivi katika maandiko”…Na Bwana akawa anamjibu “tena imeandikwa hivi”..Katika ulimwengu wa roho hapo ni pambano kati ya Bwana Yesu na shetani…shetani anaurusha upanga dhidi ya Bwana na Bwana anauzuia na kwa ushapu anamkata na upanga wake ulio mkononi..

Lakini endapo Bwana angekuwa halijui Neno..shetani angemkata kwa Neno hilo hilo..Lakini kwasababu alikuwa analijua kulitumia Neno vizuri aliweza kumshinda shetani..

Kwahiyo ukienda kupambana na Adui shetani na mapepo yake..kama hulijui neno na namna ya kulitumia ipasavyo hakika atakumaliza, kwasababu na yeye kaushikilia upanga unaofanana na wako….(Mapambano dhidi ya shetani  yatakuwa makali sana kwako)

Katika siku hizi za mwisho biblia imetabiri kuwa upendo wa wengi utapoa…Upendo unaozungumziwa hapo ni upendo wa kumpenda Mungu…na si wa kumpenda mwanamke/mwanamume. Watu wengi watakuwa hawana habari ya Neno la Mungu. Leo utamwuliza mtu mara ya mwisho kujifunza mwenyewe binafsi biblia ni lini? Bila kusubiri kutafsiriwa na mtumishi Fulani?..atakuambia ni muda mrefu sana..na hata akisoma, anasoma sura moja mbili kamaliza…Nyakati hizi mbaya tulizopo sio nyakati za kusoma sura moja ya biblia na kutulia baada ya wiki ndio unasoma nyingine…hapo shetani hashindani na wewe anakuona tu kama raia ambaye huna madhara kwake hivyo anakuchukua mateka tu, kama wanajeshi wanavyowachukua raia mateka..

Sasa siku hizi za mwisho, shetani kashawachukua wengi mateka…inawezekana hata wewe umeshachukuliwa lakini hujijui tu, (kwasababu huna silaha yoyote mkononi mwako ya kumwogopesha)…sasa choropoka leo anza kuzifaa silaha chini chini kwa kuanza kujifunza Neno, na baadaye utoke upambane naye ili ukiisha mshinda uwafungue mateka wale wote aliokuwa amewateka kwa uongo wake na kuwafanya kuwa mateka yake kwa uongo wake… wewe wageuze wawe mateko wa Kristo wote aliowateka yeye, kwa elimu yako ya uongo na tabu zake… Kama biblia inavyotuambia..

2 Wakorintho 10:3  “Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;

4  (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)

5  tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; NA TUKITEKA NYARA KILA FIKIRA IPATE KUMTII KRISTO;

6  tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia”

Na silaha hiyo ni NENO LA MUNGU..Ukilifahamu Neno la Mungu, Bwana atakutumia kumnyang’anya shetani mateka…na yeye atabaki hana kitu..na jeshi la Bwana litakuwa kubwa zaidi kuliko lake.

Sasa utawezaje kuanza kujivika silaha hizo.?

Kwanza tubu, mpe Yesu Kristo maisha yako kama hujaokoka..kisha jikane nafsi na beba msalaba wako..Halafu anza kupunguza mizigo katika maisha yako ya kila siku, ondoka kwenye magroup yote ya kidunia katika mitandao, Kanunue biblia leo kama huna… “Biblia ya maandishi sio ya kwenye simu”,..kila siku tenga muda mrefu wa kusoma Neno, na unaposoma zima simu na pia kaa sehemu ya utulivu..kisha yasome maandiko na utaona mambo Bwana atakayokufunulia ambayo ulikuwa huyajui…usisome kimstari kimoja au sura moja…Soma angalau kitabu kizima…kwasababu ufunuo wa Roho unaachiliwa pale unapolielewa Neno katika msingi wake, lakini ukisoma kijimstari kimoja hutaelewa chochote na hutapata ufunuo wowote. Soma kitabu cha Injili ya Mathayo uone ni vitu vingapi ulikuwa huvijui na jinsi gani likuwa vinakupita tu na shetani alivyokuwa anakudanganya.

Wakolosai 3: 16 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote..”

Na siku zote kumbuka, mapambano dhidi ya shetani hayajaisha.

Bwana akubariki.

Tafadhali share na wengine, na pia kama utapenda kuyapata masomo haya kwa njia ya whatsapp au email au inbox yako ya facebook basi utatutumia ujumbe mfupi, hali kadhalika unaweza kuyapata bure kwa njia ya internet, tembelea website yetu hii kwa masomo Zaidi /www wingulamashahidi org/.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

JILINDE NA UNAJISI, UNA MADHARA MAKUBWA.

Kwanini kila nikitaka kusali naingiwa na uvivu?

NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE

RABI, UNAKAA WAPI?

Shetani ni nani?

KWA VILE ALIVYOKUWA MTU WA HAKI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Temwan
Temwan
5 days ago

Mungu awabariki sana