Je! Habari iliyo katika 1Nyakati 21:25, na 2Samweli 24:24, ya Daudi kununua kiwanja  inajichanganya?

Je! Habari iliyo katika 1Nyakati 21:25, na 2Samweli 24:24, ya Daudi kununua kiwanja  inajichanganya?

SWALI:  Ni ipi gharama sahihi ambayo Daudi aliilipia, kununulia shamba la Arauna, kwa ajili ya kumjengea Mungu hekalu. Je! Ni shekeli 600, au shekeli 50?. Je! Biblia inajichanganya.

JIBU:  Tusome,

2Samweli 24: 24 Lakini mfalme akamwambia Arauna, La, sivyo; lakini kweli nitavinunua kwako kwa thamani yake; wala sitamtolea Bwana, Mungu wangu, sadaka za kuteketezwa nisizozigharimia. Hivyo Daudi akakinunua hicho kiwanja cha kupuria na wale ng’ombe kwa shekeli hamsini za fedha.  25 Naye Daudi akamjengea Bwana madhabahu huko, akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Basi Bwana aliiridhia nchi, na tauni ikazuiliwa katika Israeli.

1Nyakati 21:25 “Basi Daudi akampimia Arauna thamani ya mahali pale shekeli mia sita za dhahabu kwa uzani  26 Kisha Daudi akamjengea Bwana madhabahu huko, akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, akamlingana Bwana; naye akamwitikia kutoka mbinguni kwa moto juu ya madhabahu hiyo ya sadaka ya kuteketezwa”

Vifungu hivyo havijichanganyi,  vyote vipo sahihi. Mwandishi wa kitabu cha Samweli anaeleza lile eneo ambalo lilikuwa ni la kupuria tu, pamoja na wale ng’ombe gharama zake jumla ndio shekeli hamsini, lakini sio eneo lote la kiwanja. Tukirudi kwenye 1Nyakati mwandishi anaeleza sasa eneo lote, anatumia neno “mahali pale”. Kwamba jumla yake yote ni shekeli mia sita. Gharama zote za mahali pale zilikuwa ni shekeli 600

Kwamfano wewe unaweza ukawa umelenga kupanunua mahali Fulani kwa ajili ya shughuli zako za kimaendeleo. Lakini ikakugharimu ununue sehemu yote ili uweze kupamiliki vizuri na pale. Hivyo kama eneo lile tu moja gharama yake ilikuwa milioni 1, Lakini kwasababu ya kulipia fidia kwa watu kando kando kuwahamisha, na kodi, na ukarabati n.k. unajikuta unaenda mpaka milioni 20.

Ndicho kilichomkuta Daudi.

Kwahitimisho ni kuwa vifungu hivyo vipo sahihi havijichanganyi.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mada Nyinginezo:

Swali: Je idadi ya askari waliohesabiwa katika 1Nyakati 21:5 na 2Samweli 24:9 inajichanganya?.

Biblia inamaana gani iliposema “Dhambi ilipozidi, Neema ilizidi kuwa nyingi Zaidi”.

KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?

NI KWANINI WATU WENGI WANASHINDWA KUMWELEWA MUNGU?

Je Kauli ya Mungu katika Warumi 11:4 na 1Wafalme 19:18 inajichanganya?.

Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake?

Novena ni nini? Na je ipo kibiblia?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments