Ayubu alimaanisha nini kusema ‘nami nitarudi tena huko uchi vilevile;?

Ayubu alimaanisha nini kusema ‘nami nitarudi tena huko uchi vilevile;?

SWALI: Ayubu alimaanisha nini kusema..Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; Aliwezaje kurudi tena tumboni mwa mama yake tena uchi je hilo jambo linawezekana?


JIBU: Kauli hiyo aliisema Ayubu baada ya kupotelewa na familia yake na mali zake. Lakini Kwa ujasiri akamtukuza Mungu katika hali hiyo pia, kwa kusema maneno hayo; 

Ayubu 1:21

[21]akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe. 

Lakini swali lipo hapo, katika kurudi tumboni mwa mama yake uchi. maana yake ni nini?

Ikumbukwe kuwa sisi hatukutoka tu  katika tumbo la wanamke bali pia katika tumbo la ardhi, hiyo ndio mama wa ulimwengu. yaani mama wetu wa kwanza.

soma; 

Zaburi 139:15

[15]Mifupa yangu haikusitirika kwako, 

Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi; 

Mhubiri 12:7

[7]Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, 

Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa. 

Hivyo Ayubu aliposema nami nitarudi tena huko huko hakumaanisha mama yake mzazi, bali mama wa ulimwengu wote yaani ardhi.

Na ndivyo ilivyo kwa kila mmoja wetu, hukuja na kitu, utaondoka bila kitu chochote. Ukiwa uchi vilevile.

lakini jambo lingine la kufahamu kuwa, wale walio ndani ya Kristo, wafikapo kule ng’ambo hawataonekana uchi, bali watapewa vazi jipya la rohoni la Kristo Yesu, ndio ile miili mipya ya utukufu isiyoona uharibifu idumuyo milele.

2 Wakorintho 5:1-3

[1]Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni. 

[2]Maana katika nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni; 

[3]ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi. 

Swali ni je! Umeandaliwa vazi lako baada ya kuondoka?

Kumbuka unalipokea kwa kumwamini Yesu Kristo leo, okoka tubu dhambi zako, ubatizwe, kisha upokee kipawa cha Roho Mtakatifu. vazi lako liwe limekamilika., ili siku ile usionekane uchi.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.

SIFA ZA MAMBA YULE MKUBWA WA AYUBU.

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA MFUNGO.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
john
john
18 days ago

ubarikiwe