Epafra ni nani katika biblia? (Wakolosai 1:7)

Epafra ni nani katika biblia? (Wakolosai 1:7)

Epafra ndiye alikuwa mwangalizi wa kanisa la Kolosai, Paulo alimtambua  kama mhuhudumu mwaminifu wa Kristo. Kiasili naye pia alikuwa mwenyeji wa mji huo huo wa kolosai kufuatana na kauli Paulo aliyoisema katika Wakolosai 4:12, “aliye mtu wa kwenu”

Waraka huu unaonyesha Epafra kama  mhudumu ‘mwaminifu’ wa Kristo. Ikiwa na maana alijitoa kikamilifu kwenye kazi ya Mungu bila kupunguza chochote, mtumwa aliyegawa posho kwa wakati.

Aliyeitwa pia mjoli wa Paulo. Ikimaanisha mtendakazi pamoja na Paulo katika shamba la Bwana.

Lakini pia Paulo alikuwa ni kiongozi na mshauri wake. Tunaona aliwasilisha ripoti zake kwake, za maendeleo ya kanisa. Jinsi upendo wao ulivyokuwa mwingi.

Wakolosai 1:7  kama mlivyofundishwa na Epafra, mjoli wetu mpenzi, aliye mhudumu mwaminifu wa Kristo kwa ajili yenu

8  naye alitueleza upendo wenu katika Roho.

Epafra alikuwa na juhudi sio tu kwa kanisa la Kolosai, bali pia na makanisani mengine ambayo ni  Laodikia na Hierapoli (Wakolosai 4:13).

Tunasoma pia Epafra alikuwa mtu wa bidii  ki-maombi kwa ajili ya kanisa la Kolosai

Wakolosai 4:12  Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu katika maombi yake, ili kwamba msimame wakamilifu na kuthibitika sana katika mapenzi yote ya Mungu.

13  Maana namshuhudia kwamba ana juhudi nyingi kwa ajili yenu, na kwa ajili ya hao walioko Laodikia, na kwa ajili ya hao walioko Hierapoli.

Lakini mbeleni katika waraka wa Paulo kwa Filemoni tunaona alikuja pia kufungwa, pamoja na Paulo kule Rumi.

Filemoni 1:23  Epafra, aliyefungwa pamoja nami katika Kristo Yesu, akusalimu;

Ni nini tunajifunza katika maisha ya Epafra?

Kujitoa kwake kimaombi, kwa kanisa ili lisimame kamilifu na kuthibitika katika mapenzi ya Mungu. Epafra alikuwa na juhudi isiyo ya kawaida katika kuliombea kanisa. Alijua kanisa lisipoombewa haliwezi kusimama vema. Hivyo aliwekeza sana katika maombi na kuwa pia na bidii katika uaminifu kwenye  huduma.

Bidii yake hakika ilizaa matunda, na ndio maana Bwana akaruhusu habari zake ziandikwe, na kusomwa hadi leo.

Je! Na sisi tunathamini maombi katika kuliombea kanisa? Unapoona watu wamepoa kiroho, watu wanaishi kimwili kanisani, wanafanya mambo ya aibu, sio kumnyooshea kidole mchungaji, au shemasi au mzee wa kanisa na kumlaumu. Hapo huwezi tatua tatizo. Shida ipo kwenye kupungukiwa kwa maombi. Chukua muda mwingi kuliombea kanisa kuliko kuzungumza. Bwana atayatenda yote uliyoyatamani.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Nini maana ya kuabudu malaika? (Wakolosai 2:18)

Nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho,

UAMINIFU NI KIGEZO KIKUBWA CHA KUTUMIWA NA MUNGU.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments