Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake?

Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake?

SWALI: Nini maana ya Neno hili; Mithali 22:29 “Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo”.


JIBU: Neno la Mungu linatuonyesha kuwa ‘bidii’ humkweza mtu. Na bidii inayozungumziwa kibiblia ni zaidi ile inayodhaniwa kufanya tu kazi sana kwa muda mrefu, hapana, bali ni pamoja na kutumia ujuzi wako wote na ufanisi ili kutimiza kusudi ulilowekewa ndani ya muda. Watu wa namna hii mara nyingi huwa wanateka macho ya  watu wenye vyeo au wakuu wa nchi.

Kwamfano Wafanyakazi wanaoonyesha ufanisi katika utendaji kazi, na kutimiza malengo ya shirika lao ndani ya wakati waliowekewa, huwa wanapendwa na ma-boss wao, na mara nyingi hupandishwa vyeo kama sio kupewa zawadi. Wagunduzi wa mipango ambayo inaleta mabadiliko chanya kwenye jamii, huwa wanaalikwa na viongozi wakubwa na maraisi kupongezwa na wakati mwingine kufanywa washauri wao.

Vivyo hivyo kiroho pia, ili tupate kibali kwa aliye Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana, zaidi ya wakuu wote duniani (yaani YESU KRISTO), hatuna budi kuwa na bidii katika kumtumikia yeye, na kuyafanya mapenzi yake.

Anasema,..

Kumbukumbu 28:1 Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, KWA BIDII, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; 

Umeona? Tusipokuwa walegevu, Bwana atatunyanyua juu sana tena sana kwasababu ni ahadi yake na haiwezi kutanguka..

Warumi 12:11  ‘kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;’

Hivyo, hakikisha, kile  ulichopewa na Bwana unakitendea kazi, zaidi sana angalia ni kwa namna gani utakiweka ili kilete matokeo mazuri katika ufalme wa Bwana, usikifanye bila maarifa, hakikisha unatumia vyote yaani; nguvu zake zote, akili zako zote, roho yako yote, na moyo wako wote kwa pamoja bila kusahau kimoja wapo, ndani ya muda huu mchache uliopewa na Mungu hapa duniani. Na hakika kitakapochipuka kama Bwana alivyokusudia, Bwana atakutukuza sana.

Bwana akubariki.

Lakini ikiwa upo nje ya Kristo, tambua kuwa bado huwezi kumtumikia Bwana, na hata ukifa sasa ni moja kwa moja unaenda katika jehanamu ya moto. Kwanini usiyapange upya maisha yako leo kwa kufanya uamuzi wa busara wa kumkabidhi Kristo maisha yako?

Ikiwa upo tayari kufanya hivyo sasa, basi fungua hapa kwa mwongozo huo wa sala.>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Nini maana ya Mithali 27:21  inaposema “mtu hujaribiwa kwa sifa zake?”

Nini maana ya Mithali 5:15-18 anaposema Unywe maji ya birika lako mwenyewe?

USINIPE UMASKINI WALA UTAJIRI. (Mithali 30)

Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake?

TULITAFUTE KWA BIDII TUNDA LA ROHO.

HAKUVAA NGUO SIKU NYINGI.

KUWA MAKINI, HATUA ZA UNYAKUO ZINAENDELEA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments