MAHALI UNAPOPASWA USIMVUMILIE SHETANI HATA KIDOGO.

MAHALI UNAPOPASWA USIMVUMILIE SHETANI HATA KIDOGO.

Katika injili utaona zipo sehemu kuu mbili ambazo Bwana alimfukuza shetani waziwazi.. sehemu ya kwanza ni pale shetani alipotaka amsujudie kwa mapatano kuwa atampa milki zote za ulimwengu.Na sehemu ya pili ni pale Shetani alipomfariji kuwa hatapitia mabaya yaliyo mbele yake..

Tusome..

Mathayo 4:8 “Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,

9 akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.

10 Ndipo Yesu alipomwambia, NENDA ZAKO, SHETANI; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake”.

Na mahali pengine ni..

Mathayo 16:21 “Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.

22 Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata.

23 Akageuka, akamwambia Petro, NENDA NYUMA YANGU, SHETANI; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu”.

Bwana aliona ipo mipaka ambayo mtu yeyote au kiumbe chochote hakipaswi kuvuka, Na kwamba yeyote atakayejaribu kufanya hivyo si tu kukemewa bali ni kufukuzwa kabisa.. Na shetani alifukuzwa na Bwana katika vitu hivi viwili..Kwanza ni pale alipotaka asujudiwe hilo tayari lilikuwa ni kosa kubwa machoni pa Bwana haijalishi ni ahadi ngapi nzuri zilifuata mbele yake..

Leo hii watu wengi wapo tayari, kumwabudu shetani kisa mali, wapo tayari kubadili imani kisa wanawake/wanaume, wapo tayari kula rushwa kisa wanaahidiwa pesa nzuri, wapo tayari kuua na kutoa kafara ili wawe matajiri, wapo tayari kujiuza ili wapate kipato, wapo tayari kupiga ramli wawaridhishe wazee wa ukoo, wapo tayari kufanya lolote lile haijalishi ni kinyume na mapenzi ya Mungu kiasi gani ili wapate faida Fulani au unafuu Fulani..

Ndugu hatua kama hiyo ukifikia ikiwa wewe ni mkristo Usimwangalie shetani mara mbili, usimvumilie shetani hata kidogo!, mfukuze kwa kishindo chote, haijalishi leo hii unapitia katika hali ngumu kiasi gani..Kumbuka hata wakati shetani anamletea Kristo majaribu kama haya ya kuahidiwa ulimwengu mzima na milki zote, alikuwa katika hali ya njaa, hajala siku 40, hana kibanda, wala biashara wala nini..Lakini alimwambia ondoka, hapa, kwa namna nyingine tunaweza kusema nisikuone eneo hili tena.

Sehemu nyingine ambayo unapaswa usimvumilie shetani ni pale, Mungu anapokuonyesha mafanikio Fulani makubwa mbeleni lakini sharti kwanza upitie mateso Fulani au dhiki Fulani kabla ya kuyapata, lakini shetani anatokea na kukwambia usihofu hutapitia..Hapo hupaswi kusikiliza, ni kumfukuza tu..

Embu jaribu kufiria mfano Bwana angeyasikiliza yale maneno ya shetani yaliyokuwa ndani ya kinywa cha Petro, mambo yangekuwaje leo hii? ni wazi kuwa hadi leo hii mimi na wewe tusingepata neema ya wokovu, kwasababu Kristo asingesulibiwa..Damu isingepatikana kwa ajili ya ondoleo la dhambi zetu… Lakini aliona wimbi kubwa la wanadamu linakwenda kuokolewa na ibilisi hataki hilo litendeke..akajaribu kumbunia njia za kulikwepa.

Hata Mtume Paulo, kuna wakati alijua kabisa kuwa vifungo na dhiki vinamngoja huko mbeleni, lakini hakukubali kukatishwa tamaa na watu, kwamba abaki asiende Yerusalemu. Watu wanadhani Roho Mtakatifu kumwambia Paulo vile, ilikuwa ni kumzuia asiende hapana, bali alikuwa anampa taarifa ya mambo yatakayomkuta huko mbeleni, kwasababu ni kawaida ya Mungu kuwapata watu wake taarifa kabla mabaya hayajawakuta.. Lakini Ni wale watu waliokuwa naye ndio waliomwambia asiende, lakini yeye hakukubali, akawaambia..

Matendo 21:12 “Basi tuliposikia haya, sisi na watu wa mahali pale, tukamsihi asipande kwenda Yerusalemu.

13 Ndipo Paulo alipojibu, Mnafanya nini, kulia na kunivunja moyo? Kwa maana mimi, licha ya kufungwa, ni tayari hata kuuawa katika Yerusalemu kwa ajili ya jina lake Bwana Yesu”.

Alifanya hivyo kwasababu aliona wingi wa matunda atakayoyaleta kwa Mungu ni mengi akifananishwa na dhiki fupi za kitambo, zitakazoletwa na shetani.

Hivyo na sisi wakristo, tusiruhusu mambo hayo mawili shetani ayalete mbele yetu..kwanza tusiruhusu tamaa za ulimwengu kutufarakanisa na Mungu wetu, Pia tusiruhusu dhiki za kitambo zikatukosesha Baraka Mungu alizotuchumia huko mbeleni…

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

KUTAHIRIWA KIBIBLIA

VICHEKESHO NA UTANI MADHABAHUNI

JE KUHUDUMU KWA NYIMBO ZA INJILI KUKOJE?

Je kuweka mapambo kama mikufu, vikuku na kutoboa pua ni dhambi?

JINSI SODOMA NA GOMORA ILIVYOKUWA INAVUTIA SANA..

KWANINI UBATIZO NI WA MUHIMU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Joshua kaluya
Joshua kaluya
2 years ago

Amen