Swali: Napenda kujua Daudi alikuwa na wake wangapi na je na sisi tunaruhusiwa kuwa na wake wengi?
Jibu: Mfalme Daudi alikuwa na wake nane (8), waliotajwa katika biblia, ambao ni..
Wake wengine aliokuwa nao hawakutajwa katika biblia, lakini alikuwa nao wengine wengi, pamoja na masuria (nyumba ndogo), aliowatwaa kutoka katika mji wake YERUSALEMU.
2Samweli 5:12 “Akajua Daudi ya kwamba Bwana amemweka imara awe mfalme juu ya Israeli, na ufalme wake ameutukuza kwa ajili ya watu wake, Israeli. 13 Naye Daudi akazidi kujitwalia masuria na wake huko Yerusalemu baada ya kutoka Hebroni; wakazaliwa zaidi kwa Daudi wana na binti. ”
2Samweli 5:12 “Akajua Daudi ya kwamba Bwana amemweka imara awe mfalme juu ya Israeli, na ufalme wake ameutukuza kwa ajili ya watu wake, Israeli.
13 Naye Daudi akazidi kujitwalia masuria na wake huko Yerusalemu baada ya kutoka Hebroni; wakazaliwa zaidi kwa Daudi wana na binti. ”
Lakini swali ni je!, kama Daudi alioa wake wengi, basi na sisi ni halali kuoa wake wengi?..
Jibu ni la!, ikiwa ni halali sisi kuoa wake wengi kwa kumwangalia Daudi, basi ni halali pia na sisi kuua kwasababu Daudi pia aliua!..lakini kama si halali kuua basi vile vile si halali kuoa wake wengi, kama Bwana wetu YESU KRISTO alivyotufundisha…
Mathayo 19:4 “Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, 5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? 6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe”
Mathayo 19:4 “Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe”
Hivyo ndoa ni ya mke mmoja na mume mmoja, kwa urefu Zaidi fungua hapa >>>JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI AU KUTOA TALAKA?
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Swali: Je idadi ya askari waliohesabiwa katika 1Nyakati 21:5 na 2Samweli 24:9 inajichanganya?.
NIFANYE NINI ILI NISILALE NINAPOSOMA BIBLIA.
VIGEZO VYA KUWA KARIBU NA YESU KRISTO KATIKA ULIMWENGU UJAO.
Vyemba ni nini kama tunavyosoma katika 2Samweli 18:14
JE! UNAWEZA KUWA NA GEUKO KAMA LA DAUDI?
Rudi Nyumbani
Print this post