CHAGUA UPANDE WA UZIMA.

CHAGUA UPANDE WA UZIMA.

Kama ukichunguza kwa makini, utaona Mungu kaumba kila kitu katika sehemu kuu mbili…Kwamfano utaona mtu katengenezwa kwa vipande viwili, kushoto na kulia, na vipande hivyo vinafanana..kila kimoja ni taswira ya mwenzake….Mkono wa kushoto unafanana na mkono wa kulia..lakini kimaumbile upo kinyume na mwenzake kadhalika mguu wa kushoto kimaumbile ni kinyume cha mguu wa kulia…
 
Na pia ukitazama, kuna pande mbili za mwangaza…Kuna upande wa Nuru, na upande wa Giza, hivi navyo kila kimoja ni kinyume na mwenzake…Ndio maana urefu wa usiku ni sawa na wa mchana.
 
Lakini pia zipo pande mbili nyingine zilizo pacha zenye sehemu kubwa sana katika maisha…ambazo nazo zinafanana isipokuwa kimaumbile ni kinyume na mwenzake…nazo si nyingine Zaidi ya UZIMA na KIFO. Hivi vitu viwili ili Maisha yawe na maana ni lazima viwepo. Wengi hawafahamu kuwa Kifo ni sehemu ya uumbaji wa Mungu…Na kifo Mungu hakukiumba kwa bahati mbaya au kwa makusudi mabaya…Wala giza Mungu hakuliumba kwa madhumuni mabaya…Giza Lilivyoumbwa lilikuwa na kazi yake maalumu ya kiMungu na takatifu….Kadhalika Kifo kilivyoumbwa kilikuwa na kazi yake ya muhimu na takatifu, kifo kisingekuwepo Maisha yasingekamilika hapa duniani…Ni kama tu mkono wa kushoto ulivyoumbwa!…huwezi kusema mkono wa kushoto hauna kazi yeyote katika mwili wako, au mguu wa kushoto! Kadhalika Kifo kiliumbwa kwa kusudi maalumu..
 
Kifo kisingekuwepo, zile mboga na zile mbegu za matunda Adamu na Hawa walizokuwa wanakula pale bustanini zingemea tumboni mwao, kwasababu zingekuwa bado na uzima, hivyo ilimpasa aliue kwanza lile tunda kwa kulichuma kutoka katika shina la mti kisha alile lote…kadhalika Adamu na Hawa wasingeweza kuilima na kuitunza bustani ambayo Mungu aliwaambia waiilime na kuitunza, kwasababu hata nyasi ambazo wangezilima, zingekuwa mbichi vile vile daima, zisingekauka, na kufa na kupotea… hivyo miti na nyasi zingeendelea kuota duniani na dunia nzima ingekuwa ni misitu tu, ambayo inaendelea kuota na kuota, hata maana ya kulima ingekuwa haipo tena…
 
Kwahiyo ili kuweka usawa..dunia iweze kujisafisha na kulimika na kutunzika, Bwana Mungu alikiumba Kifo… kwamba ni lazima vitu vingine vife ili viache nafasi ya vingine vipya kuja lakini kwa utaratibu…kuwe na mzunguko wa namna hiyo…mti atapata uzima, lakini utapata pia kifo pia..n.k
Sasa Mwanadamu hakuumbiwa hicho kifo tangu Edeni, yeye alipoumbwa alipewa zawadi ya upande mmoja tu wa UZIMA. Kwamba ataishi milele…Lakini baada ya anguko Adamu na Mkewe Hawa, kuvunja maagizo ya Mungu…Kifo nao kikawaingia ambacho hakikupasa kiwe kwao, uzio ukaondoka wa wao kutopenya upande wa kifo…jambo ambalo halikuwa mpango wa Mungu…kwamba Mwanadamu aje na kupita…hivyo nao wakawa wanakufa kama mimea.
 
Lakini Yesu Kristo alipokuja, kwa kupitia Msalaba alikikomesha kifo…alisema katika
Yohana 11:25 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; 26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele”.
 
Na Yesu Kristo huyo huyo ndio NJIA YA UZIMA..Hakuna mwanadamu yeyote, wala mungu yeyote anayeweza kutibu kifo! Wala awezaye kumfufua mtu…usidanganyike kwamba kuna mungu wa dini yeyote duniani, ambaye anaweza kutoa tumaini la ufufuo wa wafu! Hakuna! Ni Yesu Kristo pekee, ambaye alikufa na akafufuka! Huyo ndiye anayeweza kufufua wafu na kukikomesha kifo…Yeye peke yake ndiye aliyetabiriwa kuwa atamweka adui wa mwisho chini ya miguu yake, ambaye adui huyo ni mauti. (1 Wakorintho 15:25-26).
 
Na hakuna namna yeyote tunaweza kuishi katika haya Maisha kama hatutakuwa na uhakika wa UZIMA WA MILELE…hivyo huu ni wakati wetu wa chagua uzima au mauti, lakini kumbuka Itatufaidia nini tuwe matajiri wa kupindukia, halafu tujue baada ya miaka 70 tunakufa! Na biashara yetu itakuwa imeishia hapo?…Ni heri kutafuta kwanza uzima wa Milele, na hayo mengine yatakuja…Ni heri sasa kutafuta mabilioni na mabilioni ya miaka isiyoisha ya kuishi…na hayo mengine nitayafanya nikishapata hayo mabilioni ya miaka isiyoisha…ndani ya hayo mabilioni ya mamiaka nitakuwa na muda wa kutosha pengine hata kutafuta hizo mali, kama kutakuwa na kutafuta mali…Lakini kutafuta mali na huku nina miaka 70 tu ya kuishi na baada ya hapo ni ziwa la moto! Hiyo sio akili wala hekima.
 
Tafuta uzima wa milele! Ambao huo unapatikana kwa Yesu Kristo pekee! Baada ya kifo.
 
Bwana akubariki sana.

Mada Nyinginezo:

MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.

TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.

JE, KAMA HAUNA UBATIZO SAHIHI HAUWEZI KUWA NA ROHO MTAKATIFU?

SANDUKU LA AGANO LILIKUWA LINAWAKILISHA NINI KATIKA AGANO JIPYA?

BWANA YESU ALIKUWA NA MAANA GANI KUSEMA CHAKULA CHA WATOTO USIWAPE MBWA KATIKA MATHAYO 15:21-28?


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments