Nini maana ya Mithali 5:15-18 anaposema Unywe maji ya birika lako mwenyewe?

Nini maana ya Mithali 5:15-18 anaposema Unywe maji ya birika lako mwenyewe?

Mithali 5:15 “Unywe maji ya birika lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako.  16 Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu?  17 Yawe yako mwenyewe peke yako, Wala si ya wageni pamoja nawe.  18 Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako”


JIBU: Mstari huu unawalenga wanandoa, na unafananisha tendo la ndoa kama kisima ambacho kila mwanandoa amekichimba kunywea maji yake hapo ili kukata kiu ile ya mwili. Na kwamba mtu anapoingia katika hali hii, hawezi kunywa maji ya visima vingine na mwingine hawezi kuja kunywa maji ya kisima chake. Kwani vimeundwa mahususi kwa wale tu waliovichimba yaani wanandoa, mwingine yoyote atakayeshiriki ni mauti.

Jambo ambalo ni kweli, madhara ni mengi ambayo mtu anayapata anapotoka nje ya ndoa yake na kukutana na watu wengine kuzini nao, migogoro mingi ya kindoa inayozuka hata kupelekea kuvunjika kwa ndoa zao, wengine hata kuuana ni kwasababu ya tabia hii ya kuingilia ndoa za watu au kutoka nje ya ndoa. Magonjwa yasiyositibika kama ukimwi huingia kwa namna hii.

Na zaidi ya yote mtu afanyaye mambo kama haya ni anakwenda kinyume na agizo la Mungu ambalo litampelekea kuhukumiwa na kutupwa katika ziwa la moto atakapokufa; Maandiko yanasema.

Waebrania 13:4  “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu”.  

Kaa mbali na uzinzi, chimba kisima chako mwenyewe, (Oa au Olewa na mke au mume mmoja). Utulie hapo, epuka tamaa. Siku hizi ni za mwisho Yesu anakaribia kurudi,  mlango ni mwembamba unaoelekea uzimani  imekuwa kawaida, kwa mtu kuwa na wake kando, wakidhani kuwa ndio wamekamilika, hawajui kuwa ibilisi ameshawanasa, ulinzi wa Mungu umeshaondoka ndani yao, wapo hatarini kufa, kuzimu ikiwangojea, Je! Umejiandaaje na jambo hilo?  Ikiwa upo tayari kutubu leo dhambi zako na kuachana na hizo tabia za ibilisi, ili Yesu akusaidie kushinda dhambi basi uamuzi huo ni wa busara, waweza kufungua hapa kwa mwongozo huo wa kuokoka >>>>    KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

MAFUNDISHO YA NDOA.

BIRIKA LA SILOAMU.

Birika ni nini?, na yale Matao matano katika birika la Bethzatha ni nini?.

Kisima cha joka na lango la jaa ni nini?(Nehemia 2:13)

Biblia inamaana gani inaposema ‘tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao’?

“Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia;Achukiaye mambo ya dhamana yu salama

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments