FAHAMU TAFSIRI ZA NDOTO MBALIMBALI.

FAHAMU TAFSIRI ZA NDOTO MBALIMBALI.

Ndoto ni eneo ambalo watu wengi wanadanganywa na kupotoshwa Na hiyo yote ni kutokana na kukosa maarifa ya kutosha. Wapo watu wengi mitandaoni, wanaowaeleza watu tafsiri za ndoto mbalimbali zao na mwisho wanaambatanisha na dawa zao za kibishara wakiwadanganya watu kuwa hizo zitaleta suluhisho la matatizo yao.

Wengi wa hao watu kama si wafanyabiashara basi ni waganga wa kienyeji na hawana lolote la kukusaidia zaidi ya kukuongezea matatizo. Kumbuka Ndoto si tatizo la kimwili hivyo hakuna tiba yoyote ya kimwili kama vile dawa ya kunywa au ya kumeza itakayoweza kuleta suluhisho la ndoto zako.

Kwa ufupi Zipo ndoto za aina tatu, 

  1. Zinazotokana na Mungu:
  2. Zinazotokana na shetani
  3. Zinazotokana na mtu mwenyewe.

Ndoto zinazotokana na Mungu zinachukua sehemu ndogo sana ya ndoto zote mtu anazoota kila siku naweza kusema hata asilimia 5 tu ya ndoto zote ulizowahi kuota,..

Vivyo hivyo na za shetani nazo hazina asilimia kubwa ya ndoto unazoziota mara kwa mara.

Lakini ndoto zinazotokana na mtu mwenyewe hizi ndizo zinazochukua sehemu kubwa ya ulimwengu wa ndoto za wanadamu. Na hapa ndipo watu wengi wanapokosa shabaha, wakidhani kila ndoto tu wanayoita ni lazima iwe na tafsiri, au ni lazima iwe imebeba ujumbe maalum.

Sasa hizo aina mbili za kwanza, (yaani ndoto za Mungu, na za Shetani) huwa zinabeba maana kubwa sana rohoni, ili kufahamu jinsi ya kuweza kuzitambua aina hizi za ndoto  fungua hapa..>>> Tofauti kati ya ndoto za Mungu na Shetani

Leo hii nitajikita kuorodheshea baadhi ya ndoto ambazo watu wengi wanaota na hawajui nyingi kati ya hizo zinatokana na mwili wenyewe..

Ukiota Hizi  uzipuuzie, wala usihangaike kutafuta maana zake, kwasabu hizi huwa zinakuja aidha kutokana na shughuli nyingi..

  • Kwamfano wewe ni mkulima, hivyo kila siku kuota upo shambani unalima, au unaota pembejeo au mazao, hilo ni jambo la kawaida…

Soma..

Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi;..”

  • Au kama akili yako muda wako wote kutwa kuchwa ilikuwa unafikiria masomo tu, basi jua kuota unafanya mitihani litakuwa  ni jambo la kawaida,
  • Vilevile ndoto za namna hii zinakuja kutokana na mabadiliko ya mwili. Kama ulilala una njaa, basi tarajia usiku kuota unakula kula hushibi, kama ulikunywa maji mengi na hivyo kibofu kimejaa, tarajia usiku kuota unakojoa kojoa mkojo hauishi, n.k.

Isaya 29: 8  “Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni”.

Hivyo watu wengi wanaota ndoto nyingi za namna hiyo, na nyingine ubongo unazitengeneza wenyewe. Kwamfano utakuta mtu anatafuta kufahamu Tafsiri za ndoto mbalimbali kama hizi:

  1. Kunyonyesha mtoto: Wanaoota ndoto hizi asilimia kuwa ni wanawake, kwasababu wao ndio akili yao sehemu kubwa ilishajengeka katika mazingira ya kuwa na Watoto hata kama hajazaa..Hivyo kuota unaonyenyesha haliwezi kuwa ni jambo la ajabu
  2. Vivyo hivyo kuota mbwa:
  3. kuota  panya,
  4. Wengine wanatafuta kujua ndoto za magari zinamaanisha nini: Magari tunakutana nayo kila siku barabarani.
  5. ukiota unaswali, .
  6. Maana ya ndoto nyevu,
  7. kuota una nywele ndefu,
  8. ndoto ya kufua nguo,
  9. tafsiri ya ndoto ya harusi.
  10. kuota unavua samaki, na za  kuogelea,
  11. Kuota umegeuza nguo
  12. Ndoto za kuogelea
  13. Kuota ajali
  14. Kuota umeua mtu
  15. Kuota upinde wa mvua
  16. Ndoto za meli
  17. Kuota unanyeshewa na mvua
  18. Maana ya ndoto za kuolewa
  19. Unachuma matunda
  20. Unakunywa pombe
  21. Umevaa nguo nyeupe, 
  22. Ndoto za mayai
  23. Ndoto ya Nyama
  24. Ndoto za asubuhi
  25. Kuota unaoga
  26. Kuota Wanyama, kama mbuzi, sungura, kinyonga, kobe, ngamia, tembo, mamba, kiboko, nyani,paka, mbwa, ng’ombe.N.k. Zote hizi zipuuzie tu.Hazina maana yoyote kwako.
  27. Kuota wadudu kama sisimizi, siafu, konokono, mchwa, mbu, nge, mjusi, mende,tandu
  28. Kuota mapacha.
  29. Kuota jirani, ndugu yako,
  30. Kuota unakula mkaa.
  31. Kuota unatapika.
  32. Watu wanavuna.
  33. Ndoto za kutembea peku.
  34. Unafagia, Unalia,
  35. Kumuota raisi, waziri mkuu, makamu wa raisi, mbunge. Hawa kila siku unawaona kwenye Tv, au unawasikia kwenye Radio, ni lazima utawaota tu usiku siku moja.
  36. Ndoto Juu ya mpenzi wako.
  37. Kuota kabati.
  38. Unafua nguo,
  39. Unaosha vyombo, Maiti,
  40. Kuota jeneza
  41. Ukiota karanga, vitunguu, nyanya, pilau, sherehe,
  42. Kuota Unauza duka

Nakadhilika, Nakadhalika..zipo nyingi, nyingine unazijua wewe mwenyewe, hatuwezi kuziorodhesha zote hapa.. Lakini zote hizo hazina umuhimu wa kutafuta kujua maana zake. Kwasababu ukienda kwa mtindo huo utachanganyikiwa mwilini na rohoni.

Kikubwa ni kufahamu kuwa njia Kuu  ambayo Mungu aliichagua kuzungumza na wanadamu ni kupitia Neno lake (Biblia tu)

Ikiwa wewe ni mwenye dhambi nataka nikuambie hizi ni nyakati za mwisho, Mafundisho mengi ya uongo, na ya mashetani yamezaa kila mahali, Usipotaka kusimama, shetani ni lazima akuzombe kwenye aina ya mafundisho hayo ya mashetani na kukupa tafsiri ya kila ndoto unayoita….

Tubu mgeukie Mungu wako, dalili zote zinathibitisha hilo kuwa tunaishi katika siku za mwisho. Maisha yako yapo hatarini sana, kwani hujui siku yako ya kuondoka ni lini, na hata kama hutaondoka leo au kesho, lakini UNYAKUO upo karibuni sana.. Yesu yupo mlangoni kuja kuwachukua wateule wake.

Angalia hali halisi ya ulimwengu ulivyo sasa halafu niambie ni dalili ipo Yesu aliyosema kuhusu siku za mwisho haijatimia, angalia magonjwa ya mlipuko, angalia tetesi za vita, angalia matetemeko, angalia kuongozeka kwa maasi duniani,..yote hayo yalitabiriwa.

Huu si wakati wa kuangalia mambo mengine Zaidi ya wokovu wako. Nani ajuaye leo hii Mungu kakupitisha kwenye ukurasa huu ni ili Akuokoe? Kwasababu anaompango mkubwa na wewe maishani mwako?

Hivyo kama wewe ni mwislamu usiogope kumkabidhi YESU Maisha yako leo, fungua tu moyo wako mruhusu atende kazi, nawe utaona badiliko la ajabu atakalolileta ndani yako.

Ikiwa upo tayari kufanya hivyo basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU  MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, . NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Ubarikiwe sana.

Bofya chini kwa kujiunga na magroup yetu ya Whatsapp, kwa  mafundisho ya kila siku.

Mada nyinginezo:

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..

CHUKIZO LA UHARIBIFU

UNYAKUO.

MIJI YA MAKIMBILIO.

WAKATI ULIOKUBALIKA NDIO SASA.

MAHALI UNAPOPASWA USIMVUMILIE SHETANI HATA KIDOGO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
2 years ago

Naomba nitafsirie ndo hii kuota unakunywa pombe

Axe
Axe
3 years ago

Allah anaouwezo wa kutenda yote hayo infact same God haina haja ya kubadili Imani ni kumuomba tu

Shida mashauri
Shida mashauri
2 years ago
Reply to  Axe

Mtumishi wa mungu niombeee mwaka huu niweze kujiliwa na serikali Kwa hizi ajira za afya zilizotoka mwezi huu. Bwana yesu asifiwe