Vyemba ni nini kama tunavyosoma katika 2Samweli 18:14

Vyemba ni nini kama tunavyosoma katika 2Samweli 18:14

Vyemba kama lilivyotumika hapo ni mkuki.

Absalomu mwana wa Daudi alipomwasi baba yake, na kusababisha vita vikubwa katika Israeli, Tunasoma, alipokuwa vitani, akiwa amepanda mnyama wake, alipita chini  ya mti mmojawapo akanaswa, mnyama alipoendelea mbele yeye akabaki ananing’inia pale pale, pasipo mafanikio yoyote ya kujinasua, baadhi ya askari wa Daudi walipomwona waliogopa kumuua, kufuatana na kiapo cha Daudi alichowaagiza wasimuue. Lakini jemedari wa mfalme aliyeitwa Yoabu yeye alikaidi amri, na kwenda kumwua kumpiga hivyo vyemba vitatu, moyoni. Kisha akamaliziwa na wasaidizi wake.

2Samweli 18:14 Ndipo Yoabu akasema, Siwezi kungoja na kusema nawe hivi. Akachukua vyemba vitatu mkononi mwake, akamchoma Absalomu moyoni, alipokuwa akali hai katikati ya ule mwaloni.  15 Kisha vijana kumi, waliomchukulia Yoabu silaha zake wakamzunguka, wakampiga Absalomu, na kumwua

Hivyo Yoabu alimchoma mikuki mitatu Absalomu kifuani mwake.

Lakini katika habari hii tunajifunza nini?

Upendo wa Daudi kwa mwanae ni sawa na Upendo wa Mungu kwetu sisi. Ijapokuwa Absalomu alimuudhi sana baba yake mpaka kumvunjia heshima ya kulala na wake zake, na kuuasi ufalme wake mtukufu, Daudi bado moyo wake ulikuwa kwa Absalomu kutaka atubu. Lakini Absalomu mwenyewe hakutaka, na hivyo alikutana na majeshi yakamwangamiza kwa tabia zake za uasi ulioendelea.  Laiti angekuwa mtoto mtii, asingekufa kwasababu baba yake angeweza kumlinda.

Tunapomwasi Mungu, tunajitenga na rehema zetu wenyewe, Kama vile Yona alivyosema katika (Yona 2:8),. Kamwe usimwasi Mungu ndugu, tembea katika njia zake, kwasababu hakika huko unapokimbilia kifo kipo. Na utakapovamiwa na adui yako ibilisi Mungu hataweza kukutetea kwa lolote. Utakufa na kuangamia milele kwa vyemba hivyo rohoni.

Nje ya Kristo hakuna usalama. Mrudie Mungu wako, kwa kumfuata Bwana Yesu, Tubu dhambi zako leo, ubatizwe, upokee ondoleo la dhambi zako. Uishi maisha ya neema siku zote ndani ya pendo lake. Acha uasi, neema haitadumu kwako daima kukulinda katika hiyo mitego adui anayokutegea kila siku akuue.

Je ungependa kuupokea wokovu leo? Kwa Yesu kuwa mwokozi wako na mtetezi? Kama ni ndio basi fungua hapa kwa mwongozo huo wa Sala ya Toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:

ANGALIA UZURI WAKO, USIGEUKE KUWA KITANZI CHAKO.

UVUMILIVU NA MIKAKATI YA ABSALOMU, INA FUNZO NYUMA YAKE.

MJUMBE ASIYEKUWA NA UJUMBE.

NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?

Je idadi ya askari waliohesabiwa katika 1Nyakati 21:5 na 2Samweli 24:9 inajichanganya?.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments