WAKATI ULIOKUBALIKA NDIO SASA.

WAKATI ULIOKUBALIKA NDIO SASA.

Biblia inasema kila jambo na majira yake (Mhubiri 3)…maana yake ni kwamba hata mti una majira yake ya kuzaa matunda…sio kila wakati, tutakwenda kukuta maembe katika mti wa muembe…Inahitajika uwe ni msimu wa maembe ndipo mti uzae…Haijalishi huo mti utaumwagilia maji kiasi gani, au utauwekea mbolea kiasi gani…Kama sio msimu wake wa kuzaa hautazaa….Hiyo yote ni kwasababu gani?..Ni kwasababu kila jambo lina majira yake.

Vivyo hivyo katika roho, tangu Bwana wetu Mkuu Yesu Kristo, apae juu mbinguni kwenda kutuandalia makao..majira yalibadilika…kabla ya hapo hakukuwa na mlango wowote wa sisi kumzalia Mungu matunda anayoyataka…ikiwa na maana waliokuwa na fursa ya kumjua Mungu kwa undani na kunufaika sana walikuwa ni manabii wa Mungu wachache waliochaguliwa..na si watu wote, Roho Mtakatifu alikuwa anashuka juu ya watu wa Mungu wachache aliowachagua…kasome vizuri habari ile ya Musa katika..

Hesabu 11:24 “Musa akatoka, akawaambia watu maneno ya Bwana; akawakutanisha watu sabini miongoni mwa wazee wa watu, akawaweka kuizunguka Hema.

25 Ndipo Bwana akashuka ndani ya wingu, akanena naye, akatwaa sehemu ya roho iliyokuwa juu ya Musa, akaitia juu ya wale wazee sabini; ikawa, roho hiyo ilipowashukia, wakatabiri, lakini hawakufanya hivyo tena.

26 Lakini watu wawili walisalia kambini, jina la mmoja aliitwa Eldadi, na jina la wa pili aliitwa Medadi; na roho ile ikawashukia; nao walikuwa miongoni mwao walioandikwa, lakini walikuwa hawakutoka kwenda hemani; nao wakatabiri kambini.

27 Mtu mmoja kijana akapiga mbio, akaenda akamwambia Musa, akasema, Eldadi na Medadi wanatoa unabii kambini.

28 Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa tangu ujana wake, akajibu akasema, Ee bwana wangu Musa, uwakataze.

29 Musa akamwambia, Je! Umekuwa na wivu kwa ajili yangu; INGEKUWA HERI KAMA WATU WOTE WA BWANA WANGEKUWA MANABII NA KAMA BWANA ANGEWATIA ROHO YAKE.

30 Kisha Musa akaenda akaingia kambini, yeye na wale wazee wa Israeli”.

Umeona hapo mstari wa 29?.. Musa anasema ingekuwa heri kama watu wote wa Bwana, Bwana angewatia roho yake…Ikiwa na maana kuwa ni wachache tu waliochaguliwa kwa Neema ndio waliokuwa wananufaika na kipawa cha Roho Mtakatifu. Wengine wote walitamani lakini hawakukipata. Kwanini?..ni kwasababu haukuwa wakati wala majira ya kitu hicho, kushuka kwa watu wote.

Lakini Bwana Mungu wetu, ambaye ni alitabiri kwamba utafika wakati Roho huyu atamwagwa kwa wote wenye mwili…huo utakuwa ni msimu wa kuzaa matunda…Kwahiyo watakaozaliwa msimu huo watakuwa na bahati sana..Na wakati huo si mwingine zaidi ya tangu ule wakati Bwana wetu alipopaa mbinguni mpaka wakati huu wa sasa tunaouishi sisi.. Bwana alisema…

Yoeli 2:27 “Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe.

28 Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono”

Hii ni neema ya ajabu sana, ambayo hatupaswi tuipuuzie…Huu ndio wakati uliokubalika wa Bwana kutumwagia kipawa chake cha Roho Mtakatifu pasipo ubaguzi…Ndio maana biblia inasema katika…

2Wakorintho 6:1 “Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure.

2 (Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati ULIOKUBALIKA NDIYO SASA; tazama siku ya wokovu ni sasa)”

Ndugu huu ndio wakati uliokubalika…biblia inasema watu wa zamani walikitamani hichi kipindi tunachoishi sisi…wafalme walikitamani, wakuu walitamani waonje kipawa cha Roho Mtakatifu, waliomba na kusubiri, lakini walikufa bila kuifikia hii saa tuliyopo sasa..Lakini sisi ndio tupo hiyo saa, ambayo yule Roho aliyeshuka juu ya Musa, ndiye huyo huyo ambaye tunamiminiwa sisi wengine ambao hata hatustahili…Ni neema ya namna gani?..Tukose kila kitu lakini tusimkose Roho Mtakatifu kwasababu huyo ndiye Muhuri wa Mungu (Waefeso 4:30)..

Je umempokea huyu Roho Mtakatifu?..kama bado fahamu kuwa anapatikana bure kwa yeyote ambaye atamuhitaji, lakini hatumuhitaji kwa mdomo bali kwa vitendo..maana yake ni hii: Ili ashuke juu yako ni lazima utubu kwa kumaanisha kuacha dhambi kweli kweli…kwasababu yeye ni Roho Takatifu ya Mungu, na hivyo haichangamani na uchafu wa aina yoyote,

kwahiyo unatubu kwa dhati kabisa na kwa vitendo..kama ulikuwa unaiba unaacha wizi na kuwarudishia uliowaibia mali zao kama bado unazimiliki, kama ulikuwa unajiuza, unaacha na kufuta namba za wote uliokuwa unajishughulisha nao katika kazi hiyo, kama ulikuwa unafanya uchafu wowote ule kama kujichua, unatazama picha chafu, ulikuwa mfiraji, msagaji, mlaji rushwa, muuaji n.k unaviacha vyote hivyo…kisha unakwenda kwa Yesu, na kumwomba rehema…Na Bwana wetu mwenye huruma akiona umegeuka kwa vitendo namna hiyo…tayari Yule Roho wake Mtakatifu atakuwa ameshakukaribia sana, utaanza kuona ni kama vile ulikuwa unatembea na kuchoka na ghafla nguvu mpya imekuingia…

Na kukamilisha muhuri huo wa Roho Mtakatifu ndani yako, nenda katafute ubatizo sahihi haraka sana, na ubatizo sahihi kulingana na maandiko ni ule wa maji mengi na kwa jina la BWANA YESU KRISTO…Kumbuka jina la Bwana Yesu ndio Jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu…Hakuna jina lingine tulilopewa sisi wanadamu litupasalo kuokolewa kwalo isipokuwa jina la Yesu.

Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.

40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi”.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

MWAKA WA BWANA ULIOKUBALIWA.

USIMWOGOPE YEZEBELI.

NGUVU ILIYOPO KATIKA MAAMUZI.

FUKUZA TAI WOTE JUU YA SADAKA YAKO.

JIRANI YANGU NI NANI?

KILA KIUNGO LAZIMA KISHUGHULIKE.

MPINGA-KRISTO

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments